REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MAJANGA: MWANAFUNZI ALIYEHITIMU KIDATO CHA NNE AKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA NJIA YA ATM

2:13:00 AM Add Comment


POLISI wilayani Rungwe, mkoani Mbeya, limewanasa watu wanne akiwamo mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana, wilayani Bunda, mkoani Mara, baada ya kukutwa wakiiba fedha Benki ya NMB tawi la Tukuyu kupitia mashine za kutolea fedha (ATM).

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chrispin Meela alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2:30 usiku.
Meela aliwataja watuhumiwa  hao kuwa ni mkazi wa mjini Tukuyu,  Mfanyabishara wa Mbozi, mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana wilayani Bunda na mkazi wa Msasani Tukuyu.

Alisema akiwa nyumbani kwake usiku, alipigiwa simu na msamaria mwema na kuambiwa taarifa za kuwapo watu  wakiwa kwenye mashine hizo za kutolea fedha, huku wakiwa wanatoa fedha mfululizo na aliwatilia shaka.

“Jana  usiku saa 2:30 nilipigiwa simu na msamaria mwema na kuniambia kuwa,  kuna watu wapo Benki ya NMB wanatoa fedha ATM tena mfululilo huko wakiwa na kadi nyingi za ATM,” alisema Meela na kuongeza:“Baada ya kuambiwa hivyo nilimpigia simu OCD (Mkuu wa polisi wilaya), akatuma timu ya makachero eneo ta tukio na wakabahatika kuwakuta na kuwatia nguvuni.”

Meela alisema watuhumiwa  walikutwa wakiwa na kadi bandia za ATM 150 za watu tofautitofauti  na kwamba, hadi wanatiwa mbaroni tayari walikuwa na Sh20.5 milioni mkononi. Alisema kadi zote ni za NMB na kwamba, zilikuwa zinaonyesha  wateja wote ni walimu kutoka wilayani Mbozi.

Alisema baada ya watuhumiwa kuhojiwa  walidai ni wafanyabiashara wanajihusisha na kukopesha fedha walimu, hivyo  katika kuzirejea fedha hizo walimu waliwapatia kadi zao ili waende kutoa  benki.

“Kinachotupa hofu  hapa ni kwamba, kadi zote hizi zinaonyesha wateja kutoka wilayani Mbozi, sasa swali kwa nini waje kutolea fedha hizo wilayani kwetu?” alihoji Meela.

Alisema watuhumiwa wote wapo Kituo cha Polisi Tukuyu kwa mahojiano zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alikiri kupata taarifa hizo, lakini alikataa  kulitolea ufafanuzi kwa sababu  wanaendelea na uchunguzi.

KASHFA: MSANII BONGO, ATELEKEZA MTOTO WAKE UBUNGO

1:59:00 AM Add Comment


MPEKUZI

MREMBO aliyewahi kupamba video kadhaa za wasanii wa Bongo Fleva ukiwemo wimbo wa Kidato Kimoja ulioimbwa na J.I, anayekwenda kwa jina la Maya Silemwe, amedaiwa kumtelekeza mwanaye wa kumzaa aitwaye Junior Justine (3).

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo mtoto huyo aliokolewa na msamaria mwema.


Akisimulia mkasa mzima ulivyokuwa, shangazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Monalisa, alisema wao kama familia wameumizwa sana na kitendo kilichofanywa na Maya.

“Maya amezaa na kaka yangu Justine anayeishi Marekani na amekuwa akimjali sana kwa kumtumia fedha za matumizi mara kwa mara. Kisa ni kwamba kaka alimwambia Maya ampeleke mtoto Bukoba (nyumbani kwa baba wa mtoto) akasalimie, Maya akakubali lakini akamwambia atapitia kwanza Arusha (nyumbani kwao) ndipo waende Bukoba.

“Justine akamuelewa lakini kumbe alidanganya, hakwenda Arusha na kuna watu walimuona akiingia kwenye klabu moja hapahapa Dar es Salaam, wakamjulisha kaka. Sasa alipompigia kumuuliza, akawa anajing’atang’ata, siku iliyofuata akadamkia Ubungo ili kumsafirisha mtoto kwenda Bukoba kwa mama yetu (bibi wa mtoto) lakini alitaka kumsafirisha kwa kumtumia kondakta,” alisema Monalisa na kuongeza:

“Alikubaliana na kondakta huyo kisha akamwachia namba ya simu ya mama na yake ili waweze kuwasiliana na kumpokea mtoto huko Bukoba.

Kwa bahati mbaya siku ile yule konda alikuwa hasafiri mpaka siku inayofuatia. Mtoto akaanza kuhangaika stendi siku nzima bila uangalizi mzuri.

“Bahati nzuri mama mmoja msamaria mwema akafuatilia na kuonana na huyo konda, akamuomba namba za mama wa Bukoba kisha akawasiliana naye, kwa kuwa alikuwa na safari ya kwenda huko siku iliyofuata, akaamua kuchukua jukumu la kusafiri naye.”

Monalisa alikubali kutoa namba za simu za msamaria aliyejitolea kusafiri na mtoto huyo, alipopigiwa alikiri lakini aliomba sana asitajwe .

“Mimi kama mzazi iliniuma sana kumuona mtoto mdogo anahangaika stendi bila uangalizi. Nilishangaa sana kuona mzazi aliyeingia ‘leba’ anawezaje kumwacha mwanaye mdogo namna ile asafiri mwenyewe?” alisema.


Naye baba mzazi wa mtoto huyo, Justine aishiye Marekani ambapo alisema kuwa: 
“Jambo hilo limeniumiza sana. Kwa kweli kama ningekuwa huko nyumbani (Bongo) ningehakikisha namfundisha adabu huyo mwanamke kupitia sheria.

