Mwenyekiti wa Yanga FC, YUSUPH MANJI
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Kanuni
za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(4) katika
kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Januari 2013, ilijadili
pingamizi zilizowekwa dhidi waombaji uongozi wa TFF na TPL Board na
kutoa maamuzi kama ifuatavyo:
1.Waombaji
uongozi wa TPL Board
(a)Pingamizi
dhidi ya Ndg. Said
Muhammed Abeidanayeomba
kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL
Board): Kamati
ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na Ndg. Frank M.
Mchaki dhidi
ya Ndg. Said
Muhammed, aliyeoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF kumwondoa
mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Said
Muhammed:
(i) Si
Mwenyekiti wa Klabu ya Azam na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa
TPL Board.
(ii) Si
mkweli katika maelezo aliyoyatoa kwenye fomu yake ya maombi ya
uongozi.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilipitia maelezo ya Mweka pingamizi na
ilijiridhisha kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake na Ndg.
Mchaki haikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2)
kwa kuwa haikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo
ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa
pingamizi hiyo.
(b) Pingamizi
dhidi ya Ndg.
Yusufali Manji anayeomba
kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati
ilijadili pingamizi zilizowasilishwa na Ndg.
Daniel T. Kamna na Ndg. Juma Ally Magoma walioomba
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kumwondoa mwombaji uongozi
kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Yusufali
Manji :
(i) Hana
uzoefu wa
uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano
(5) wa
uendeshaji wa mpira wa miguu.
(ii) Hana
sifa ya kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki
katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi
daraja la kwanza.
(iii) Hana
elimu ya kidato cha nne
(iv) Ameshindwa
kusimamia katiba ya Young Africans Sports Club Ibara ya 10(6),
18(1)b, 27 (2) na (5).
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa
pingamizi zilizowasilishwa mbele yake na Ndg. Daniel T. Kamna na
Ndg. Juma Ally Magoma hazikukidhi
matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa
hazikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya
pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFFimezitupa
pingamizi hizo.
(c) Pingamizi
dhidi ya Ndg.
Hamad Yahya Juma anayeomba
kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati
ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na Ndg. Frank M.
Mchaki dhidi
ya Ndg. Hamad Yahya Juma,kwamba
Ndg. Hamad Yahya Juma:
(i) Si
Mwenyekiti wa Klabu ya Mtibwa na hivyo hana sifa za kugombea uongozi
wa TPL Board.
(ii) Si
mkweli na mwadilifu na amekuwa akijipachika cheo cha mwenyekiti wa
klabu.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF imeitupa
pingamizi ya Ndg.
Frank M. Mchaki kwa kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake
haikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya
11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo
ya pingamizi.
2. Waombaji
uongozi wa TFF
(a) Pingamizi
dhidi ya Ndg.
Athumani K. Kambi anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda
ya 9 (Mtwara na Lindi): Ndg. Kambi aliwekewa pingamizi kwamba
amefanya Kampeni kabla ya muda uliopangwa.
Kamati imeitupa
pingamizi ya Ndg.
Jeremiah John Wambura kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati
alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake
kuhusu pingamizi.
(b) Pingamizi
dhidi ya Ndg.
Eliud P. Mvella anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda
ya 7 (Iringa na Mbeya): Ndg. Mvella aliwekewa pingamizi na Ndg. Said
Kiponza, Ndg. Abu Changawa na Ndg. Peter Naminga, kwamba Ndg. Mvella:
(i) Akiwa
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda hiyo ameshindwa
kuleta maendeleo ya soka katika ukanda huo.
(j) Ana
kesi ya rushwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa
Kamati imeitupa
pingamizi hiyo
kwa kuwa haikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara
ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha
maelezo ya pingamizi.
(c) Pingamizi
dhidi ya Ndg.
Epaphra Swai anayeomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda
ya 3 (Shinyanga na Simiyu): Kamati ilijadili pingamizi
zilizowasilishwa na Ndg. Ramadhani Sesso na Ndg. Tsotsie
Chalamila, kwamba Ndg. Epaphra Swai:
(i) Alifanya
ubadhilifu wa fedha alipokuwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Mwanza (MZFA).
(ii) Alitumia
madaraka yake vibaya alipokuwa MZFA kujinufaisha kwa kutumia MZFA.
(iii) Alivunja
Katiba ya MZFA na FIFA
(iv) Anavuruga
shughuli za uendeshaji mpira wa miguu mkoani Simiyu.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa
wawekaji pingamizi hawakuwa na sababu za msingi zilizoambatana na
vielelezo vinavyothibitisha maelezo ya pingamizi na kuwa pingamizi
zilizowasilishwa mbele yake zina chembechembe za wazi za mapatano ya
hila na udanganyifu (collusion) dhidi ya Ndg. Epaphra Swai. Kwa
kutokidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) na
hila/udanganyifu kwa Kamati, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa
pingamizi hizo.
