Muimbaji wa nchini Kenya Nyota Ndogo amekanusha info na udaku ulioenea sehemu mbali mbali afrika Mashariki kuwa ni mjamzito.
Mama huyo wa watoto wawili na mwenye miaka 31 aligeuka kuwa
gumzo kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na madai kuwa anategemea kupata
mtoto wa tatu.
Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Mwanaisha Abdallah
alikiambia kituo kimoja cha radio mjini Mombasa kuwa, “Nimenepa tu na nipo
kwenye hatua katika maisha yangu ambapo nimerelax. Ni mapema mno kwangu kuwa na
mtoto wa tatu. Mtoto wangu wa pili ndio ana miaka miwili sasa.”
EmoticonEmoticon