“Nashukuru kusikia kwamba mwanangu alifikishwa salama Bukoba.”

Mama wa mtoto huyo alipopigiwa simu alizua kioja baada ya kukataa kwamba hajawahi kumuacha mtoto kwa konda Ubungo na pia akadai eti hana mtoto na wala hajawahi kuzaa katika maisha yake yote.

Wakati tukijiandaa kwenda mitamboni juzi Jumatatu, habari zilizopenyeza katika chumba chetu cha habari zilisema kwamba mrembo huyo alimpigia simu mama mkwe wake na kumchimba mkwara mzito.

FULL SECURITY: JACKLINE PATRICK AONESHA BASTOLA YAKE INSTAGRAM

1:49:00 AM Add Comment

OH MY GOOOOOOOOD...akiwa bado katika Msala wa Kumchapa na Chupa Mrembo mwenzake, Kama hakijatokea kitu vile, Jackline wa Patrick amesanua Mguu wake wa Kuku...namaanisha Bastola kupitia Mtandao wa INSTAGRAM, kama uonavyo hapo, Huku akipost Kauli hii

"This is For Security Purpose, nat harmful to anyone. Loool"

SWALI:, Kama umemtandika yule dada na BOTTLE, je hii ukiwa nayo karibu si utamfyatulia Mtu akikuudhi?

ONYO: WALIMU WAPEWA KALI

1:26:00 AM Add Comment


MKUU wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele, ametoa onyo kwa baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari wanaotumia vibaya madaraka na kuwachangisha michango mipya wananchi bila maelezo ya msingi.

Henjewele ametoa kauli hiyo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilayani hapa juzi.

Alisema kuanzia sasa atawaagiza wakaguzi wa ndani kukagua hesabu zote katika shule za sekondari wilayani hapa.

Alisema katika siku za hivi karibuni wazazi wamekuwa wakielezwa kuchangia fedha nyingi kila mwanzo wa muhula wa kwanza wakati hakuna hesabu maalumu katika shule hizo zinazoonyesha matumizi ya michango ya mwisho wa kila mwaka.

“Baadhi ya wazazi wamelalamika juu ya utitiri wa michango hususan katika shule za serikali za kata kila wanapoanza muhula wa kwanza kila mwaka kiasi cha baadhi yao kushindwa kuwapeleka watoto wao kuanza kidato cha kwanza kwa wakati.

“Kuanzia sasa nimewaagiza wakaguzi wa hesabu wa ndani wa halmashauri kufanya ukaguzi katika shule zote za sekondari…na iwapo itathibitika kuwa ubadhirifu umetokea na kusababisha upotevu wa fedha hatua stahiki zitachukuliwa,” alisema Henjewele.

Alisema michango hiyo imegeuka neema kwa baadhi ya wakuu wa shule hizo ambapo sasa baadhi wamekuwa wafanyabiashara huku wakiacha watoto bila kufundishwa sawasawa na kusababisha kupatikana matokeo yasiyoridhisha wakati wa mtihani wa kidato cha nne.

FEDHEHA : MOSHI WAMKERA MHE. CHARLES TIZEBA

1:15:00 AM Add Comment

Na Rodrick Mushi, Moshi


NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba, amesema amefedheheshwa na kitendo cha uongozi wa manispaa ya Moshi kutaka kuua uwanja wa ndege wa Moshi kwa kugawa ardhi ya uwanja kwa baadhi ya watu.

Mbali na hilo alisema pia kuna mkanganyiko wa mchoro wa uwanja huo wa awali baada ya kubadilishwa.

Tizeba alisema hayo mjini hapa jana baada ya kufanya ziara yake kwenye uwanja huo akiwa ameambatana na Mbunge wa Jimbo la Moshi, Philemon Ndesamburo.

Katika ziara hiyo walizunguka maeneo mbalimbali ya uwanja huo na kujionea ujenzi uliofanyika ndani ya uwanja huo.

Akizungumza kwenye kikao kilichofanyika ndani ya uwanja huo, Tizeba alisema kufa kwa uwanja huo kunachangiwa na watu wa Moshi wakiwemo baadhi ya viongozi wa manispaa.

Kutokana na hali hiyo alimtaka kufika Ofisa Mipango Miji, Alex Poteka, ambaye alifika muda mfupi huku majibu yake yakionyesha kutomridhisha naibu waziri huyo.

Awali akitoa malalamiko kwa Waziri Tizeba, meneja wa uwanja huo wa ndege, Francis Massao, alilalamika kuomba michoro ya awali ya uwanja huo toka kwa uongozi wa manispaa akiwamo ofisa mipango miji, Poteka, kwa kuandika barua bila mafanikio.

“Hivi ni wapi au ni uwanja gani wa ndege unaoweza kuongoza ndege huku kukiwa kuna nyumba imejengwa katikati ya uwanja!?” alisema Massao.

Tizeba alisema kuwa uwanja wa Moshi ni uwanja mkongwe kuliko yote ila umechoka kutokana na kutofanyiwa ukarabati muda mrefu.

Kwa upande wake, Poteka alijitetea kuwa hana taarifa kamili juu ya watu waliojenga kwenye eneo hilo la uwanja.

WIZI KWA NJIA YA ATM WAZIDI KURINDIMA

1:02:00 AM Add Comment


NA Christopher Nyenyembe

WIMBI la wizi wa fedha kwenye mitandao ya benki kupitia njia ya mashine za kuchukulia fedha (ATM), umewatia hasara wateja wengi wa benki ambao zaidi ya sh milioni 20 zinadaiwa kuchotwa kwa nyakati tofauti na watu wanne wanaomiliki kadi zipatazo 150.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano umegundua kuwepo kwa mtandao wa wizi kwa njia ya ATM unaotumiwa na watu wanaojifanya kuwa ni madalali wa fedha wanaowalaghai watumishi wa serikali.

