Serikali ya Venezuela imetoa hadharini kwa mara ya kwanza
picha za rais Hugo Chaves ambae hajaonekana katika macho ya umma wa taifa hilo
tangu Desemba mwaka jana.
Katika picha hizo rais Chaves anaonekana amelala kitandani
huku Mabinti wake wawili wanaonekana
wakiwa wamesimama pembezoni mwake.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 58 anaendelea kurejea
katika afya yake baada ya kupata matatizo yanayohusishwa na upasuaji wa ugonjwa
wa saratani.
Mpaka sasa serikali ya Venezuela anaendelea kumsubiri Chaves
apate nafuu ili aweze kuapishwa ili kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine
wa miaka sita.
EmoticonEmoticon