Na Francis Godwin
Mwanahabari mwingine
mkoani Dar es Salaam apigwa
risasi na askari polisi
ambao wanadaiwa kuwa
walikuwa wakimsaka mtuhumiwa wa ujambazi
mwanamke na kuishia kumpiga mwanahabari
huyo mwanaume Bw Shaban Matutu wa gazeti la Tanzania Daima.
Tukio hilo limetokea
jana majira ya saa 2 usiku jijini
Dar es Salaam ambapo askari hao
walipofika nyumbani kwa
mwanahabari huyo na kumgongea mlango na wakati akifungua mlango ndipo
Matutu amepigwa
risasi na Polisi, ambao wanadaiwa walikuwa wanamtafuta mhalifu ambapo katika
zoezi hilo, walienda na kugonga chumbani kwa Mwandishi huyo, kabla ya kutwanga
kwa risasi.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, mara baada ya tukio hilo,
mwandishi huyo amekimbizwa hospitali ya Mwananyamala ambako anaendelea kupatiwa
huduma ya haraka na inaelezwa kuwa, amejeruhiwa lakini hali yake si mbaya sana
Habari zaidi zitakujieni
Taarifa za uhakika na ambazo zimethibitishwa zinaeleza kuwa
jana usiku polisi mwenye silaha, aina ya bastola alimjeruhi begani kwa risasi,
mwandishi wa habari wa Tanzania Daima, Shaaban Matutu.
Risasi bado imenasa kwenye bega lake hadi sasa Matutu
alipigwa risasi nyumbani kwake Kunduchi, Dar es Salaam wakati askari
walipovamia nyumba yake kwa madai kwamba kuna kibaka aliingia kujificha
nyumbani hapo. Hivi sasa Matutu anatibiwa Mwananyamala hospitali, lakini
amepewa rufaa kwenda Muhimbili.
Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania Bw Absalom
Kibanda, ambaye amefanya jitihada za kumuhamishia Matutu Muhimbili, anasema
hali ya Matutu siyo nzuri na kwamba wanajipanga kwenda Muhimbili kuona iwapo
risasi hiyo itaondolewa mwilini.
Hata hivyo Kibanda ameeleza kusikitishwa kwake ni vitendo vya uvunjifu wa amani dhidi ya wanahabari nchini Tanzania ambavyo vimeendelea kufanywa na jeshi la Polisi nchini na kutaka polisi waliofanya
hivyo kuchukuliwa hatua kali.
Alisema wakati Taifa likiwa bado katika majonzi ya mauwaji ya
kinyama ya Mwandishi wa Chanel Ten mkoa wa Iringa Daudi Mwangosi
leo tunashudia tena unyama mwingine
dhidi ya mwanahabari huyo.
Hivyo iwapo jeshi
la polisi litakosa majibu juu ya sababu
ya kumpiga risasi mwanahabari huyo ambaye hata hivyo hakuwa mlengwa katika msako wao wa kumsaka mtuhumiwa wa ujambazi ambae ni
mwanamke basi itafika sehemu wanahabari nchini watalichukulia jeshi la polisi ni maeneo ya
hatari kwao
EmoticonEmoticon