Wananchi wameshauriwa kutekeleza agizo la Utalii kwa wote
kwa kuyatembelea maeneo mbali mbali ya utalii Zanzibar ili kufahamu historia ya
nchi ya Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa
Divisheni ya Makumbusho Zanzibar Khamis Abdallah Ali wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari katika ziara iliyojumuisha wanahabari na
maafisa wa Makumbusho.
Pia ameongeza kuwa katika kutekeleza agizo la Utalii kwa wote
wananchi wanapaswa kushajihishwa kutembelea maeneo ya kihistoria badala ya
kuwaachia watalii peke yao kufanya ziara katika maeneo hayo. Bw. Abdala amesisitiza kuwa ni jambo
la kusikitisha kuona wenyeji hawana hamu ya kujua historia ya nchi yao na
kuwafanya wageni kujua historia ya Zanzibar.
Aidha Mkuu huyo wa makumbusho amemaliza kwa kusema kuwa Idara ya
Makumbusho imeweka kiwango kidogo cha Shilingi 1000 ili kumrahisishia mwenyeji
pale anapohitaji kwenda kutembelea maeneo ya makumbusho kwa ajili ya kujua
historia ya nchi yao
EmoticonEmoticon