MSANII wa filamu na
tamthilia bongo Rayuu, inadaiwa kuwa amepewa mchongo mkubwa wa pesa ndefu
endapo atakubali kushiriki kwenye picha ya ngono huko Afrika Kusini ambayo
inashirikisha nyota kibao wa ndani ya Afrika.
Inadaiwa kuwa msanii huyo ameonekana na watu hao baada picha
zake kadhaa kuzagaa kwenye mtandao ndipo wapoliamua kumtumia ujumbe kwa njia ya
mtandao, na kama atakubali basi atakula mshiko ambao hajawahi kuukamata tangu
alipodhaliwa.
Chanzo kikubwa cha kuaminika kilichofanya upekuzi huo,
kilibaini ukweli kwamba msanii huyo anachati na watu hao lakini hajawaweka wazi
kama ataweza kufanya ishu hiyo ambayo itambidi asafiri.
Mpekuzi wetu alitumia muda wa saa kadhaa kukaa na msanii
huyo na kumdadisi lakini hakupewa chochote na inadaiwa kuwa ishu hiyo ipo na
watu wanamtaka kutokana na uzuri wake, pia wameona ni mtu ambaye hana aibu
baada ya kuziona baadhi ya tattoo kwenye makalio yake.
“Inadaiwa kuwa jamaa walichokipenda kwanza ni msanii pia
hana aibu kwani aliweza kuchora tatoo, lakini sijui kama msanii huyo amewajibu
kwani habari nilizonazo tena nimeona kupitia macho yangu ni hizo, asa sijui ni
watu wanamzingua au vipi,” alisema mpekuzi wetu.
Hata hivyo alipotafuwa Rayuu kuulizwa juu ya ishu hiyo
alibaki kuchecheka na hakuna chochote alichozungumza zaidi ya kudai kuwa kuna
watu wamemtumia mail ya kumtaka akacheze picha hizo kwa dau kubwa lakini
hajawajibu kwani anahisi wanataka kumuharibia mipango yake ya maisha kwa madai
hiyo kitu ambayo hawezi kufanya katika maisha yake.
EmoticonEmoticon