Majeruhi wakipatiwa Huduma ya Kwanza baada ya Ajali
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Abbas Kandopro akiwafariji Majeruhi wa Ajali Hiyo
Mheshimiwa Kandoro akichukua Maelezo kutoka kwa Mmoja wa Majeruhi
Majeruhi wakipatiwa Huduma ya Kwanza
Mheshimiwa kandoro akizungumza na Waandishi wa habari
Damu zilivyotapakaa katika Eneo la Ajali
Lori lilikuwa limewabeba Majeruhi na Marehemu katika Ajali hiyo mapema hii leo
Eneo la Ajali
Majeruhi wakiwa katika maumivu ya Ajali hiyo
WATU
watano wamepoteza maisha na wengine 130 wamejuruhiwa vibaya huku
hali zao zikiwa mbaya baada ya Lori walilokuwa wakisafiria shambani
kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Mapogolo kata ya
Itamboleo Wilayani Mbarali Mkoani hapa.
Ajali hiyo imetokea leo saa 1:30 asubuhi ambapo
lori hilo ambalo ni mali ya Mwekezaji
wa shamba la Kapunga Rice
Project, na kwamba watu hao walikuwa wakielekea kwenye shamba la
mwekezaji huyo lililkuwa limebeba vibarua hao zaidi ya 200 ambao ni
wakazi kitongoji cha Kapunga.
Lori
hilo lenye namba za uasjili T398 BSE Scania Tipa, ambalo lilikuwa
likiendeshwa
na dereva aliyejulikana kwa jina Baraka Moreli,
lilionekana likiwa katika mwendo kasi na dereva huyo
akiwa na lengo la kutaka kuipita pikipiki iliyokuwa mbele yake.
huku akishangiliwa na vibarua hao ipite ipite hiyo pikipiki haiwezi
kutushinda sisi gari kubwa moja ya majeruhi alisema. ndipo walipofika
kwenye kona dereva lilimshinda gari hilo na kupinduka
Akiwa Hospitalini hapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Abbas Kandoro ambaye aliweza kufika hospitalini hapo alisema kuwa
mara baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya
ya ,Mbarali Gullam Hussein Kiffuu, huku akiombwa kupatiwa msaada wa
kuongezewa madaktari, kuongezewa vifaa vya mataibu sambamba na
uwezekano wa kupata damu kwa ajili ya kuwaongezea majeruhi hao
alifanikiwa kuwasiliana na uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Mbeya,
hospitali ya Mkoa ili kuweza kuona namna ya kwenda kuokoa maisha
watanzania hao.
Kandoro, alisema kuwa katika ajali hiyo
wanaume wanne wamefariki na mwanamke mmoja. watatu wametambuliwa
Samweli Mapugilo mbena 30 mkazi wa Ilembula
Bon Mfupa 27 mkazi wa mapogolo na Edgar
Mwakipesile 35 mkazi wa Nonde Mbeya
Aidha,
Kandoro alisema kuwa idadi ya majeruhi katika ajali hiyo kuwa
ni 130 ambapo wanawake ni 40 na wanaume 89 huku idadi ya watoto
waliokuwa wameongozana na wazazi wao haikuweza kufahamika kwa haraka.
NA MBEYA YETU.
EmoticonEmoticon