Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
ameeleza sababu zinazosabisha kukosekana kwa umeme katika jiji la Dar es salaam
na maeneo mengine nchini.
Akiongea na Radio One asubuhi ya leo Mheshimiwa Muhongo
alisema lilikuwepo tatizo katika mfumo wa gesi ambao umerekebishwa zaidi ya
mara tatu na kusabasha gesi kukata.
“Tumeomba wataalamu wetu waangalie na ikiwezekana isitoke,
sasa ikishatokea namna hiyo inamaanisha kwamba watumiaji wa gesi wanaendelea
kutumia gesi iliyo kwenye hilo bomba, kama nyingine haiji inamaanisha pressure
inapungua kwahiyo wanahitaji muda wa masaa ili pressure irudi kuwa sawasawa, “
alisema.
“Tatizo la pili ilikuwa ni kwamba mitambo yetu ile ambayo
ilikuwa inatumia mafuta kama unavyojua kwa zaidi ya wiki mbili palitokea
mtafaruku mafuta yalikuwa hayapo na kama unavyofahamu mafuta ndo yameanza
kufika hata huko mikoani sehemu nyingi mafuta ndo yameanza kuwafikia watumiaji
kwahiyo haya matatizo mawili yote tumeyaangalia kwa makini sana nadhani
kwasababu ni vitu vinatokea mara kwamara tuna jitaidi visitusumbue tena.”
“Lakini umeme wetu mwingi hautokani na maji sasa hivi hilo
ndilo Watanzania wana paswa kufahamu, umeme wetu mwingi unatokana na gesi kati
ya asilimia 40 na 60 inategemea na uzalishaji wa siku hiyo ukoje alafu unafuata
umeme wa mafuta na mwisho kabisa unafuata umeme wa maji.”
Alieleza kuwa tatizo jingine ni la miundombinu ya kusambaza
umeme imechoka na hivyo kuhitaji marekebisho ya mara kwa mara.
“Miundombinu ni kwamba kweli imeshoka inahitaji muda kuweka
miundombinu mizuri ambayo ni ya kisasa kwamfano kuna sehemu ambazo sehemu moja
ikipata hitilafu karibu wilaya mzima inakosa umeme , saa zingine mkoa mzima
kwahiyo hiyo ni miundombinu ya kizamani na hilo tatizo mafundi wa Tanesco
wanajitaidi na Tanesco tumewaeleza kwamba wajitahidi sana kuwa wanakagua
miundombinu yao na kutengeneza.”
Aliongeza kwa kudai kuwa sababu nyingine kubwa ni wizi wa
miundo mbinu ya Tanesco ikiwa pamoja na wizi wa mafuta ya transfoma na nyaya za
umeme.
EmoticonEmoticon