KAMISHNA WA JESHI LA POLISI KITENGO CHA MAZINGIRA NCHINI UGANDA, amenusurika kuuawa na Wananchi waliokuwa wakiishi katika eneo la KYETINDA WETLAND.
Kamishna huyo, TAIRE IDWEGE, alikumbana na tafrani hiyo ambayo hakuitarajia, alipokwenda kuwaonya Wananchi hao ambao walikuwa wakiishi eneo hilo Kinyume cha Sheria ya Mazingira Nchi Humo
Taarifa zinaeleza kuwa, Kamishna IDWEGE aliponea Chupu chupu kufanyiwa Unyama huo na Wanachi wenye Mapanga makali, ambao tayari walishaanza kumzonga, Baada ya Risasi kadhaa kufyatuliwa Hewani na Jeshi la Polisi liliokuwa Eneo hilo, kwa dhamira ya kuwatawasha na kuwaogopesha
Taarifa zilizidi kumiminika kuwa, wakati Kamishna IDWEGE akitoa tamko la wananchi hao (Wavamizi) hao katika Kando ya Ziwa Viktoria kuondoka, ndipo Mmoja wa Kundi lao alisimama na kupiga kelele
"Wewe Si una nguvu?, sasa hesabu siku zako huku tukikuonesha sisi ni akina nani"
Aidha kabla tukio hilo halijatokea, Askari wenzake waliingilia kati kuzuia Adha hiyo
KYETINDA WETLAND ni eneo a,balo liko pembezoni mwa Ziwa Victoria, ambalo ni sehemu ya Vyanzo vya maji vinavyosaidia kutiririsha Maji katika Sehemu mbali mbali za Mji wa Kampala