Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy
Mwalimu, akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya pinga unyanyasaji na
matusi sokoni iliyofanyika Soko la Kivukoni, Ferri Jijini Dar es Salaam ikiwa
ni muendelezo wa siku 16 za kupinga unyanyasaji kijinsia.
Naibu Waziri Ummy Mwalimu na Balozi wa Uingereza nchini
Diana Croner, wakikata utepe kuzindua mabango yatakayobandikwa katika masoko
mbalimbali yakihamashisha kupinga vita dhidi ya unyanyasaji kijinsia na matusi
sokoni
Naibu Waziri Ummy akiwa na wanawake wafanyabiashara kutoka
masoko ya Ilala wakionyesha mabango ya kupinga matusi katika masoko.
************************************************************
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy
Mwalimu, ameahidi kuwa atahakikisha vinapatikana vituo maalum vya kuripoti
taarifa za unyanyasaji na matusi katika masoko na magulio wilaya ya Ilala ili
kurahisisha mapambano dhidi ya unyanyasaji.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za siku 16
kupinga unyanyasaji kijinsia katika soko la Kivukoni Feri leo iliyobebwa na
kauli mbiu ya “pinga unyanyasaji na matusi sokoni” “nipe riziki na si matusi”
iliyozinduliwa katika masoko matano ya Ilala, Kigogo Saambusa, Kibasila,
Mchikichini na Feri.Amesema kuwa, kutokana na hali halisi, wanawake wanapaswa kutoa taarifa katika madawati maalum katika vituo vya polisi, lakini kutokana na umbali wa vituo hivyo anaangalia uwezekano wa kusogeza huduma hizo kwenye masoko hayo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, ameeleza kuwa, katika tafiti zilizofanywa zinaonyesha kuwa asilimia 43 ya wanawake wamejikita katika ujasiriamali katika sekta isiyo rasmi ambapo wanakabiliwa na changamoto kadha wa kadha ikiwemo mitaji midogo, maeneo madogo ya kufanyia biashara wakijihusisha na biashara kama za mama ntilie, ushonaji, kutengeneza batiki na nyinginezo.
Ameongeza kuwa, utafiti uliofanywa katika masoko 10 ya jijini Dar es Salaam unaonyesha kuwa wanawake wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya unyanyasaji ukatili wa kingono, matusi na kiuchumi.
EmoticonEmoticon