REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

Recent Posts

2 CHAINZ: MIE NI MTU MZIMA/ MSINIKAGUE KIJINGA.

7:17:00 AM Add Comment

  Na Hezron Munis  
RAPPER 2 CHAINS hakufurahishwa na Ukaguzi aliofanyiwa alipokuwa Airport Nchini Dubai huku akidai nkuwa umepitiliza na kumkwa yeye kama mtu mzima ambaye anastahili kuheshimiwa

Tukio limetokea Hivi karibuni ambapo 2 Chainz anadai kuwa, hakukataa kukaguliwa, lakini ule Ukaguzi ulizidi kiwango kiasi kwamba akahisi kusumbuliwa na hata kuingiliwa katika uhuru wake hasa mahali ambapo watu wengine wa kawaida hawakustahili kufika

  PICHA LIKO HIVI     
Kwa Mujibu wa Malalamiko ya 2 Chainz kupitia Instagram account yake, anadai kuwa Wahusika wa ukaguzi katika Airport hiyo, walimkagua mpaka mifukoni mwake na hata katika Begi lake Binafsi wakidhani kuwa huenda amebeba "Bangi" kitu ambacho yeye asingeweza kufanya kwa sababu anajua sheria nzi Nchi hiyo haziruhusu kabisa utaratibu huo wa Bangi.

Tofauti na hilo, 2 Chainz anadai kuwa, Wakaguzi walifikia mpaka hatua ya "Kumnusa" mikononi mwake ili kuthibitisha kuwa hajavuta kabisa hicho kitu kabla hajafika katika uwanja huo wa ndege.

Aidha Rapper Huyo ameongeza, yeye ni mtu mzima na wala hakuna kinachomzuia kuvuta "Bangi" , lakini isfikie hatua wakamkagua kupita kiasi ilihali yeye anafahamu sheria zote

VERA SIDIKA: HUWA SIPENDI NGUMZUNGUMZIA OTILE BROWN/ SIJUTII CHOCHOTE

6:59:00 AM Add Comment

VERA SIDIKA:Amesema kuwa Huwa hazungumzii Mahusiano yake yaliyopita


Na Baba Juti   

SOCIALITE kutokea Nchini Kenya ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, VERA SIDIKA maarufu kama "Queen Vee Bosset" ameweka wazi kuwa hajutii kamwe kuachana na aliyekuwa mpenzi Wake OTILE BROWN

Akifanya mahojiano na Kituo cha Redio cha Milele Kilichopo Nchini Kenya, Vera Sidika ambaye hivi sasa ana mahusiano mapya tayari, amesema kuwa mara nyingi hajutii kitu hata kidogo kwa Otile Brown ambaye hawakuachana vizuri, na ndio maana mara kwa mara huwezi kukuta anamzungumzia.

OTILE BROWN


Vera Sidika ambaye pia ni Mjasiriamali kutoka Nchini Kenya, amesema kuwa mara kadhaa amekuwa akisikia baadhi ya "Madongo" na habari nyingine tofauti kuhusu yeye ambazo Otile amrkuwa akizizungumza juu yake, lakini hawezi kujibu kwa sababu ni Takribani Miaka miwili na Ushee sasa imepita Tangu waachane

Pia ameongeza kuwa, huwa hana tabia ya kuzungumzia mambo ambayo yalishapita na hata kutoweka katika maisha yake, hivyo haoni haja ya kuendelea kumzungumzia mtu kama huyo

Kauli hiyo ya Vera Sidika ambaye hivi sasa ana mahusiano ya Kimapenzi na Msanii kutoka Nchini Tanzania JIMMY CHANSA, imetoka baada ya Otile Brown kutembelea Nchini Tanzania na kudai kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo Vera amewahi kumfanyia na hawezi kuyasahau.

