Mamlaka ya
Uthibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na majini( Sumatra) Mkoani Mbeya
imesitisha  utoaji wa leseni ya kubeba
abiria  wa kawaida kwa waombaji wapya
wenye magari yenye uwezo wa kubeba abiria 
wasio zidi 14.
Aidha  Mamlaka hiyo imesema kuwa endapo wamiliki hao
wa magari hayo watahitaji kutoa huduma kwa jamii mamlaka hiyo itatoa  leseni kwa ajili ya kubeba watalii tu .
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mbeya na Kamanda wa Polisi
Mkoani hapa Ndugu Diwani Athumani wakati akizungumza na madereva wa mabasi
madogo yaendayo Mji mdogo wa Tunduma Wilayani 
kufuatia kuwepo kwa mgomo uliodumu kwa miezi 3 sasa  ambao umefanywa na madereva hao kwa kuto
safirisa abiria waendao Tunduma.
 Mgomo huo wa
madereva hao umesababishwa na baadhi ya wamiliki wa magari madogo aina ya(
Noah) ambayo yamekuwa yakifanya shughuli ya kubeba abiria toka Mbeya hadi
Tunduma hali iliyo zua mgogoro mkubwa baina ya wamiliki wa gari hizo Ndogo
pamoja na madereva wa Costa ambao ndio wenye leseni za  kusafirisha abiria Toka Mbeya hadi Tunduma.
Awali wakati akizungumzana madereva hao Kamanda Diwani
amewataka mara moja watu wanaofanya biashara hiyo kuacha mara moja kwani sheria
itachukua mkondo wake.
Amesema sababu
kubwa ya kusitisa huduma inayo tolewa na magari hayo madogo ni kuzuia majanga
ambayo yanaweza kutokea kwani gari hizo hazina madirisha makubwa pamoja na
milango yake kuwa midogo ambayo na haina milango ya dharura endapo kunaweza
kutokea tatizo lolote.
Kufuatia  hali hiyo Kamanda Diwani amewataka madereva
costa ambao wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa muda mrefu kuachana  na mgomo huo badala yake waendelee kutoa
huduma kwa  wananchi kama ilivyo kuwa
awali.
MBEYA YETU 
EmoticonEmoticon