Sababu kuu
ya kukamatwa,ni kuhusishwa na tukio la kumwagiwa tindikali Bwana Musa Tesha 9
Sept,2011 huko Igunga kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Mbunge ambapo mgombea
wa CCM bwana Peter Kafumu alimshinda mgombea wa CHADEMA bwana Joseph Kashinde.
Bwana
Oscar alifuatwa dukani kwake stand ya mabasi ya 
Shinyanga mjini mnamo saa 9 mchana 
na askari nane ambao hawakuvaa sare.
Baada ya
mazungumzo ya muda mfupi askari hao waliwaomba majirani wa duka hilo
wasogee  ili wawe mashuhuda  wakati wanampekua.
Hata
hivyo,polisi  hao hawakukuta kitu
chochote walichokihitaji na kuamua kuondoka naye kwenda kumpekua nyumbani kwake
ambako nako pia hawakuambulia kitu.
Taarifa
iliyopatikana  jana  mchana 
kutoka ofisi ya RPC shinyanga ni kuwa Oscar amepelekwa Tabora kwenda
kufunguliwa mashitaka.

EmoticonEmoticon