Madalali hao wanadaiwa kuwakopesha watumishi hao wa serikali kwa sharti kwamba wawapatie kadi zao za kuchukulia fedha benki kama dhamana.

Uchunguzi umebaini kuwa, mtindo huo umeenea katika maeneo kadhaa mkoani Mbeya na hasa ukiwalenga watumishi wa serikali ambao kutokana na hali ngumu ya kifedha, wamejikuta wakiingia kwenye mtego huo na kuamua kutoa kadi zao za ATM ili waweze kupata mikopo.

Habari ambazo gazeti hili imezipata kutoka kwa waathiriwa wa wizi huo wa mtandao, unasema kuwa wapo madalali ambao wanawafuata watumishi wa serikali kwa lengo la kuwakopesha fedha kwa masharti kwamba watoe kadi zao za ATM na namba za siri kama dhamana.

“Mtandao wa kuchukua fedha kutoka kwa watumishi wa umma umeenea sana, haukuanza leo, wapo watu wanakopesha fedha kwa sharti la kutoa kadi ya ATM na namba yako ya siri ili mshahara wako unapoingia, wao wanakwenda kuchukua fedha zao walizokopesha na riba,” alisema mtumishi mmoja wa serikali jijini Mbeya.

Wakati hali ikiwa hivyo, habari kutoka Wilaya ya Rungwe zinadai kuwa kiasi kikubwa cha fedha kimechukuliwa benki na watu wanaomiliki kadi za ATM zaidi ya 120, na kwamba tayari Jeshi la Polisi linawashikilia watu hao ambao wamekutwa na idadi hiyo ya kadi zisizokuwa zao.

Habari zaidi zinasema kuwa, mtandao wa madalali hao wa fedha umekuwa mkubwa, na kwamba watu hawaibiwi kwani wametoa kadi zao wenyewe baada ya kukubali kukopeshwa.

“Ndugu mwandishi tumefikia uamuzi huu kutokana na hali ngumu ya maisha, watoto wanatakiwa walipiwe ada, tunahitaji mbolea kwa ajili ya kilimo na gharama za maisha zipo juu, tutafanyaje? Ndiyo maana tumejikuta tukitoa kadi zetu za ATM ili tutatue matatizo yetu, kama wapo matapeli hilo sijui, ila wengi tumeingia kwenye mtego huo,” alisema mama mmoja aliyejitaja kuwa ni muuguzi.

Meneja mmoja wa benki ambaye hakutaka jina lake liandikwe wala benki anayofanyia kazi, alisema wizi kwa njia ya ATM ni tatizo sugu kwa wateja wao, kwani wamekuwa wakipokea malalamiko kila siku kuwa fedha zao zinaibwa bila wao kujua.

Alisema hana taarifa kama kuna wateja wanaotoa namba zao za siri na kadi zao kwa madalali wa fedha.

“Kinachonishangaza benki yetu inakopesha, sasa huu mtindo uliozuka kati ya wateja na madalali wa nje unatia shaka usalama wa fedha kwenye benki zetu, inabidi hatua kali zichukuliwe kwa wateja wanaoruhusu watu wengine wawachukulie fedha, hilo ni kosa la jinai kufanywa na wateja wasiokuwa waaminifu,” alisema meneja huyo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman alipohojiwa alisema kuwa amepokea taarifa za kuwepo kwa tukio hilo, hasa Wilaya ya Rungwe na kwamba tayari anasubiri taarifa kamili kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Mbeya (RCO) ili atoe taarifa kamili leo.

NANI KAMA MAMA?.. YOUNG AND BEAUTIFUL

12:40:00 AM Add Comment
KAMA huna kawaida ya kumpenda Mama Yako Mzazi, basi hakika una baraka Chache sana Maishani mwako. 

Binafsi Tunampenda sana Mama Yetu Mzazi, MAGRETH KAGARUKI (Kushoto) ambaye amekuwa chachu kubwa sana ya Maendeleo katika Familia Yetu. Upendo wake wa Dhati kwa Baba Yetu Mzazi MAGNUS JOACHIM na Sisi watoto wao, umekuwa ni Sukari ya Furaha, Mapendo na hata Amani ndani ya Familia Yetu.

Tunakupenda sana Mama Yetu, na Hata Baba Pia. Ila amini usiamini, nimekumiss sana, maana ni Miaka Mitatu sasa Sijaonana na Wewe, ila nakuahidi Mwezi March mwaka huu, lazima nije kuitembelea Familia Yangu.

WE LOVE YOU ALOT, AND WE ARE VERY PROUD OF YOU MAMA and DADY TOO

HANKER CHIEF YANGU: BINAFSI NIMEMUELEWA TIMBULO

12:30:00 AM Add Comment

HANKER CHIEF YANGU LEO inamfguta Jasho Timbulo kutokana na Msala ambao ulikuwa unamkabili, kuhusu MADAWA YA KULEVYA;

Timbulo amesema ni kweli alihisiwa kuwa amebeba madawa ya kulevya kitu kilichowafanya wanausalama kuomba kumkagua na kweli kumkuta na Pipi ambazo mara nyingi zimekua ni mfumo wa kubebea madawa ya kulevya katika begi lake, lakini katika maelezo ya timbulo anasema hazikuwa dawa za kulevya kweli bali ni mfano wa dawa ambazo alifanyia shooting katika movie yake ya hivi karibuni na kusahau kuzitoa.

