REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

JAMANI JAMANI JAMAAAANIIIII !!!: AMEJIUA KISA SNAPCHAT

2:33:00 AM

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu hili linmaweza kuwa ni Tukio la kwanza kabisa kufanyika Snap Chat ikiwa ni mara nyingi sana matukio haya huwa yanafanyika Kupitia mitandao Mingine ya Kijamii

Bruno Monteiro mwenye miaka 30, aliamua kujiua kwa kujirusha katika Daraja la RIO NITERIO huko huko Nchini Brazil kwa sababu aliingia katika Ugomvi Mzito na Mke wake kabla hajaamua kujiua

Taarifa ambazo tumezipata na hata kupitia Video Clip ambayo ilimuonesha Bruno ambaye pia ni Msanii kutoka Huko huko Brazil, ni kwamba kwa siku kadhaa amekuwa katika mgogoro wa Kimahusiano  na Mke wake Huyo, kitu ambacho kilimfanya alalamike mara kadhaa kupitia Mitandao ya Kijamii

Katika Hali nyingine, inasemekana kuwa, ugomvi mkubwa ilikuwa ni Mtandao wa Snap Chat ambao Mke wake amekuwa akiutumia vibaya, ikiwemo kujianika kwa wanaume wengine, lakini pia amekuwa akiutumia mtandao huo huo kufanya Biashara ya Ngono kitu ambacho kilimkwaza sana Marehemu

Baada ya kuona Mke wake amemblock kupitia Snapchat, aliamua kuchukua jukumu la kujiua na kuanika moja kwa moja kupitia Snapchat huku akidai kuwa chanzo kikubwa ni mtandao huo huo.

Ingawa baadhi ya Madreva piki piki na wasamalia wema kujitahidi kumzuia, Bruno alitupa Simu Chini na kisha kujirusha ikiwa ni baada ya kutoa malalamiko yake huku akiutuhumu Mtandao wa Snapchat kuwa kama chanzo cha hayo yote Kutokea

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER