Wapalestina wasiopungua 23 wameuwawa jana katika Ukanda wa
Gaza huku mapambano makali kati ya Israel na wanamgambo wa kundi la Hamas
yakizidi kupamba moto.
Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema
wengi wao walikuwa watoto. Idadi ya watu waliouwawa katika mzozo huo uliodumu
siku tano sasa, imefikia 69. Israel imesema mfumo wake dhidi ya makombora
umeyaangusha maroketi mawili yaliyovurumishwa kutoka Ukanda wa Gaza katika anga
ya mji wa Tel Aviv.
Waisraeli 3 wameshauwawa na maroketi kutoka Gaza tangu
Jumatano iliyopita. Ongezeko la machafuko linakuja huku waziri mkuu wa Israel,
Benjamin Netanyahu akionya kwamba nchi hiyo iko tayari kuitanua harakati yake
ya kijeshi.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon jana ameitaka Israel
na Hamas kushirikiana na Misri kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.
EmoticonEmoticon