Na Frank M. Joachim & DW.
Upinzani Misri umesema leo kwamba utawasilisha rufaa ya
kupinga kura ya maoni ambayo imeidhinisha katiba mpya inayoungwa mkono na
viongozi wenye itikadi kali za Kiislamu, na kuapa kuendelea na mapambano ambayo
yamesababisha wiki kadhaa za ghasia na kuvuruga utuluvi nchini humo.
Chama cha
National Salvation Front kimesema matokeo ya awamu ya pili na ya mwisho ya kura
ya maoni iliyopigwa jana yamevurugwa na visa vya wizi na udanganyifu.
Mwanachama mmoja ameitaka tume ya uchaguzi kuchunguza visa hivyo kabla ya
kuyatangaza matokeo ya mwisho, yanayotarajiwa Jumatatu. Ujerumani imeunga mkono
miito ya kufanywa uchunguzi huru kuhusu matokeo hayo.
Waziri wa Mambo ya Kigeni
Guido Westerwelle amesema katiba mpya inaweza kuwa halali tu, kama itatimiza
masharti ya mchakato mzima wa kuidhinishwa bila kuwepo dosari zozote.
Lakini
Westerwelle amesema kwamba siyo kupitia nguvu za maandamano ya barabarani, bali
moyo wa mapatano na kuvumiliana ambao utaamua mustakbali wa Misri. Televisheni
ya taifa na chama cha Udugu wa Kiislamu cha Rais Mohamed Mursi kimesema katiba
hiyo imepitishwa kwa zaidi ya theluthi mbili ya kura za wananchi.
EmoticonEmoticon