Msikilize Hapa
CHANZO: Milele FM-KENYA

MWANDISHI WA HABARI ASIMAMISHWA KAZI KWA KUPOST TUHUMA ZA UBAKAJI ZILIZOKUWA ZIKIMUANDAMA KOBE BRYANT

6:34:00 AM Add Comment

  Na Hezron Munisi   
GAZETI la Washington Post linalochapisha Taarifa za kila Siku kupitia machapisho yake Nchini Marekani, limemsimamisha Kazi mwandishi wake wa Habari kwa kitendo cha "Kutweet" taarifa za Unyanyaaji wa kijinsia kupitia Ubakaji alizowahi kutuhumiwa Marehemu KOBE BRYANT mnamo mwaka 2016

FELICIA SONMEZ alipost "Link" a,bayo ilichapishwa mwaka 2016 kuhusu tuhuma hizo zilizokuwa zikielekezwa kwa Mkongwe huyo wa mpira wa kikapu katika Ligi ya NBA katika kipindi ambacho Mataifa mewngi na wadau wengi wa Marehemu Kobe Bryant wakiwa katika majonzi mazito.

FELICIA SONMEZ: Amesimamishwa Kazi Baada ya Kutweet Kuhus Tuhuma za Ubakaji zilizokuwa zikimuandama Marehemu Kobe Bryan



Uongozi wa Gazeti hilo la Washington Post, umedai kuwa, haikuwa sawa kabisa kwa mwandishi huyo wa Habari kupost kitu kama hicho katika kipindi hiki kigumu hasa kwa familia ambayo mpaka hivi sasa bado ipo katika majonzi makubwa ya Kumpoteza Kobe Bryan na Binti yake Gianna Bryant katika Ajali mbaya ya Helcopter

"Badala ya Kumlinda na kuendelea kumuunga Mkono mwanahabari katika Sura ya Udhalilishaji, Uongozi umemsimamisha kwa kumpa likizo ya Lazima" Barua kutoka katika Idara ya Uhalili ya Gazeti hilo ilinukuliwa hivyo

Tweet Aliyopost Mwandishi Huyo


Felicia Sonmez alitweet taarifa hiyo ambayo ilikuwa ikizungumzia tuhuma za Ubakaji zilizokuwa zikimuhusu Marehemu Kobe Bryant mnamo mwaka 2003, ambazo zilitia Doa kubwa katika Shughuli zake. Tuhuma hizo za ubakaji zilikuwa zikidai kuwa Marehemu Kobe alimbaka Mchezaji mwenzake wa kike aliyekuwa na Umri wa miaka 19 katika Kipindi hicho.

Hata hivyo mwandishi huyo aliondoa Tweet hiyo baada ya kuandamwa sana, huku akidai kuwa alianza kutishiwa kuuwa na baadhi ya watu


AMBER LULU : “MNATAKA NICHEKE CHEKE TU?”

6:14:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
#WatuWaMungu Malkia wa “Watakoma” Amber Lulu kuna namna ambavyo akiongea ama kuandika chochote katika Social Network accounts zake, lazima utajua tu kuwa kuna jambo “Limemvuruga”

Na hii inatokana na kile ambacho ameamua kukivunjia ukimya Baada ya waungwana wengi kuanza kumuandama kuwa ni kwanini amemficha “Chalii” ambaye inaaminika ndiye Mpenzi wake Mpya baada ya kutokuonekana akijihusisha na Mahusiano ypoyote ya kimapenzi kwa muda sasa

Sasa, Amber lulu ambaye hivi sasa anasukuma vizuri katika Game la muziki wa bongo Flava kupitia Track yake mpya ya “HATERS” , ameamua kuwafyatukia waungwana wanaopenda kutokumuona akipost mahusiano yake kuwa ni kwanini wanataka awe ni mtu wa kucheka cheka tu, na wala hawafurahii yeye kuwa katika mahusiano yake
 ' Ivi nyie mbona watu mnapenda kuwapangia watu maisha yao mnataka nianze kucheka cheka ovyo mana nyege zikizidi ndo nakoelekea nimekaa muda bila mahusiano so vyovyote ndo uyoo shemeji yenu mtake msitake imeishaa iyoooo ….size yangu '



