REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

DECEMBER HII....MTOTO MTUKUTU ANAZALIWA

3:21:00 AM Add Comment

Ikiwa ni Umoja wa Vijana Wadogo lakini wanauwezo wa Kufika Mbali na Kuikuza Tasnia ya Habari, Hatua ya awali itafanyika Hivi.

Hiki Kitakuwa na Kijiji ambacho kitadhihirisha Rasmi Taaluma yao na Uwezo wao Mkubwa wa Kukufikia wewe kwa Namna yoyote Ile.

Mawazo yao yamesheheni Ubunifu Mkubwa na Ari ya ajabu katika kufanikisha ndoto zao na Jamii inayowazunguka Kiujumla

Endelea kufuatilia Hapa hapa kwa Taarifa Zaidi. Ahsante

Imetolewa na 
SAFIYA MOHAMED RASHID
Kaimu Afisa Habari wa HATUA (HAMECO)

JACK WA CHUZI "ATAUAWA " JACOB KWA DHURUMA YA 325,000/=

3:03:00 AM Add Comment
                                                    Jackline Pentzel "Jack Wa Chuz"

IKO HIVI...


MAISHA ya msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ yako hatarini kufuatia ujumbe wa kumuua unaosambazwa na muongoza filamu, Mandela Nicholas ‘Jacob’ anayedai kudhulumiwa na msanii huyo kiasi cha shilingi 325,000.

Kwa mujibu wa ujumbe huo, jamaa huyo amedhamiria kumfanyizia Jack kwa kumcharanga mapanga kisa eti kadhulumiwa kiasi hicho cha fedha ambazo ni malipo ya kumuongozea filamu yake.

Jacob anadai kuwa, awali alimuandikia ‘script’ na kumuongozea filamu msanii huyo lakini kabla kazi haijaisha, wakazinguana hadi kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo Ilala jijini Dar.

Hata hivyo, mahakama alimuamuru Jack alipe fedha hizo lakini kinyume chake msanii huyo akawa mgumu kutekeleza, hivyo kwa hasira Jacob akamuandikia Jack sms hiyo ya vitisho.

Sehemu ya ujumbe huo inasomeka hivi; 

 “Labda kifo kiniite leo Jack nitamuua, kama laki 325,000 hajanipa mtasikia. Kama rafiki au ndugu jiandae na mazishi ya marehemu Jk Pentzel full panga tu.”

Sehemu nyingine ya ujumbe huyo ilisomeka hivi;

“Wapendwa Jack anachohitaji sasa ni kifo na nitamuua kweli, mimi simsukumi…ila mapanga tu ndiyo dawa yake.

“Utapeli utamuua Jaki, leo kesho, keshokutwa mkisikia msiba ulizia kapigwa panga au? Kama siyo panga siyo Jacob, kama panga na vipande 150 ewaa. Yeye kaburini mimi Segerea. Jasho la mtu haliliwi.”

Akizungumza na mwandishi wetu kuhusiana na sms hiyo, Jack alisema kuwa naye ameipata na katika kujihakikishia usalama wa maisha yake amekwenda kuripoti polisi na kupew

CHEKI VIMWANA WA SHINDANO LA"UNIQUE MODEL 2012" Wakila Bata !!

2:50:00 AM Add Comment




PICHA NA DAR TALK

HAYA NDIYO YALIYOIKUMBA NDOA YA SANDRA

2:45:00 AM Add Comment


                                                                           Sandra
IKO HIVI....
Sandra aliyeolewa na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Haisam na kufanikiwa kupata watoto wawili, inadaiwa ndoa yao imefikia ukingoni kutokana na wawili hao kutofautiana.

Kwa mujibu wa MPEKUZI, mmoja wa ndugu wa mwanaume aliyeomba jina lake lisiandikwe mtandaoni alisema, wawili hao waliachana hivi karibuni baada ya kuona ndoa yao ‘inanyevuliwa’.

