REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MATUMIZI YA DEODORANT YANA MADHARA MAKUBWA KATIKA CANCER.

7:20:00 AM Add Comment


Na Dr. Felician Kiyando, 
NI DHAHIRI kabisa kuwa Wanawake wanapenda sana kutumia Deodorant kwa ajili ya Manufaa ya Afya zao, na hata maumbile yao Pia

Lakini kwa Wanawake ambao wanatumia Deodorant zenye ALUMINIUM SALTS wanaweza kuwa katika hatari ya kukumbana na Ugonjwa wa Cancer ya Titi, na hii ni kwa Mujibu wa Utafiti ambao umefanyika hivi karibuni, yaani utafiti Mpya

Watafiti kutoka Uswiss wanasema kuwa, matumizi ya Muda Mrefu ya ALUMINIUM CHROLIDE, yanaweza kusababisha kusambaa kwa Cancer katika maeneo mengineyo pia ya Mwili
Ingawa utafiti wa awali, yaani wa zamani uliweka wazi kuwa, matumizi ya Deodorant hizo, ni salama kwa afya ya binadam


Utafiti huu mpya, umefanywa na Chuo cha Geneva, na inasisitizwa  kuwa, kuna hatari ya ongezeko la Ugonjwa huu wa Cancer kwa Wanawake hasa wakitumia bidhaa hizi ambazo zinamadini haya ya ALUMINIUM, katika maeneo ya Vikwapa.

Pia utafiti huo unaongeza kuwa, Madini haya ya aluminium, huziba yale matundu yanayoruhusu utoaji wa jasho katika kikwapa kutoka katika tishu za Titi na kutengeneza oestrogen ambazo ni kama athari

THE GAME: HUU MSALA MWINGINE. AMEHUSISHWA NA WIZI WA GARI AINA YA POSCHE

7:05:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
KUNA uwezekano Mkubwa kabisa Huu mwaka ukawa ni mwaka Mbovu sana kwa Rapper The Game kutokana na kuhusishwa sana katika Kashfa za Wiz wizi

Safari Hii, The Game ambaye anatarajia kuachia Albamu yake mpya 1992, amehusishwa na Wizi wa Gari aina ya Posche ambayo ilikuwa imeporwa kwa muda Kidogo.

Picha Lilichomeka kipindi ambacho The Game Yuko Balmore Nchini Marekani, ambapo moja kati ya Vijana ambaye pia ni Rafiki yake  BIKER BOY SEAN, alileta Mchuma huo katika Kiwanja amacho Game na washkaji wengine walikuwa wamechill na kuoneshana maujuzi ya kudrive.

Na baada ya Muda kadhaa, Game alipost Picha akiwa ndani ya Gari hilo la Wizi na kijana huyo, kitu ambacho kilionesha dhahiri kuwa alikuwa na Connection na Mwizi huyo

LIL WAYNE: NIMEWAHI KUOA WANAUME WAWILI GEREZANI.

6:58:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
KITABU CHA LIL WAYNE kama utakuwa unahitaji kucheka na kufahamu yale ambayo alikuwa akiyafanya na hata kupitia wakati yuko Gerezani, basi Jiandae kukipata na hata kukutana na Vituko kadha wa kadha

Kitabu Hicho ambacho kitatoka OCTOBER 11, kinazungumzia Mambo mbali mbali, Mengi sana, ikiwemo namna ambavyo alioa Wanaume wawili katika Gereza hilo na Kufanya Bash ambalo dah, ni hatari.

Weezy anadai kuwa kipindi amepigwa Kufuri zito katika Gereza la NEW YORK RICKERS ISLAND, manmo Mwaka 2010, aliamua kuwaoa Wanaume wawili na kuandaa party Kabisa (Kimasihara Lakini) . Na kama haitoshi, mambo ambayo yalitumika katika Party hilo, ilikuwa ni Toilet Pepa, huku wakigonga Chears kinywaji ambacho kilikuwa kina Rangi ya Gold... (Yaani Kinyesi)

Tofauti na hilo, Pia Lil Wayne amezungumzia namna ambavyo Askari wawili wa Kike walisimamishwa Kazi, baada ya kuwa karibu naye sana pamoja na kumtembelea sana katika Maeneo yake

Kwa Upande Mwingine Hit Maker Huyo wa FIRE FLAME, anadai kuwa, Demu wake alikuwa akija kumtembelea Gerezani na walikubaliana asiwe anavaa nguo za ndani , ili iwe rahisi Kumdungua kimya kimya Bila mtu kujua, lakini mwisho wa Siku, ishu hiyo haikufanikiwa, maana kulikuwa na ukaguzi mkali, na kuanza kumvalisha Boxers kadhaa kabla hajaingia kumuona Weezy.

Dawa ya watoto ya kifua kikuu kuzinduliwa Kenya

5:10:00 AM Add Comment

BBC SWAHILI
Dawa ya kwanza duniani ya kutibu ugonjwa wa kifua kikuu miongoni mwa watoto inatarajiwa kuzinduliwa leo siku ya Jumanne mjini Nairobi.

Hadi kufikia sasa,watoto hutumia dawa zinazotumiwa na watu wazima ambazo hugawanywa kusagwa na kutiwa katika maji.

Daktari Cherise Scott,mkurugenzi wa maswala ya magonjwa ya watoto katika muungano wa utengezaji wa dawa za TB ,anasema kuwa dawa hiyo mpya inaweza kuleta afueni kwa watoto milioni moja ambao huambukizwa kifua kikuu kila mwaka ,pamoja na waangalizi wao.

Kenya ndilo taifa la kwanza kutoa dawa hiyo mpya kwa raia wake huku mataifa zaidi yakitarajiwa kuendelea na utoaji wa dawa hizo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Dawa hiyo ni mchanganyiko wa dawa tatu zinazotumiwa kutibu Tb,zikiwa zimechanganywa kikamilifu na kuwekwa ladha ili kuwavutia watoto.

Inaweza kuyayuka kwa urahisi ndani ya maji,hivyobasi kuifanya kuwa rahisi kutumia kila siku katika kipindi cha miezi sita.

Hadi kufikia sasa ,waangalizi wa watoto hulazimika kuzivunja dawa hizo kabla ya kuwapatia watoto hao.Dawa hizo ambazo ziko uchungu ni vigumu kumeza.

Ugonjwa wa kifua kikuu unaongoza miongoni mwa magonjwa hatari dunia,na huwaua watu 3000 kila siku.
Dawa hiyo mpya itayasaidia maisha ya watoto zaidi

Mpiganaji wa Kiislamu kutoka Mali Al Mahdi afungwa jela ICC

5:06:00 AM Add Comment

BBC SWAHILI
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) imemhukumu mwanamgambo wa Kiislamu raia wa Mali Ahmad Al Faqi Al Mahdi kifungo cha miaka tisa jela. 

Al-Mahdi alikuwa ameshtakiwa makosa ya uhalifu wa kivita kuhusiana na kuharibiwa kwa makaburi tisa na msikiti mashuhuri katika mji wa kale wa Timbuktu, 2012.

Wakati wa kusikizwa kwa kesi yake, Al Faqi Al Mahdi alikiri mashtaka.

MNADA BANNER