Polisi ya Misri imewatia mbaroni watu 120 waliokuwa
wakiandamana karibu na medani ya Tahrir mjini Cairo.
Taarifa zinasema kuwa
polisi ya Misri imetangaza kuwa watu hao wamekamatwa katika machafuko
yaliyojiri kati ya waandamanaji na askari usalama. Pia zaidi ya watu 60
wamejeruhiwa kwenye ghasia hizo kati ya waandamaji na vikosi vya polisi.
Waandamanaji hao walikuwa wakitaka Rais Muhammed Morsi wa Misri awapandishe
kizimbani wale wote waliohusika katika mauaji ya raia wakati wanajeshi
walipokuwa wakitawala nchi hiyo baada ya kuangushwa utawala wa dikteta Hosni
Mubarak.
Maandamano hayo yalianza Jumatatu ikiwa ni mwaka mmoja tangu kutokea
machafuko kati ya wanamapinduzi na askari polisi, ambapo watu 42 waliuawa.
EmoticonEmoticon