IKO HIVI...
KIZITO Mahamba (50) (pichani), mkazi wa Mwananyamala Mtaa wa
Msili B jijini Dar es Salaam, amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala wodi
namba 5A baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha na mkewe ambaye amemmwagia maji
ya moto mwilini.
YEYE ANASEMAJE........
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii huku akiwa katika
hali mbaya wodini alikolazwa, Mahamba alidai kuwa mkewe, Rabina Mkakamba (38)
kabla ya kufanya tukio hilo alianza kuonyesha dalili za kumdharau kila
alipojerea nyumbani.
“Siku ya tukio ambayo ilikuwa Oktoba 20, mwaka huu, mke
wangu hakuwa katika hali ya kawaida maana kila nilichomwagiza kufanya alikataa,
nikajiuliza kulikuwa na nini?
“Hayo yote yalipokuwa yakiendelea, jikoni alikuwa anachemsha maji, nikiwa
nimelala nilishitukia mke wangu akiingia
chumbani na chupa ya chai ambayo alinitupia na maji kuniunguza sehemu kubwa ya
mwili wangu, nadhani alitaka kuniunguza usoni.
AISEE....POLE SANA...IKAWAJE TENA?
Baada ya kufanya kitendo hicho alichukua sanduku la nguo
zake na fedha zangu na kutoweka huku akiniacha nikigaagaa .
“Nililetwa hapa hospitali na mtoto wa ndugu yangu na ndiye
anayenisaidia,” alisema Mahamba.
SOURCE : MPEKUZI
EmoticonEmoticon