TAARIFA: HUU NDIO UFAFANUZI WA RAPPER PREZZO KUHUSU KUBAKWA

5:53:00 AM Add Comment

 Na Hezron Munisi  

#WatuWaMungu kama utakuwa umetembea katika mitandao kadhaa ya Kijamii, utakuwa unafahamu vizuri kuhusu taarifa za Msanii kutoka Nchini Kenya, PREZZO kuwa amepelekwa Hospitali baada ya Kubakwa na Wanawake Watatu Nchini Humo

Taarifa hizo zimeibuka hivi karibuni kuwa Hitmaker huyo wa “PREZZO” kutoka katika Mitandao miwili kutoka Nchini UGANDA na Mwingine kutoka Nchini TANZANIA , kuwa Rapper huyo amefanyiwa tukio hilo baada ya kuwekewa madawa ya Kulevya aina ya COCAINE.

Tofauti na hilo, pia mitandao hiyo imefafanua kuwa, Prezzo hakuwekewa Dawa za Kulevya tu, bali hata zile za kuongeza nguvu za kiume aina ya VIAGRA, kitu ambacho yeye mwenyewe amekikanusha na kuongeza kuwa hakuna kitu kama hicho na wala hayuko hiospitali

Tunamnukuu
“ Niko salama kabisa, na wala sipo hospitali. Taarifa hiyo ni Uwongo Mtupu na imetengenezwa na watu ambao wana mpango wa kuharibu jina Langu”



Katika hatua Nyingine, Pia Prezzo amesema kuwa hiyo ni sehemu ya Njama za kutaka kumuondoa katika Malengo yake ya kugombea katika uchaguzi wa mwaka 2022

“ Ukikaa Mbali na watu, huwa wanatafuta aina ya taarifa za Uwongo kuzungumza kuhusu wewe. Nimejikita katika Mlengo wa Kisiasa hivi sasa. Nina uhakika wa Asilimia MIA MOJA NA KUMI kuwa nitawatumikia Wananchi wa Kenya 2022”

#BAABEKI !!: NELLY ANATAKA ALIYEMSINGIZIA KWA KESI YA UNYANYASAJI WA KINGONO AJITOKEZE HADHARANI !!!!!

12:33:00 AM Add Comment

Na Rich Sam 
#WatuWaMungu yule Hitmaker wa Mkwaju wa "Dilemma" , NELLY, bado hajaridhika kabisa na kitendo cha Bibie aliyemsingizia na kumfungulia kesi ya Unyanyasaji wa Kingono, aendelee kujificha, anatakiwa kujitokeza.

JANE DOE, ndiye mwanamke ambaye Mwezi November 2018 aliushangaza ulimwengu kwa kumfungulia Mashtaka Rapper Nelly, akidai kuwa msanii huyo alimdhalilisha kijinsia mnamo mwaka 2017 katika Tamasha ambalo lilifanyika Nchini Uingereza, na Nelly alikuwa ni msanii ambaye alikuwa akishusha show yake katika jukwaa hilo

Katika maelezo yake, Jane alidai kwamba alielekea upande wa "BACKSTAGE" kwa ajili ya kumuona Rapper huyo na kusalimiana nae, lakini alipofika pale, alishangaa kumuona Nelly akianza kumshawishi kingono, kisha akaanza kujichua uume wake, na kisha akamlazimisha JANE kufungua mdomo wake ili Nelly amalizie haja yake kwa  njia ya mdomo

Aidha, Mlalamikaji anadai kuwa, awali hakutoa taarifa kuhusu tukio hilo kutokana na kuwa na hofu kama Jeshi la Polisi lingemuamini.

