REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

TAARIFA: HUU NDIO UFAFANUZI WA RAPPER PREZZO KUHUSU KUBAKWA

5:53:00 AM

 Na Hezron Munisi  

#WatuWaMungu kama utakuwa umetembea katika mitandao kadhaa ya Kijamii, utakuwa unafahamu vizuri kuhusu taarifa za Msanii kutoka Nchini Kenya, PREZZO kuwa amepelekwa Hospitali baada ya Kubakwa na Wanawake Watatu Nchini Humo

Taarifa hizo zimeibuka hivi karibuni kuwa Hitmaker huyo wa “PREZZO” kutoka katika Mitandao miwili kutoka Nchini UGANDA na Mwingine kutoka Nchini TANZANIA , kuwa Rapper huyo amefanyiwa tukio hilo baada ya kuwekewa madawa ya Kulevya aina ya COCAINE.

Tofauti na hilo, pia mitandao hiyo imefafanua kuwa, Prezzo hakuwekewa Dawa za Kulevya tu, bali hata zile za kuongeza nguvu za kiume aina ya VIAGRA, kitu ambacho yeye mwenyewe amekikanusha na kuongeza kuwa hakuna kitu kama hicho na wala hayuko hiospitali

Tunamnukuu
“ Niko salama kabisa, na wala sipo hospitali. Taarifa hiyo ni Uwongo Mtupu na imetengenezwa na watu ambao wana mpango wa kuharibu jina Langu”



Katika hatua Nyingine, Pia Prezzo amesema kuwa hiyo ni sehemu ya Njama za kutaka kumuondoa katika Malengo yake ya kugombea katika uchaguzi wa mwaka 2022

“ Ukikaa Mbali na watu, huwa wanatafuta aina ya taarifa za Uwongo kuzungumza kuhusu wewe. Nimejikita katika Mlengo wa Kisiasa hivi sasa. Nina uhakika wa Asilimia MIA MOJA NA KUMI kuwa nitawatumikia Wananchi wa Kenya 2022”

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER