Watu wasiopungua 7 wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa katika
mlipuko uliotokea kwenye gari la abiria maarufu kwa jina la 'matatu' mjini Nairobi, Kenya.
Polisi ya
Nairobi imetangaza kuwa, mlipuko huo umetokea kwenye eneo la Eastleigh ambalo
linakaliwa na Wakenya wenye asili ya Kisomali. Hadi sasa haijafahamika ni
kikundi gani ambacho kilitekeleza shambulio hilo la bomu la kutegwa ndani ya
basi la abiria.
Kwa upande mwengine, watu wasiopungua 18 wamejeruhiwa kufuatia machafuko yaliyotokea muda mchache
baada ya kutokea mlipuko wa basi la abiria la 'matatu' mjini Nairobi. Taarifa
zinasema kuwa, wengi kati ya majeruhi hao walikuwa wamechomwa visu na wengine
wakiwa na majeraha yaliyotokana na kupigwa mawe.
Maduka kadhaa ambayo ni ya
Wasomali yalilengwa katika mashambulio hayo ambapo vijana wa Eastleigh walikuwa
wakiwatuhumu Wasomali hao kwamba, ndio waliohusika na mlipuko wa basi la abiria
la 'matatu'.
EmoticonEmoticon