SIKU ya Jana, Ulimwengu Mzima
ulikuwa katika kumbu kumbu ya kumpoteza Mfalme wa POP, Marehemu Michael
Jackson, ambaye alifariki JUNI 25, 2009.
Katika Kukumbuka Mengi ambayo
Michael aliyafanya ama kuchangia katika Kuboresha Ulimwengu wa Muziki kwa
Baadhi ya wasanii, Beyonce ni Moja kati yao, ambaye kuna machache ya Msingi
sana hatoyasahau kutoka kwa Wacko Jacko…
Akiandika Maelezo Kadhaa katika
Website yake, BEYONCE ambaye hivi sasa bado anatisha na kwaju lake la DRUNK IN
LOVE, alisema kuwa, Marehemu Michael alimbadilisha kwa Kiasi kikubwa, na
Kumfanya Awe Msanii ambaye hivi sasa anaonekana kuwa.


Aidha Beyonce aliongeza kuwa,
Michael alimfundisha kuwa, Kuna Muda unatakiwa Kusahau kabisa kuhusu Mbinu
zako, kusahau kile ulichonacho, bali kuzingatia ni nani ambaye uko naye,
anayekukubali, na kumwaga hata machoi kwa ajili yako.
Beyonce amemalizia kwa kumshukuru
sana Michael jackson kwa Kumfanya awe msanii Mkubwa hivi sasa.
EmoticonEmoticon