Huko Ujerumani, msemaji wa
serikali amesema kuwa anaheshimu kazi kubwa iliyofanywa na Papa huyu
aliyezaliwa katika Jimbo la Bavaria la nchini humo.
Papa Benedict
Baba Mtakatifu ameelezea kwamba
matatizo ya kiafya yamemfanya kutangaza kujiuzulu
Waziri Mkuu wa Uingereza David
Cameron, amemsifu Papa kwa jitihada zake za kuimarisha mahusiano baina ya
Vatican na Uingereza.
Askofu mkuu wa Canterbury amesema
amazipokea taarifa za kujiuzulu kwa Papa kwa huzuni mkubwa ingawa anaelewa
undani wa hatua yake.
Kiongozi wa Ujeremani, Bi. Angela
Merkel amesifu mchango wa Papa wa kupendekeza mjadala baina ya makanisa,
waislamu na wayahudi.
Alikumbusha hotuba ya Papa
alipozuru bunge la Ujerumani mnamo mwaka 2011.
Uwamuzi na hatua ya Papa Benedict
XVI wa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya takriban miaka minane
akiongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni mkubwa kiasi
kwamba hawezi kuendelea kuhudumu zaidi ya umri huo.
Makao makuu ya Kanisa Katoliki
huko Vatican yanasema yanatarajia Papa mpya atachaguliwa kabla ya mwisho wa
mwezi wa tatu, na sherehe za Pasaka.
Tabia ya kujiuzulu kwa Papa si
ngeni, ingawa ni tukio jipya katika karne za hivi karibuni.
EmoticonEmoticon