Rais Wa Kenya , Mwai Kibaki. (Picha na Maktaba) |
Mswada huo ni miongoni mwa miswada 30 iliyotiwa sahini na kiongozi huyo wa taifa, kuwa sheria, saa chache baada ya kufanyika maandamano ya kumtaka kutotia saini mswada unaowapa wabunge mlipo ya kiinua mgongo cha mabilioni ya pesa.
Hata hivyo, rais Kibaki HAKUTIA saini miswaada inayowapa waziri mkuu, makamu wa rais, jaji mkuu na maafisa wengine wa serikali malipo ya pindi wanapostaafu.
Mapema jumatatu, mashirika ya kijamii yaliandaa maandamano katikati ya jiji la Nairobi wakimtaka rais kutotia saini mswaada ambao ungewapa wabunge kiinua mgongo cha shilingi milioni 9.3 kila mmoja pamoja na marupurupu mengine.
1 comments:
Write commentsMswada Huu ingekuwa Nchini Tanzania, nini Kingezuka?
ReplyEmoticonEmoticon