Tume huru ya Uchaguzi na Uratibu wa Mipaka IEBC Jumapili imetoa tahadhari kuhusu kuwepo kwa vyeti bandia ambavyo inadai vimekuwa vikisambazwa jijini Nairobi na vinadaiwa kutolewa na tume hiyo.
Kulingana na IEBC vyeti vitatolewa na IEBC baada ya vyama kuwasilisha vyeti vya uteuzi, na wagombezi wa viti mbalimbali. IEBC inatarajiwa kutoa vyeti kwa wagombezi wa urais tarehe 29 na 30.
Watakaowania nyadhfa za ugavana, useneta na wawakilishi wa wanawake katika kaunti na wengine watawasilisha karatasi zao za uteuzi tarehe 31. IEBC imebaini kwamba vyeti hivyo bandia ambvyo vinasambazwa vina maelezo bandia ikiwemo sahihi ya mwenyekiti wa IEBC Isaac Hassan na baadhi ya wakuu wengine.
Tayari IEBC imewaarifu maafisa husika wa usalama na mshukiwa mmoja ametiwa mbaroni.
EmoticonEmoticon