BALAA: BOBBY BROWN ATUPWA JELA

12:14:00 AM Add Comment


WAKATI Binti ake akiwa katika Skendo la Kufuata Tabia za Mama Yake Marehemu Whitney Huston kwa kuchoma Shisha, Boby Brown ambaye ni Mume wa Marehemu Whitey ametupwa Jela kwa Siku 55.

Kwa Mujibu wa WADAKU wa Mbele, Mkali huyo wa RnB amekutana na Nyundo hiyo baada ya kukamatwa na Askari akiendesha Gari kwa Kasi huku harufu ya Pombe ikiwa imetawala ndani ya Gari L:ake.

PICHA : NAUANGALIA

12:07:00 AM Add Comment
 MAHALI PA KUKAA: RaisJakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi  mkubwa wa mikutano multi-purpose conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali(picha na Freddy Maro)



UNAONEKANA VIZURI AISEE: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi  mkubwa wa mikutano multi-purpose conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali(picha na Freddy Maro)

UKATILI: ALBINO AUAWA KIKATILI, HUKU WAWILI WAKIJERUHIWA

11:54:00 PM Add Comment

Na Vicky Ntetema
HALI ya wasiwasi imetanda miongoni mwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) nchini, baada ya watu watatu kukatwa viungo na mmoja wao kuuawa mwezi huu.


Katika miaka ya hivi karibuni, jumla ya albino 72 wameuawa, 34 wamenusurika, wengi wao kwa kukatwa viungo au kuumizwa. Makaburi 15 yamefukuliwa na viungo kuchukuliwa na kumekuwa na majaribio manne ya kufukua makaburi.

Katika matukio ya hivi karibuni, walemavu hao wakazi wa Tabora na Sumbawanga wamekatwa mikono ya kushoto. Ukatili huo safari hii umekwenda kinyume na ilivyokuwa mwaka 2010-2011 wakati mikono ya kuume ndiyo iliyokuwa inakisiwa.
Aliyeuawa ni
Lugolola Bunzari (7) na waliojeruhiwa ni Mwigulu Matonange (10) na Maria Chambanenge (39).


Katika matukio hayo, mtoto mwenye umri wa miezi saba alinusurika kuuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia nyumba ya mama yake usiku katika eneo la Lamadi, Wilaya ya Busega, Mwanza siku moja baada ya kupokea ujumbe mfupi wa simu kwamba mtoto wake anawindwa.


Marehemu Lugolola
Kijiji cha Kanoge kina umbali wa takriban kilomita 75 kutoka Tabora Mjini, barabara iendayo Ulyankulu kwenye machimbo ya dhahabu.
Imenichukua saa mbili na nusu kufika huko. Saa moja na nusu kati ya hizo, nilizitumia katika safari ya kilomita 15 tu kutoka Kanoge makao makuu ya kijiji hadi Kitongoji cha Kinondoni alikouawa mtoto Lugolola.


Nyumbani kwa Bunzari niliwakuta ndugu na jamaa kutoka vijiji vya jirani vya Wilaya hiyo ya Kaliua, Tabora. Bibi mzaa baba wa Lugolola, Gama Zengabuyanda (60), ndiyo kwanza alikuwa amerejea kutoka Hospitali ya Mkoa ya Kitete alikokuwa akitibiwa baada ya kushambuliwa na majambazi alipotaka kumwokoa mjukuu wake.


Huku akilia kwa huzuni, Zengabuyanda alinisimulia jinsi mjukuu wake na baba yake mzazi, Zengabuyanda Meli (95) walivyouawa kikatili.


Katika muda wa kati ya saa 10 na 11 alfajiri ya kuamkia Februari Mosi mwaka huu, Lugolola aliuawa kikatili baada ya kukatwa mkono kwa panga, kukwanguliwa nywele, kujeruhiwa mkono wa kulia na sikioni na kuondolewa ngozi kwenye sehemu ya paji la uso.


Katika mashambulizi hayo, babu yake Meli pia aliuawa alipojaribu kumwokoa mjukuu wake. Vilevile baba yake mzazi, Bunzari Shinga alijeruhiwa wakati alipojaribu kumlinda mwanaye.
Nilimkuta mama mzazi wa Lugolola aitwaye Kulwa akisaidiana na ndugu zake kumenya maharage mabichi waliyoyatoa shambani mwao muda mfupi tu uliopita.


Yeye ni mke mkubwa wa Bunzari Shinga (35). Walibahatika kupata watoto sita, wawili kati yao ni albino. Lugolola na marehemu mdogo wake aitwaye Maganga aliyefariki kwa malaria mwaka 2011.


Usiku wa mashambulizi hayo, Kulwa anasema alikuwa amelala na watoto wake wadogo wa kike (mmoja, Shija mkubwa) na Lugolola kwenye nyumba yake inayotazamana na ile ya mke mwenzake Pili, umbali wa takriban mita 20. Bunzari alikuwa amelala kwa mke huyo mdogo na binti yao mwenye umri wa mwaka mmoja hivi.


Mzee Meli alikuwa amelala na watoto wa kiume upande wa kulia wa nyumba ya Kulwa.
“Aliamshwa usingizini na kelele za watoto waliokuwa wakilalamika kwamba wanapigwa na fimbo. Alipotaka kwenda chumbani kwa watoto alishambuliwa kwa mapanga kichwani, usoni, mgongoni, mikononi na miguuni,” Gama anaelezea huku akilia.

OFISI YA WAZIRI MKUU: TUMETOKELEZEYAAA!!!!