Sasa Basi, January 24, Rapper Nelly ameiomba mahakama kufutilia mbali mashtaka na malalamiko ya mwanamke huyo, huku akisihi mahakama imuamuru mwanamke huyo kujitokeza mbele ya umma ili watu wamfahamu, pengine huenda ukapatikana ushahidi imara zaidi.


KUTANA NA KASHFA NYINGINE KUHUSU MTANDAO WA FACEBOOK..SAFARI HII NI "UBAGUZI"

1:20:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
MTANDAO wa Facebook umekutana na tuhuma nyingine za kutoa matangazo ya ajira ambayo kwa asilimia kubwa yamekuwa yakionekana kuwa na ubaguzi wa “kijinsia”

Kwa mujibu wa mashtaka hayo mapya yaliyofunguliwa na Taasisis mbili ambazo ni ACLU na  Equal Employment Opportunity Commission, inasemekana kuwa Matangazo mengi ya ajira ambayo huwa yanapostiwa Facebook, yamekuwa yakikiuka Haki za Ajira kwa sababu Waajiri wengi huonekana kupendekeza na kutangaza nafasi za kazi kwa jinsia ya kiume tu na sio ya kike kwa wingi

Aidha, Pia Taasisis hizo zimeweka wazi orodha ya Waajiri/Makampuni 10 ambayo yamekuwa yakitoa nafasi za kazi kibaguzi hasa wanawake wakiwa ndio waathirika wakubwa.

Makampuni ama waajiri 10 ambao wametajwa kutangaza nafasi za kazi zenye ubaguzi wa kijinsia katika Mtandao wa Facebook ni pamoja na Abas USA, Defenders, Nebraska Furniture Mart, City of Greensboro North Carolina, Need Work Today, Renewal by Andersen LLC, Rice Tire, JK Moving Services, Enhanced Roofing & Modeling and Xenith.

Uongozi wa Mtandao wa Facebook umeweka wazi kuwa, wao kama njia ya kuunganisha watu wote ulimwenguni katika suala la mawasiliano, hajaruhusu na wala hawakubaliani na “Ubaguzi” wa aina yoyote katika mtandao huo, na wako tayari kufuatilia kile kinachodaiwa  ili wachukue hatua haraka iwezekanavyo

REDSAN KAFANYA FUJO...TAARIFA HII HAPA

3:37:00 AM 1 Comment

Na Baba Juti
MAPEMA asubuhi ya leo, taarifa zimefikishwa katika dawati la "Hit Zone" kuhus kitendo cha Producer SAPPY kutoka jijini Mwanza ambaye muda mwingi hufanya kazi zake Nchini Kenya, kuvamiwa na kujeruhiwa akiwa studio kwake Nchini Humo

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa ERVIX ambaye pia ni Msanii kutoka nchini Tanzania anayefanya kazi Nchini humo chini ya SAPPY MUSIC LAB inayomilikiwa na Producer Sappy, tukio hilo limetokea Siku ya jana na Vurugu hizo ziliznzishwa na msanii nguli kutoka nchini Kenya, REDSAN.

Msanii huyo amezidi kueleza kuwa, chanzo cha ugomvi huo, ni kitendo cha wao (Ervix na Sappy) kutokuhudhuria katika Uzinduzi wa Album ya REDSAN ilihali Sappy ndiye aliyeproduce nyimbo nyingi zinzopatikana katika Album hiyo.

Sababu ambazo ziliwafanya wawili hao kutokuhudhuria katika Uzinduzi huo, ni pamoja na Sappy kupata safari ya kikazi Mombasa, kutokuelewa mustakabali wa faida ambayo ataiapata sababu ameproduce nyimbo kadhaa na hajui atanufaika vipi maana nyimbo iliyolipiwa ni moja, Ervix kutokuhudhuria katika Shughuli hiyo sababu ya mizunguko ya hapa na pale....

SIKILIZA sauti ya ERVIX

SUBIRI KWANZA !!!!! : JUSTIN BIEBER NA HAILEY BALDWIN WAMEFUNGA NDOA TAYARI?

