Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt. Terezya Huviza leo ameendelea kufanya ziara za kushtukiza katika viwanda na mahoteli mbalimbali jijini Dar es salaam kuangalia hali ya usafi wa mazingira.
Katika ziara hiyo Mh waziri na ujumbe wake wametembelea
kiwanda cha Bia cha Serengeti, CI Group Marketing Solution, Coco Beach, hoteli
za Golden Tulip na Sea Cliff.
Akitoa maamuzi kuhusu mazingira aliyoyakuta katika kila
sehemu, Mh. Dkt. Huviza amesema Kiwanda cha Serengeti kina mfereji unaomwaga
maji machafu na bahati mbaya unatitirisha katika makazi ya watu kitu ambacho ni
hatari, hivyo atashauriana na NEMC na Mwanasheria waone jinsi ya kuwasaidia,
lakini kama itashindikana kwa kuwa maji wanayomwaga ni mengi sana itabidi
wafunge kwa muda.
Kuhusu maeneo mengine aliyoyatembelea Mh. Waziri amesema
hawezi kutoa maamuzi kwa sasa kwa sababu kila aliyekutwa na makosa amepewa muda
wa kuyarekebisha na ambaye atashindwa kufanya hivyo basi atafungiwa kwa mujibu
wa sheria.
EmoticonEmoticon