11:49:00 PM Add Comment

TUNAFURAHA: Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akifurahia jambo wakati wa mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh (kushoto) na Mkaguzi  Mkuu  wa hesabu za Serikali wa Sweden  Jan Lindahr Hjelmaker. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

FAGIO LA MWAKYEMBE: 11 KIKAANGONI TPA TANGA

11:51:00 PM Add Comment


FAGIO la Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe la kusafisha uozo katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) sasa limehamia katika Bandari ya Tanga ambapo jumla ya wafanyakazi 11 wamepewa barua za kujieleza walivitoa wapi vyeti walivyowasilisha kwa mwajiri wao.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Meneja TPA Tanga, Awadhi Massawe  zilisema wafanyakazi hao ni wale waliopata ajira mpya  Septemba mwaka jana na hatua ya kuwaandikia barua imefikiwa baada ya kuwasiliana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) .

Wafanyakazi hao ni wa Idara za Operesheni, Marine na Ulinzi ambao waliajiriwa  mwaka jana baada ya nafasi zao kutangazwa na kufanyiwa usaili.

Wafanyakazi hao waliopewa barua za kujieleza ni 11 kati ya waliofuzu usaili uliosimamiwa na maofisa wa TPA Tanga na baadaye  kuonekana kufanya vizuri kuwashinda waombaji wengine.

“Hapa bandarini sasa hivi hakuna raha kila mtu ana wasiwasi, hawa  vijana walishaajiriwa na kulipwa mishahara, lakini leo wanaambiwa kuwa hawafai, imetushtua sana,”alisema mfanyakazi aliyejitambulisha kwa jina moja la Mariam.

Ilielezwa kuwa barua za kuwataka watoe maelezo ya vyeti vyao zilianza kusambazwa Jumatatu wiki iliyopita na kwamba hivi sasa baadhi yao hawafiki tena kazini kutokana na kuhofia kukamatwa.

Akithibitisha habari hizi, Massawe alisema ni kweli kuna watumishi 11  waliopewa barua za kujieleza juu ya vyeti vya kuhitimu kidato cha nne na sita, lakini bado hawajafukuzwa kazi.

Meneja huyo alisema katika kipindi cha kukamilisha mkataba wa waajiriwa hao, TPA iliwasilisha vyeti vyao kwenye NECTA ili kujua kama ni halali au la, ndipo ikabainika hao 11 vyeti  vyao havikutoka NECTA.

Alisisitiza kuwa wakati wa ubabaishaji katika kutoa ajira TPA sasa umekwisha ili kuleta ufanisi.
 sheria ili kuleta ufanisi na kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa  yakijitokeza mara kwa mara.

“Baada ya NECTA kuvikana  vyeti vya waajiriwa hao wapya, polisi wameanza kufanya uchunguzi ili kuwafikisha mahakamani kwa kughushi vyeti,” alisema.

Inasemekana vyeti hivyo vyote bandia vimetengezwa sehemu moja iliyopo jijini Dar es salaam na kwamba ilibainika hivyo baada ya mmoja wa  wafanyakazi hao kubanwa na kuwataja wengine kuwa wote wamechapishiwa na mtu mmoja.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Constantine Massawe hakutaka kuelezea juu ya sakata hilo na kusisitiza kuwa atazungumza na  vyombo vya habari mara uchunguzi utakapokamilika.

MWANANCHI

TAARIFA: RUSHWA KUITAFUNA JWTZ

11:36:00 PM Add Comment


TANZANIA imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na tatizo la rushwa ndani ya jeshi.Taasisi ya Transparency International (TI), ambayo hutafiti masuala ya rushwa duniani imeitaja Tanzania kwamba jeshi lake lina rushwa kubwa na ndogondogo.

Kwa mujibu wa gazeti dada la The Citizen la jana Jumapili, uongozi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) umekanusha vikali taarifa ya taasisi hiyo.

TI inadai katika taarifa yake kuwa sekta ya ulinzi ya Tanzania inakabiliwa na tatizo hilo na hiyo ni kutokana na mambo yake kuendeshwa kwa usiri mkubwa.

“Hakuna kitu kibaya kama la rushwa kwenye jeshi, maana kuna fedha nyingi inatembea kutokana na ughali wa vifaa vya kijeshi. Bado Serikali nyingi zinafanya mambo haya kuwa siri na kutoa mwanya kwa rushwa kutembea.
“Fedha inayotumika vibaya kwa masuala ya kijeshi, ingeweza kutumia vizuri zaidi katika masuala ya maendeleo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo iliyoandikwa na Mark Pyman, ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha masuala ya Ulinzi cha Transperancy International.

Transparency International inaeleza kuwa fedha ya rushwa inayotembea kwenye sekta ya ulinzi inakadiriwa kufikia kiasi cha Dola 20 bilioni (Sh32 trilioni).

“Ripoti ya Transparency International itufungue macho Watanzania maana kwa kawaida huwa kila watu wakihoji mapato na matumizi ya jeshi tunaambiwa hatuwezi kujibiwa kwa madai ya woga wa kuhatarisha usalama wa taifa,” alikaririwa mbunge mmoja na gazeti la The Citizen.

Tanzania, hata hivyo, iko juu ya nchi nyingi za Afrika kwa tatizo la rushwa ingawa inatakiwa kurekebisha mianya mingi kwenye sekta hiyo.

“Tunaona Tanzania ina changamoto ya kuimarisha vyombo vya kutupa jicho kwenye jeshi. Mathalani, kuna Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Mambo ya Nje, lakini haina meno ya kuingia kwa undani masuala ya kijeshi,” iliongeza Transparency International.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, hata hivyo, alikaririwa na gazeti la The Citizen akidai kuwa taasisi yake imekuwa ikifanya kazi kitaalamu na kimaadili akitolea mfano jinsi wanavyoajiri wanajeshi kwa kufuata vigezo.