(d)Pingamizi
dhidi ya Ndg.
Vedastus F.K Lufano na Ndg.
Mugisha Galibona wanaoomba
kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda
ya 2 (Mwanza na Mara): Ndg. Lufano na Ndg.
Galibona waliwekewa pingamizi na Ndg. Paul
Mhangwa kwamba hawana
uzoefu wa
uendeshaji wa Mpira wa Miguu wa miaka mitano (5).
Kamati imeitupa
pingamizi hiyo kwa
kuwa haikuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).
(e) Pingamizi
dhidi ya Ndg.
Michael R. Wambura anayeomba
kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF: Pingamizi ziliwasilishwa na
Ndg. Said Rubea Tamim na Ndg. Josea Samuel Msengi kwamba Ndg.
Wambura:
(i) Alikiuka
Katiba ya TFF kwa kuishitaki Klabu yake ya Simba mahakamani kuhusu
masuala ya uchaguzi.
(ii) Alikosa
uadilifu kwa kutumia kampuni yake binafsi kufanya biashara na Taasisi
aliyokuwa aniongoza akiwa Katibu Mkuu wa FAT.
(iii) Amekuwa
akijaribu kupotosha umma kwamba vyombo vya TFF havifanyi kazi zake
kwa kutumia haki na kuviita ‘Mahakama za Kangaroo (Kangaroo
Courts).
(iv) Mwaka
2004 alikiri kwamba alikuwa akiandikwa vizuri na vyombo vya habari
kwa kuwa alikuwa akivipa pesa na kwamba vyombo vya habari vilimgeuka
kwa sababu aliacha kuwapa waandishi pesa.
(v) Mwaka
2004 alikataa kutekeleza maagizo ya FIFA ya kutaka nafasi ya Katibu
Mkuu wa FAT iwe ya kuajiliwa.
(vi) Alikosa
uwezo wa kutekeleza wajibu na malengo ya TFF.
Ndg.
Josea Samuel Msengi aliondoa pingamizi lake dhidi ya Ndg.
Wambura. Kamati imelitupa
pingamizi la Ndg.
Said Rubea Tamim kwa
kuwa halikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya
11(2).
(f) Pingamizi
dhidi ya Ndg.
Jamal E. Malinzi anayeomba
kugombea nafasi ya Rais wa TFF; Aliwekewa Pingamizi na Ndg. Agape
Fue kwamba:
(i) Alivunja
Katiba ya TFF kwa kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa
wanachama wa TFF kikiwemo Chama chake cha Mkoa wa Kagera haviheshimu
wala kutekeleza maagizo ya TFF, CAF, CECAFA na FIFA baada ya Kamati
ya Utendaji ya TFF kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba
kwa njia ya Waraka, ambayo yalihusisha pia maagizo ya FIFA
na CAF
(ii) Hana
sifa ya uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
(iii) Anakosa
uadilifu na haiba ya kuliwakilisha Shirikisho nje na ndani.
Kamati imeitupa
pingamizi ya Ndg.
Agape Fue kwa
kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye
Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu pingamizi hilo.
(g)Pingamizi
dhidi ya Ndg. Athumani J. Nyamlani anayeomba kugombea nafasi ya
Rais wa TFF: Ndg. Nyamlani aliwekewa pingamizi na Ndg.
Mintanga Yusuph Gacha na Ndg. Medard Justiniani kwamba:
(i) Ni
Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Tanzania na kwa maana hiyo ni
mtumishi wa umma hivyo alikosa kigezo na sifa ya kugombea nafasi ya
urais wa TFF.
(ii) Anakatazwa
na Judicial
Service Act, Public
Service Act 2002 na Code
of Conduct for Judicial Officers of Tanzania kugombea
nafasi aliyoomba ya Rais wa TFF.
(iii) Kutakuwa
na Mgoganao wa kimaslahi endapo Ndg, Nyamlani atachaguliwa kuwa Rais
wa TFF.
(iv) Amekosa
umakini na uadilifu kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na
kusababisha Akanunti za TFF kufungiwa na TRA.
Ndg.
Mintanga Yusuph Gacha hakufika kutetea Pingamizi lake ni hivyo
halikujadiliwa na Kamati. Kamati imelitupa
pingamizi la Ndg.
Medard Justiniani kwa kuwa alishindwa kuithibitishia Kamati kuwa
alikuwa na ufahamu wa kutosha wa pingamizi lake ikiwa ni pamoja na
viambatanisho vyake, hali iliyotanabaisha kuwa pingamizi hilo
lilikuwa na chembechembe nyingi za hila na udanganyifu.
Angetile
Osiah
KATIBU
KAMATI
YA UCHAGUZI
EmoticonEmoticon