“Ni kweli wameshindwana na sasa kila mmoja yuko kivyake,” alisema ndugu huyo.

Sandra alipotafutwa kuzungumzia hilo hakuwa tayari kutoa ushirikiano, mumewe hakuweza kupatikana ila mdogo wa mume ambaye ni Miss Tanzania 2012, Salha Israel alikiri ndoa ya kaka yake kusambaratika.

CONFIRMED : John Mnyika Hana Ubishi UBUNGO..Ashinda Kesi !!

2:37:00 AM Add Comment
 Mbunge Wa Jimbo La Ubungo kwa Tiketi ya Chama Cha Deokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameshinda Kesi iliyokuwa Ikimkabili, dhidi ya Wizi wa Kura

Akipokelewa kwa Shangwe

RAIS KIKWETE aliandaa Chakula Jioni na Wajumbe wa GAVI FORUM

1:40:00 AM Add Comment
 Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Aliyekuwa Mke wa Rais wa Afrika Kusini, Bi. Graca Machel, Ikulu

 Hawa Ni Wageni Waalikwa
 Rais Jakaya Kikwete Akipokea zawadi ya CD ya Nyimbo za Afrika ya Kusini 

Wakibadilishana Mawazo

PICHA NA IKULU

Mh. Mwalimu Aliahidi Haya...

12:53:00 AM Add Comment

 

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya pinga unyanyasaji na matusi sokoni iliyofanyika Soko la Kivukoni, Ferri Jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa siku 16 za kupinga unyanyasaji kijinsia.

 

Naibu Waziri Ummy Mwalimu na Balozi wa Uingereza nchini Diana Croner, wakikata utepe kuzindua mabango yatakayobandikwa katika masoko mbalimbali yakihamashisha kupinga vita dhidi ya unyanyasaji kijinsia na matusi sokoni



Naibu Waziri Ummy akiwa na wanawake wafanyabiashara kutoka masoko ya Ilala wakionyesha mabango ya kupinga matusi katika masoko.
                                     ************************************************************

NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, ameahidi kuwa atahakikisha vinapatikana vituo maalum vya kuripoti taarifa za unyanyasaji na matusi katika masoko na magulio wilaya ya Ilala ili kurahisisha mapambano dhidi ya unyanyasaji.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za siku 16 kupinga unyanyasaji kijinsia katika soko la Kivukoni Feri leo iliyobebwa na kauli mbiu ya “pinga unyanyasaji na matusi sokoni” “nipe riziki na si matusi” iliyozinduliwa katika masoko matano ya Ilala, Kigogo Saambusa, Kibasila, Mchikichini na Feri.

Amesema kuwa, kutokana na hali halisi, wanawake wanapaswa kutoa taarifa katika madawati maalum katika vituo vya polisi, lakini kutokana na umbali wa vituo hivyo anaangalia uwezekano wa kusogeza huduma hizo kwenye masoko hayo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, ameeleza kuwa, katika tafiti zilizofanywa zinaonyesha kuwa asilimia 43 ya wanawake wamejikita katika ujasiriamali katika sekta isiyo rasmi ambapo wanakabiliwa na changamoto kadha wa kadha ikiwemo mitaji midogo, maeneo madogo ya kufanyia biashara wakijihusisha na biashara kama za mama ntilie, ushonaji, kutengeneza batiki na nyinginezo.

Ameongeza kuwa, utafiti uliofanywa katika masoko 10 ya jijini Dar es Salaam unaonyesha kuwa wanawake wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya unyanyasaji ukatili wa kingono, matusi na kiuchumi.

AKILI YANGU ILIVYO FINYU : Baada Ya TANESCO Kutunyima Umeme kwa Siku Nzima Jana..

12:51:00 AM Add Comment
Wadogo Zangu Ashura Mnyika Na Fortunata GervaZ Wakicheza Karata katika Mchezo wa "LAST CARD" baada ya Tanesco Kutunyima Umeme...Ilisukuma Muda Off Course...

MNADA BANNER