Transparency International inasema kuwa kuna Kitengo cha Utawala Bora cha Serikali ambacho hufanya ukaguzi kwenye jeshi ingawa halijatoa ripoti ya aina yoyote kuhusiana na ukaguzi wa bajeti ya jeshi. “Mfano kuna taarifa kuwa Kitengo cha Kilimo cha Jeshi la Kujenga Taifa (Suma-JKT) kuna kinajishughulisha na uchimbaji madini na biashara nyingine lakini kuna udhibiti mdogo,” iliongeza taarifa yao.

Julai mwaka jana, maofisa saba waandamizi wa Bodi ya Zabuni ya Suma-JKT walifunguliwa mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi na uhamishaji usio wa halali wa zaidi ya Sh 3.8 bilioni.
Waliotuhumiwa ni pamoja na Kanali Ayoub Mwakang’ata, Luteni Kanali Mkohi Kichogo, Luteni Kanali Paul Mayavi, Meja Peter Lushika, Sajini John Laizer, Meja Yohana Nyuchi na Luteni Kanali Felix Samillan wanaodaiwa kufanya makosa hayo mwaka 2009.

Tanzania imewekwa katika Kundi D kwenye orodha hiyo ya Transperancy International ya nchi zinazokabiliwa na kiwango cha juu cha rushwa na vigezo vinavyoangaliwa ni sekta za siasa, fedha, utumishi wa Kundi la D ni nchi ambazo zinakabiliwa na kiwango cha juu cha rushwa na katika orodha hiyo zimo pia nchi za Russia na China.

Hata hivyo, nchi zenye kiwango cha juu cha rushwa ziko katika Kundi F wakati zile zenye kiwango cha chini cha rushwa ziko Kundi A.

MWANANCHI

IKULU: RAIS KIKWETE KUHUDHURIA MAZISHI YA BABA WA RAIS MUSEVENI

11:25:00 PM Add Comment


AHSANTENI SANA KWA UKARIMU WENU : Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa jana jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es salaam leo, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta, aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake


KWA HERI MHESHIMIWA..KARIBU TENA : Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati) na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete wakati ndege yake ikiondoka uwanjani hapo leo jioni ya  Februari 24, 2013.

Picha na IKULU

AFYA: MUHIMBILI NA AGA KHAN KUTOA HUDUMA YA UPASUAJI WA MOYO

11:17:00 PM Add Comment


HUDUMA za matibabu na upasuaji wa moyo zitaanza kupatikana nchini, kutokana na mipango ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na ile ya Aga Khan.

Hatua hiyo itawawezesha wagonjwa wa moyo nchini kutopelekwa kwa wingi nje ya nchi kama ilivyo sasa. Pia itaokoa mamilioni ya fedha ambazo zimekuwa zikitumika kugharimia tiba hiyo nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Huduma za Afya wa Hospitali za Aga Khan Tanzania, Dk Jaffer Dharsee akiwasilisha taarifa kuhusu ongezeko la magonjwa ya moyo nchini katika kongamano la wataalamu wa magonjwa hayo alisema, jitihada kubwa zinafanywa ili kuhakikisha tiba ya moyo inaanza kutolewa nchini.

Alisema Hospitali ya Muhimbili inakusudia kuanza kutoa tiba hiyo katika kipindi cha miezi miwili ijayo baada ya ujenzi wa taasisi yake kukamilika, wakati Hospitali ya Aga Khan itaanza kutoa matibabu hayo mwakani. Kongamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Hatua ya kuwapo kwa tiba za moyo nchini, itawezesha gharama za tiba kupungua kwa asilimia 57.1, ikilinganishwa na gharama za tiba hizo nje ya nchi.

Dk Dharsee alisema hapa nchini gharama za tiba zitakuwa Dola za Marekani 1,500 sawa na Sh2.4 milioni tofauti na Dola 3,500 (Sh5.6 milioni) zinazotumika kumpeleka mgonjwa kwa ajili ya upasuaji nchi za nje kama India.

Alisema gharama hiyo inatokana na kuwapo kwa gharama kubwa zinazohitajika kuandaa maabara hiyo ambayo ina thamani ya Dola 200 milioni (Sh320 bilioni) bila kuingiza gharama za wataalamu wa kuiendesha na kuhudumia wagonjwa.

SAKATA LA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE: MTIHANI ULIKUWA KATIKA MFUMO TOFAUTI

11:09:00 PM Add Comment


Na Fredy Azzah na Kelvin Matandiko 
MATOKEO mabaya ya mtihani wa kidato cha nne yamezidi kuibua mapya, baada ya wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini kusema mitihani ilitungwa kwa mfumo tofauti na uliozoeleka miaka yote, huku tume iliyounndwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ikipondwa na baadhi ya watu.Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi nchini (TAMONGSCO), Mahmoud Mringo alisema kwamba maswali waliyoulizwa watahiniwa yalikuwa ya kujieleza tofauti na miaka ya nyuma, ambapo
mfumo uliotumika uliwataka watahiniwa kutaja vitu tu bila ya kulazimika kuvielezea kwa undani.

Kauli yake iliungwa mkono na Mkuu wa Taaluma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Marian, Florence Mapunda ambaye alisema kuwa mtihani wa mwaka jana ulitaka zaidi watoto kujieleza tofauti na 
miaka ya nyuma wakati wanafunzi walipokuwa wanakariri.

Hata hivyo, Msemaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), John Nchimbi alisema mfumo wa mtihani haukubadilika kwa namna yoyote na kuwa upo kama ule wa miaka yote.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo, kwa upande wake alisema madai yanayotolewa hayana msingi, huku akihoji kwa nini yasitoke tangu mitihani ilipokuwa ikifanyika na badala yake yanatoka baada ya kutangazwa kwa matokeo.

Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yanaonyesha kuwa watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.
Kutokana na matokeo hayo, Waziri Mkuu Pinda, juzi alitangaza kuunda tume ya kuchunguza chanzo cha matokeo hayo kuwa mabaya, hatua ambayo hata hivyo imekosolewa na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Tume hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka Taasisi za Elimu, Chama cha Waalimu, Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahossa) inatarajiwa kuanza kazi wiki hii.

Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema kuunda tume ni kupoteza muda kwa sababu matatizo na changamoto zote ndani ya sekta hiyo yanajulikana, huku mwenzake, Profesa Chriss Maina pia wa UDSM akisema kuunda tume hakutaisaidia kwa kuwa Serikali inaidharau sekta ya elimu.
“Tatizo ni kutowekeza kikamilifu katika sekta ya elimu, imekuwa na matumizi makubwa katika mambo yasiyokuwa ya lazima,”alisema Profesa Mpangala.

Alisema matatizo mengine ni mazingira magumu ya kufundisha na uhaba wa walimu. “Kinachotakiwa wajipange kufanyia kazi changamoto hizi zilizopo badala ya kuunda tume, wakati fedha nyingi tunasikia inapotea kwenye ubadhirifu,”alisema Profesa Mpangala.

Naye Profesa Maina alisema: “Hiyo tume ya kazi gani kwa sababu matatizo yanafahamika wazi, umewahi kusikia taifa gani ambalo halina mtalaa wa elimu. Hiyo ndiyo hali halisi kwa nchi yetu. ”

KENYA: NAULI YA Kshs 20 Yaua Abiria

3:50:00 AM Add Comment


Mwanamume amefariki baada ya kutupwa nje ya Gari aina ya matatu kufuatia ugomvi kuhusu nauli ya shilingi 20 katika barabara ya Juja hapa Nairobi. 

Polisi wanasema kwamba mwanamume huyo alizozana na kondakta wa matatu hiyo kabla ya kusukumwa nje ya matatu hiyo mwendo wa saa tano jana usiku. Polisi wanawasaka wahudumu wa matatu hiyo walitoweka kwa gari hilo, mara tu baada ya tukio hilo.Kisa hiki kimetokea mwezi mmoja tu baada ya tukio sawa na hilo kutokea mtaani Kawangware ambako mwanamke mmoja aliskumwa nje ya basi kufuatia ugomvi kati ya na kondakta kuhusu nauli ya shilingi 10.

ISTA-FATHER

3:45:00 AM Add Comment

Picha ya Wizzy Khalifa ambayo aliipost katika Mtandao wa Instagram "Ready to Be a Fathere" wakati wa hati hati za Amber Kujifungua.

Hongera za Dhati kwa Amber Rose na Wizzy Kahlifa kwa kupata Dume..

PICHA : RAIS KIBAKI ALIPOTEMBELEA KIWANDA CHA MAGEREZA-UKONGA

3:35:00 AM Add Comment
  
TWENDE TUKAJIONEE: Rais wa Kenya, Mwai Kibaki (wapili kutoka kulia) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili kutoka kushoto),  Mkuu wa Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia) pamoja na maofisa mbalimbali kutoka nchini na Kenya, wakiingia ndani ya kiwanda hicho.


 SALAM YA KENYA NA TANZANIA: Rais wa Kenya, Mwai Kibaki (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Magareza nchini, Kamishna Jenerali John Minja kabla ya kuingia ndani ya  Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, anayefuata ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.

KITI CHA WAPENDANAO: Rais Mwai Kibaki (wa kwanza kutoka kulia aliyevaa tai) akiwafurahia Askari Magereza na ofisa kutoka nchini Kenya wakiwa wamekaa kwenye kiti cha wapendanao kilichotengenezwa na wafungwa kiwandani humo.

ITASAIDIA SANA KATIKA AJALI: Mshauri Mtaalamu wa Mradi wa Kiwanda cha kutengeneza kofia ngumu katika Jeshi la Magereza, Alpherio Moris (kulia) akimuonyesha Rais Mwai Kibaki moja ya kofia ngumu (Helmet) ambayo inatarajiwa kutengenezwa na kiwanda cha magereza Ukonga hivi karibuni.

POKEA KIDOGO TULICHO NACHO Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jeneral John Minja (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum ya kiti Rais Mwai Kibaki wa Kenya.

PAMOJA: Rais Mwai Kibaki akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali nchini pamoja na maofisa kutoka nchini Kenya.


HAKIKA NIMEJIONEA MWENYEWE: Rais Mwai Kibaki (wa pili kushoto) akiwa na maofisa mbalimbali wakiondoka Kiwanda cha Magereza Ukonga baada ya kumaliza kuangalia vifaa mbalimbali vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.




PICHA ZOTE NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

TANZANIA YANG'ARA LONDON

3:18:00 AM Add Comment




CHANZO: Urban Pulse na Freddy Macha
Jumapili mchana  wilaya ya Westminster jijini  London ilikuwa na mashindano ya ubunifu na urembo katika maonyesho  ya kimataifa ya London Fashion Week. Mashindano haya yalifanyika jumba la Somerset lililosimama imara  kwenye upembe wa  kaskazi ya mto Thames.

Maonyesho ya London Fashion Week, bado yanaendelea jumba hili  la Somerset toka tarehe 14 hadi tarehe 28. Wiki hizi mbili nzima zitakutanisha kila mtu anaye husika na biashara ya mavazi na urembo. Magwiji na mapapa wa mitindo, wabunifu, walimbwende, watafuta vipaji, wafanya biashara, wazalishaji mali ghafi na wamiliki viwanda.  Wote hukutana katika maonyesho haya. Hapa si vipaji tu vinavyojionyesha, bali pia watu wa biashara.

