IKO HIVI...
MAISHA ya msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack
Chuz’ yako hatarini kufuatia ujumbe wa kumuua unaosambazwa na muongoza filamu,
Mandela Nicholas ‘Jacob’ anayedai kudhulumiwa na msanii huyo kiasi cha shilingi
325,000.
Kwa mujibu wa ujumbe huo, jamaa huyo amedhamiria kumfanyizia
Jack kwa kumcharanga mapanga kisa eti kadhulumiwa kiasi hicho cha fedha ambazo
ni malipo ya kumuongozea filamu yake.
Jacob anadai kuwa, awali alimuandikia ‘script’ na
kumuongozea filamu msanii huyo lakini kabla kazi haijaisha, wakazinguana hadi
kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo Ilala jijini Dar.
Hata hivyo, mahakama alimuamuru Jack alipe fedha hizo lakini
kinyume chake msanii huyo akawa mgumu kutekeleza, hivyo kwa hasira Jacob
akamuandikia Jack sms hiyo ya vitisho.
Sehemu ya ujumbe huo inasomeka hivi;
“Labda kifo kiniite leo
Jack nitamuua, kama laki 325,000 hajanipa mtasikia. Kama rafiki au ndugu
jiandae na mazishi ya marehemu Jk Pentzel full panga tu.”
Sehemu nyingine ya ujumbe huyo ilisomeka hivi;
“Wapendwa Jack anachohitaji sasa ni kifo na nitamuua kweli,
mimi simsukumi…ila mapanga tu ndiyo dawa yake.
“Utapeli utamuua Jaki, leo kesho, keshokutwa mkisikia msiba
ulizia kapigwa panga au? Kama siyo panga siyo Jacob, kama panga na vipande 150
ewaa. Yeye kaburini mimi Segerea. Jasho la mtu haliliwi.”
EmoticonEmoticon