2:57:00 AM Add Comment

Na Hezroni Munisi  
WATU WA MUNGU inawezekana kabisa kuwa Justin Bieber na Mchumba wake HAILEY BALDWIN wakawa wameshafunga ndoa "Kimya Kimya" ?

Kipindi cha nyuma kidogo, taarifa zilikuwa zimeshaenea kabisa kuwa Justin Bieber ambaye awali alikuwa katika mahusiano na Selena Gomez, amezama kwa bibie huyo ambaye anatokea katika familia ya watu maarufu hapa ulimwenguni.

Sasa baada ya kutokuambiwa Ndoa ya wawili hao ni lini, huku wao wakificha licha ya kwamba wameshavalishana pete ya Uchumba, hatimaye Mjomba wa Hailey Baldwin, muigizaji ALEC BALDWIN amejikuta akitoa taarifa ambayo inashabiliana kabisa na wawili hao kufunga Ndoa tayari na ilikuwa ni ya Siri haswa

Akiwa katika upande wa "Red Carpet" kunako Tuzo za EMMYS (Emmys Awards 2018), Alec ambaye ni Mjomba wa Hailey alisema kuwa wamefunga ndo ya Haraka na ya siri kwa asilimia kubwa kwa sababu kwao , suala zima la ndoa, ndicho kitu ambacho wamekuwa wakikitamani muda mrefu na kitawaunganisha na kuwapa Furaha

"Kilichotokea mahakamani, ni kitu cha mahakamani na ni suala la kisheria. Ila Ndoa, ni pale ambapo watu wawili wanaweka wakfu mbele ya mwenyezi mungu na watu wanaowapenda...."
alisema Mjomba mtu

RAPPER WALE AZUIWA KUKAA KATIKA DARAJA LA KWANZA KWENYE NDEGE YA AMERICAN AIRLINES

2:10:00 AM Add Comment




Na Rich Sam
WAKATI mataifa mengi na wananchi wengi ndani ya mataifa hayo yakiendelea kupinga kabisa kitu kinachoitwa "UBAGUZI WA RANGI" safari hii huenda mambo yakawa magumu haswa kwa shirika la ndege Nchini Marekani (American Airlines) baada ya kulalamikiwa kwa mara nyingine tena

RAPPER Kutoka Nchini humo ambaye asili yake ni Nigeria Barani Afrika, WALE, ametoa kilio chake kup[itia account yake ya Twitter kwa madai kuwa alifanyiwa ubaguzi wa Rangi baada ya baadhi ya Wahudumu kumwambia kuwa hakustahili na hana hadhi ya kukukaa katika daraja la kwanza ndani ya ndege hiyo

Tukio hilo limetokea hivi karibuni ikiwa ni baada ya Wale kulalamika kuwa alikuwa amekata Ticketi ambayo ni sahihi na alitakiwa kukaa katika Seat yake sahihi kabisa, lakini baadaye alizuiwa kuingia katika daraja hilo kwa Takriban dakika 30 mpaka 45, na kisha baadaye safari yake kuahirishwa


Wale ambaye ni "member" wa MMG, kundi ambalo liko chini ya Rapper Rick Ross, aliona hana budi kulalamika kupitia Twitter huku akiripoti kuwa ataenda kuwashtaki polisi kwa kitendo hicho

"Vipi kuhusu wafanyakazi wenu MEGUUMI na DON waliponiambia kuwa sitakiwi kuwa katika Daraja la Kwanza?... ninawapigia Polisi" alilalamika hivyo Wale

Ukiachilia mbali Twitter hiyo, Wale alidirikikuhoji ni hatua gani zitachukuliwa zidi ya wafanyakazi hao wawili

"Nyie nyote ni wabaguzi wa Rangi. Ninataka kujua ni hatua gani itachukuliwa. MEGUUN na DON ndio majina yao"



MNADA BANNER