UHUSIANO wa kimapenzi baina ya msanii wa filamu nchini
Elizabeth Michael maarufu kama (Lulu) ambaye anadaiwa kumuua bila kukusudia
msanii mwenzake Steven Kanumba yamewekwa wazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu baada ya msanii huyo kukiri kuwa alikuwa na uhusiano na Kanumba.
Mahakama Ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam
Upande wa serikali
ulisoma maelezo ya mashahidi tisa wanaotarajia kutoa ushahidi kwenye
kesi hiyo pamoja na maelezo ya onyo ya Lulu aliyoyatoa kituo cha
polisi Oysterbay ambayo ni moja ya vielelezo
vitakavyowasilishwa mahakamani wakati kesi itakapoanza kusikilizwa rasmi katika
Mahakama Kuu
EmoticonEmoticon