Na Ahmad James Nandonde, MUSOMA
KIWANDA CHA MAZIWA CHA MARA (MARA MILK) MUSOMA KIMEPATA
HASARA
ZAIDI YA SHILLINGI MILIONI 8 ILIYOSABABISHWA NA ITILAFU YA
UMEME ILIYOTOKEA JANUARI 9 MWAKA HUU.
AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE LEO HII
MKURUGENZI MTENDAJI WA KIWANDA HICHO JAMES MATHAYO AMESEMA KUWA KIWANDA HICHO
KIMESIMAMA KWA MUDA WA SIKU MBILI KUTOKANA NA UHARIBIFU WA BAADHI YA VIFAA VYA
KIWANDA HICHO
AMESEMA KUWA BAADA YA ITILAFU YA UMEME KUTOKEA VIFAA VIWILI
VYA MOTO VILIUNGUA AMBAVYO ALIVITAJA KUWA NI HEATER ELEMENT YENYE GHARAMA YA
SHILINGI 3.6 NA PAMPU YAKUPOOZA MAJI CHILLER MACHINE YENYE THAMANI YA SHILINGI
MILLIONI 1.2. NA KWAMBA VINAPATIKANA NCHI JIRANI YA KENYA NAITAWALAZIMU
KUVINUNUA.
NAYE KAIMU MENEJA WA KIWANDA HICHO AMBAYE PIA NI PLAN
ENGENEER WA TANESCO MKOA WA MARA AMEKIRI KUWEPO KWA TATIZO HILO NA AMESEMA KUWA
WANATAMBUA MCHANGO WA KIWANDA HICHO KWA SHIRIKA LA UMEME MKOANI HUMO NA WAMEOMBA
RADHI KWA USUMBUFU HUO NA KWAMBA WANAENDELEA KULITAFUTIA UFUMBUZI.
AMESEMA KUWA ITILAFU HIYO IMETOKEA KUTOKANA NA KUANGUKA KWA
TRANSFOMA INAYOHUDUMIA KIWANDA HICHO NA TAYARI WAMEKWISHA BADILISHA NA KUWEKA
TRANSFOMA NYINGINE.
KIWANDA CHA MAZIWA MARA MILK KINAZALISHA MAZIWA YA MTINDI,
YOGATI, NA MAJI YA KUNYWA AINA YA SUPER WATER.
EmoticonEmoticon