Mtu aliyekuwa na silaha nzito amefanya mashambulizi katika
shule ya awali iliyoko Newtown kwenye jimbo la Connecticut, nchini Marekani na
kuwaua watu 26 wakiwemo watoto wadogo 20 wenye umri kati ya miaka 5 hadi 10.
Mtu huyo anayekadiriwa kuwa katika umri wa miaka 20,
alivamia darasa kwenye shule hiyo ambayo mama yake alikuwa mwalimu na
kumfyatulia risasi mama yake pamoja na wanafunzi 18 darasani humo kabla ya
kuwauwa watu wazima watano na kisha kujiua mwenyewe.
Wanafunzi wengine wawili walifariki wakiwa hospitalini
kutokana na majeraha waliyopata. Polisi wamesema kuwa hilo ni moja kati ya
matukio mabaya ya mauwaji ya raia katika historia ya Marekani. Polisi imesema
kuwa mtu huyo alikutwa amekufa ndani ya shule hiyo.
Muuwaji anaripotiwa alikuwa na silaha nne za mkononi na
alivalia mavazi ya kujikinga na risasi. Mtu mwingine alikutwa amekufa kwenye
mji huo wa Newtown na kufikisha idadi kuwa 28.
Obama awalilia watoto waliouawa
Rais Barack Obama akizungumzia mauwaji ya Newtown Rais
Barack Obama akizungumzia mauwaji ya Newtown
Rais Barack Obama ametoa tamko akiwa katika hali ya majonzi
makubwa kwenye Ikulu ya nchi hiyo White House na kuapa kupigania udhibiti wa
silaha kwa kiwango kikubwa.
Obama alionekana akijifuta machozi mara kwa mara wakati
anazungumza na waandishi wa habari kuhusu vifo vya watoto wadogo ambao aliwaita
"watoto wazuri wenye umri wa miaka kati ya 5-10".
Alisema "leo mioyo yetu sote imevunjika. Wazazi, bibi
na babu, dada na kaka wa watoto hawa wadogo na pia familia familia za watu
wazima waliouawa kwenye kisa hiki" alisikika Obama katika sauti ya mtu
anayelia.
Mara baada ya kuenea kwa tarifa hizo za mauwaji, wazazi
waliokuwa na wasiwasi walikimblia shuleni hapo kuwatafuta watoto wao wakati
wanafunzi waliokuwa wamelwa damu walipokuwa wanatolewa nje ya jengo. Mamia ya
wakaazi wa Newtown wamekusanyika katika kanisa laKatoliki la Mtakatifu Rose wa
Lima lililopo umbali mdogo kutoka eneo la tukio kuwaombea waathirika.
Taarifa kuhusu mshukiwa
Taarifa kuhusu mshukiwa wa mauwaji hayo zinasema kuwa kijana
huyo anatambulika kwa jina la Adam Lanza na mama yake aliitwa Nancy Lanza.
Silaha zilizotumiwa na kijana huyo zilinunuliwa kisheria na mama yake mzazi.
Jirani wa mama huyo amesema kuwa aliwahi kumweleza kwamba anapendela kwenye
kwenye mafunzo ya kufyatua risasi na wanawe
Kikosi cha usalama kwenye eneo la tukio Kikosi cha usalama
kwenye eneo la tukio
Hapo awali vyombo vya habari viliripoti kuwa kijana
ajulikanae kwa jina la Ryan Lanza mwenye umri wa miaka 24 ndiye mshukiwa wa
mauwaji hayo. Baadae ikafahamika kuwa Ryan ni kaka mkubwa wa Adam.
Ryan alikuwa kazini New York City wakati muuwaji alipofyatua
risasi katika shule ya awali ya Sunday Hook. Miongoni mwa watu wazima waliouawa
ni pamoja na Mkuu shule hiyo ambaye ni mwanamke aliyefahamika kwa jina la Dawn
Hochsprung.
Hochsprung alikuwa miongoni mwa watu watatu waliokimbilia
kwenye madarasa ilikosikika milio ya risasi pamoja na msaidizi wake na mwalimu
wa saikolojia shuleni hapo. Baada ya muda mkuu msaidizi alitoka nje ya eneo
akiwa amejeruhiwa mguu na wawili hao hawakurejea na baadae kufahamika kuwa
wameuawa.
EmoticonEmoticon