Akina mama waombolezaji wakisawazisha kaburi la marehemu
Sinjembele Julius(62) aliyeuawa kwa kupigwa na mwanae Ndele Julius(25)
Baadhi ya
waombolezaji wakishuhudia mazishi ya Sinjembele yaliyofanyika Nyumbani kwake
katika kitongoji cha Igawilo kata ya Swaya Mbeya
Kaburi baada ya
kuzikwa marehemu
************************************
Mkazi wa Swaya jijini
Mbeya Ndugu Ndele Julius amemuua mama
yake mzazi kwa kumpiga mateke na ngumi kisha kutoroka pasipo julikana Novemba
25 mwaka huu.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10 jioni nyumbani kwa
mama huyo mara baada ya kutokea kwa ugomvi kati ya mtoto wake na kijana mwingine hali iliyopelekea mama huyo
kuingilia ndipo alipo kutwa na mauti huo.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani amesema
kuwa Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliokuwepo kati ya mtoto wake na
kijana mwenzake kitendo ambacho
kilipelekea mama huyo kuingilia ugomvi huo .
Amesema wakati mama
huyo akijaribu kuamulia ugomvu huo mtoto wake alicha kupigana na mwenzake na
kuanza kumshambulia mama yake kwa kumpiga ngumi na mateke mwilini.
Amesema mama huyo alifariki muda mchache kutokana na kupigwa
sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababishiwa majeraha makuibwa yaliyopeleka
kupoteza uhai wake.
Awali akizungumzia tukio hilo Mtoto wa Kwanza wa mama huyo
Ndugu Razaro Mbwiga amesema kuwa mdogo wake alikuwa na tabia ya kugombana na
mama yake marakwamara .
Hata hivyo teyari mwili huo umekwisha chukuliwa hospitali na
kuzikwa ambapo katika maziko hayo Chama cha Muungano wa kijamii (Mujata)
umewataka vijana kujiepusha na vitendo viovu kama uvutaji bangi na pombe za
kienyeji kwani ndio chanzo cha kutokea kwa vurugu nyingi.
EmoticonEmoticon