REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

"ADAM JUMA ANATAKIWA KUKUA"-Q Chillah

10:17:00 AM
Na Frank M. Joachim "Hasta La Vista Baby"

Wengi sana tushazoea kusikia kuwa Q Chilla ana Bifu na Msanii Fulani...kutokana na Sababu Fulani..ila Hii sasa imekuwa ni nyingine kabisa kabisa.

Q-CHIEF Msanii wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania Maarufu kama Bongo Flava, Leo amempasukia Vilivyo Director wa Visual Lab, Adam Juma kwa Madai kuwa ameshindwa kumfanyia Video yake Mpya.

Kwa Mujibu wa "YOU HERD" ya XXL ya Clouds Fm inayokamatiliwa na GOSSIP COP Mwenyewe "Sudd Brown", Chiilah amediriki kumuambia ADAM kuwa antakiwa kukua na kufanya vitu vya kiutu uzima, kwani kamwe hatofanya nae kazi tena kutokana na Sababu hiyo.


Aidha kwa Mujibu wa Chief Kiumbe The Boss ambaye ndiye alilipia Video hiyo, amesema kuwa, yeye ndiye aliyeamua Gharama za Video ya Q-CHILLAH ambazo zilishakabidhiwa kwa Adam,kufanyia Video mpya Ya Shettah inayotambulika kwa BONGE LA BWANA kutokana na Maelezo aliyopata kwa Adam Mwenyewe kuhusu ugomvi wake na Chillah

"Adam alikuwa ameshashoot Video nzima ya Chilla, na kazi iliyobaki ilikuwa ni kumalizia kazi. Iloa kwa Mujibu wa Adam ni kwamba, Laptop yake ilidondoka chini kidogo na kupata Mushkeli, hali iliyosababisha baadhi ya Clips kutoonekana. Baada ya Adam kuona hivyo, alimtaarifu Chilah na Kumwambia kuwa inabidi waanze upya kabisa Video Nzima katika Kushoot, jambo ambalo inasemekana Chilla hakukubaliana nalo, na baadaye akamjibu Adam maneno makali na kuzua kutokuelewana baina yao wawili. Baada ya kuona Adam amegoma kufanya Kazi tena Chillah, ikabidi gharama zote ambazo nilimlipa kwa ajili ya Video ya Chillah zisiende hivi hivi, bali zitumike kutengeneza Video ya Shetta BONGE LA BWANA, na Kuzungumza na Q Chillah kuhusu ni wapi atapenda kufanyia Tena Video na mimi nitamgharamikia maana Chillah Ni Mtu wangu wa Kitambo tu." Alisema CHIEF KIUMBE

Kwa upande wake Chillah, huku akionekana kuwa na hasira haswa, alisema kuwa kamwe hawezi kufanya kazi tena na Adama, na asitegemee kuwa atashoboka na Rangi za Video ambazo zinawababaisha wasanii wengine, kwani bado baadhi yao wanaonekana na Sura mbaya licha ya kupoambwa na Rangi ambazo hazina Msingi.
HILI NI BIFU TAYARI?...au?

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER