MILIONI SITA zinahitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto
Selemani Said (1), ambaye anajisaidia haja kubwa kupitia utumbo mkubwa huku
ukiwa nje ya tumbo lake imeleezwa.
Akizungumza na wandishi wa habari Katika Ukumbi wa Idara ya
Habari (Maelezo),jijini Dar es Salaam leo, mama wa mtoto huyo, Veronika Laurent
ambaye ni Mkazi wa Bunju, alisema mtoto huyo alizaliwa huku akiwa na sehemu ya
kutolea haja kubwa lakini cha kushangaza, haja kubwa ilikuwa ikitokea mdomoni.
Alisema msaada wa fedha hizo utasaidia katika kumfanyia
operesheni mtoto huyo ambaye kwa sasa anaishi akiwa katika mateso makubwa.
Veronika alisema hivi sasa yeye pamoja na mwanaye huyo
wanaishi maisha ya kubahatisha baada ya baba wa mtotohuyo kuitelekeza familia
hiyo kutokana na hali ya ugonjwa wa mtoto huyo.
“Mimi ni nachoomba ni msaada wa fedha ili niweze kumpeleka
kwenye matibabu kwani sina msaada wowote,ukichukulia wazazi wangu kufariki na
hivi sasa naishi kwenye nyumba ya
mwenyekiti wa Mtaa wa Bunju wilayani Kinondoni jijini baada ya kushindwa
kupangisha chumba kwani sina kazi yeyote”alisema.
Aidha, alisema hadi utumbo wa mtoto huyo kutoka nje, ni
baada ya kufanyiwa operesheni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo
hata alipompeleka tena kwa ajili ya matibabu alikosa ushirikiano kutoka kwa
madaktari na wahudumu wengine.
Alisema kwa yeyote ambaye yuko tayari kumsaidia anaweza
wasiliana naye kwa kupiga simu namba 0715 83 77 00, na namba ya mwenyekiti huyo
wa mtaa 0656780236.
Veronika ni mzaliwa wa Mkoa wa Kilimanjaro eneo la Kijiji
cha Uru,Moshi ambye alimzaa mtoto huyo na mwanamme aliyemtaja kwa jina la
Abdalah Said, kabilake makonde mfanyabiashara wa viatu Ubungo.
EmoticonEmoticon