Siku hii Tanzania ilikuwa moja ya nchi mbili tu za Kiafrika zilizochaguliwa na British Council na LFW kushiriki kwenye mashindano  ya kutafuta vipaji chipukizi kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi na urembo.  Watanzania Anna Lukindo, Jacqueline Kibacha na  Christine Mhando ndio wasanii waliobeba bendera ya taifa letu na kutuwakilisha katika mashindano haya ya kimataifa yanayofanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka 27 sasa.

Katika kuunga mkono maendeleo ya Tanzania na Watanzania,  Ubalozi wetu  Uingereza na Bodi ya Utalii Tanzania, nao pia walichukua nafasi hii kuwasaidia wananchi hawa kufanikisha mahitaji yao ya ushindani. Ubalozi umetoa Ukumbi wa Nyumba Ya Tanzania ulioko Bond Street ili wasanii hao waweze kuonyesha nguo na sanaa zao kwa juma zima kama sheria za London Fashion Week zinavyoamuru. Vile vile Bodi ya Utalii ya Tanzania imesaidia katika mchango  wa mali ghafi zilizotumika katika shughuli hizi  ili kuiuza Tanzania kimataifa.

Mshindi wa tukio alikua Estonia. Ingawa  Tanzania haikuwa mshindi wa mwanzo- ilichaguliwa kati ya Kumi Bora jambo ambalo limetikisa nyoyo na vichwa vya  waandaaji, wabunifu,wafanya biashara na watafuta vipaji vya kimataifa. Hii ni mara ya kwanza kwa taifa letu kushiriki katika shughuli na  wote wameguswa na kupumbazwa na usanii wa hali ya juu ulioonyeshwa na wasanii  watatu wa Kitanzania.   Lukindo, Mhando na Kibacha wamechukua nafasi waliyopewa kwa mikono miwili na wote wameisogeza Tanzania hatua moja zaidi ndani ya ulingo wa kimataifa na katika biashara hii ya mavazi na urembo ambayo inasemekana ina thamani ya  Pauni Billioni 10  ama  shilingi Trillion 25 za Tanzania.


UJANGIRI TENA

3:15:00 AM Add Comment



Na Hamza Mashole  wa  Songea
Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA kwa kushirikiana askari wanyamapori wa Selou na Askari wa vijiji vinavyozunguka pori la Akiba la Selou wamefanikiwa kukamata meno ya tembo 15 yenye thamani ya milion miambili, Risasi 9, Bunduki moja aina ya RIFFLE 458 na Gobole moja ambavyo hutumika kuulia wanyama .

Doria hiyo imechukua takribani siku tatu katika pori la Akiba la Selou ikiwa ni sehemu ya kuwatafuta majangili wanaofanya mauaji ya wanyamapori katika pori hilo,
Akizungumza na mwandishi wetu Bw. Mohamed Mpapa ambaye ni mwakilishi wa kampuni hiyo ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA, Amesema kuwa hiyo ni kujituma kutokana na motisha ya fedha anayoitoa mwezeshaji wa kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA ndio chachu ya mafanikio ya kukamata meno,bunduki na risasi.

 Akiendelea kuzungumzia tukio hilo Bw. Mohamed Mpapa amesmea baada ya majangili kuwaona Game Frontiers Tanzania wakiwa katika doria ndani ya pori hilo huku wakiwa wamekamilika kimapigano majangili hao waliweza kukimbia na kuacha nyara hizo baada ya kuona nguvu yao ni ndogo katika kupambana na kundi la doria.

Ameongezea kwa kusema Kampuni yake imefurahishwa na mafanikio na ushirikiano uliopo kati yao, Serikali na wanavijiji kukabiliana na ujangili unaoendelea kuwamaliza tembo katika Pori la Akiba la Selou pia ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano katika kuwafichua majangili.

Nae Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la Selou Bw. Bernald Lijaji amesema Pembe zilizokamatwa ni 15 pamoja na Bunduki aina ya RIFLE 458,Gobole moja na Risasi 9 aina ya 458 vimekamatwa katika Doria iliyofadhiriwa na Mwekezaji wa Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA

PICHA: PUMZIKA KWA AMANI PADRE EVARIST

4:54:00 AM 1 Comment
PUMZIKA KWA AMANI PADRI EVARIST MUSHI. BWANA AMETOA...NA BWANA AMETWAA. UWASAMEHE WALE WOTE WALIOKUTENDEA UNYAMA HUO, MAANA KAMWE HAWAJUI WALITENDALO

ZA FASTA: AMBER ROSE YUKO LABOUR

4:49:00 AM Add Comment
Mamito Amber Rose ambaye ni Mchumba wa Wiz Kharifa, inasemekana kuwa Yuko Labour, na Muda wowote tunaweza kupata taarifa Njema za Kujifungua kwake.
Mungu Amsaidie, na tutaendelea kuwajuza kitakachojiri hapa hapa BLACK TOUCHEZ

PICHA : NAZINDUA KIWANDA CHA KUSINDIKA MBEGU ZA PAMBA

1:13:00 AM Add Comment

MBEGU NZURI SANA HIZI: Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mbegu za pamba wakati alipofungua kiwanda cha kusindika mbegu za pamba za kisasa cha Quton kilichopo Bariadi Februari 18, 2013. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti.



NAKATA UTEPE: Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua kiwanda cha kusindika mbegu za pamba za kisasa  cha Quton kilichopo Bariadi Februari 18, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti  na Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho, Morgan Nzwele. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MNADA BANNER