WAKATI wadau wakizidi kuzitoa kasoro filamu za bongo msanii
Rayuu, amedai kuwa filamu nyingi zinazotengenezwa nchini hazina ubora na hazina
mvuto wa mtu kuziangalia, zinaongoza kwa ubaya ni zile zinachezwa na wasanii
wanaojiita bongo movie.
Ndani ya tasnia ya filamu Tanzania kuna makundi mawili na
kati ya hayo lipo moja la wasanii wanaojiita bongo movie ambao wanajiona ni
mastaa, pia kuna kundi lingine ambao si maarufu na ndilo linalojulikana kama
wasanii wa filamu.
Kutokana na makundi hayo msanii huyo kwa upande wake alidai
kuwa hayupo kwenye upande wa bongo movie, kwani kundi hilo limejaa majungu na
wasanii wake wanajiona ni mastaa kuliko wengine huku wakisahau kuwa tasnia ya
filamu ni moja.
Hata hivyo aliongeza kuwa uwepo wa filamu zisizo na ubora
unatokana na hayo makundi kwani kila mtu anataka kutoa filamu kila siku bila
kujua ubora wa kazi anayofanya na hii yote ni kutaka kushindani bila
kujuavushindani huo unaharibu soko kwa sababu ya kazi zisizo na ubora.
“Mimi si msanii wa bongo movie na ukiniita hivyo utakuwa
umekosea kuna kundi la wasanii ambao wanajiita bongo movie, lakini hata hivyo
unaweza kuona filamu zao si nzuri kama za wasanii wengine ambao hutumia muda
mrefu kutengeneza kazi moja, lakini wao kila baada ya wiki wanatoa filamu.”
alisema.
Hata hivyo alisema kuwa ubaya wa kazi hizo unakuja pale
unapokuta ndani ya filamu moja wamecheza watatu filamu nzima.
EmoticonEmoticon