Serikali ya Ivory Coast imeingiwa na kiwewe juu ya
kutekeleza agizo la Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC la kumkabidhi mke wa
Laurent Gbagbo Rais wa zamani wa nchi hiyo, kwa kuhofia kuvurugika mapatano ya
umoja wa kitaifa nchini humo.
Taarifa zinasema kuwa, hatua ya kukabidhiwa
Simone Gbagbo kwa Mahakama ya ICC itaitumbukiza nchi hiyo kwenye hatari zaidi
serikali ya Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast.
Taarifa hizo zinasema kuwa,
Rais Ouattara yuko njia panda kati ya kutekeleza agizo hilo la kimataifa na
kuitumbukiza nchi yake kwenye mfyatuko na mpasuko.
Mahakama ya ICC imeeleza
kuwa, Simone Gbagbo ana kesi ya kujibu kwani anakabiliwa na tuhuma za kutenda
jinai dhidi ya binadamu kuanzia tarehe 16 Oktoba 2010 hadi Aprili 12, 2011
nchini humo. Waranti uliotolewa na ICC wa kutiwa mbaroni na kukabidhiwa mke wa
Rais wa zamani wa Ivory Coast umekabiliwa na upinzani mkali kutoka Ivorian
Popular Front FPI chama kikuu cha upinzani nchini humo.
EmoticonEmoticon