REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KALI YA LEO : JAMANI......MPAKA MBUZI?

3:20:00 AM Add Comment
Hebu muone huyu Mpuuzi asivyo na akili. Kama Mimi ni hakimu, Ninamhukumu kwa Makosa Manne Huyu Jamaa
1. Kuwadhalilisha Wanawake
    Kwani kaambiwa wanawake wanakasoro mpaka amfuate huyu Mbuzi?
2. Kuwadhalilisha Wanaume.
    Hii ni kuonesha kuwa Wanaume hatuna akili kiasi kwamba kila kitu sisi Tuna******
3. Kavunja Haki za Wanyama.
     Tunakubali Mbuzi tunamtafuna Nyama zake kama Kitoweo...Lakini haimaanishi hii ni haki Nyingine ya Mbuzi huyu ambaye ana haki ya Kutokudharirishwa hivi
4. Ubakaji
     Sina Imani na Sintokuja Niamini Kama Huyu Mbuzi alikubali kutopa Huduma ama Burudani hii Kwa Jamaa


"STAREHE ZINAPELEKEA UMASIKINI WA KUJITAKIA"- Chuchu Hans"

1:32:00 AM Add Comment
                                                                  Chuchu Hans


MSANII wa filamu anayetokea mkoani Tanga, Chuchu Hans, amesema kuwa suala la umaskini kwa wasanii huwa linakuja kwa kujitakia kwani walio wengi wanashindwa kufanya kazi kuweka akiba ya pesa na badala yake wakipata chochote kidogo wanashinda wakifanya ufuska na uzinzi.

Chuchu alisema kuwa inawezekana wengi wanajisahau na kuamini kuwa kila siku watakuwa wanapata pesa, na ndiyo maana kila kile kidogo wanachokipata wanakitumia kwa hasara bila kujua siku ya kesho itakuwaje.

‘'Sidhani kama mashabiki wetu wanakuwa wanatuelewa wanapotuona tukifanya starehe na anasa kila siku, umaskini tunajitakia kwa sababu endapo tukiwa na tabia ya kujiwekea akiba si dhani maisha duni yatakuja tena kikubwa ni kujipanga na kuacha kujisahahu,” aliongeza.

THE MAKING OF VIDEO ya Keisha na Diamond Platnumz

1:30:00 AM Add Comment


 IN CAR SCENE.............................






 COUPLE OUT SCENE..........................




FOOD SESSION..................................




 IT'S KEISHA TIME...................


PICHA KWA HISANI YA "This is Diamond"

"JAMANI...WANAUME ACHENI KUNIPIGIA SIMU !!...MIMI SIYO SHOGA" - BOB JUNIOR

1:11:00 AM Add Comment
                                        Bob Junior "Chocolate Flavour"
IKO HIVI..................


HATIMAYE staa wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ ameifungukia skendo yake ya kwamba yeye ni shoga...

Akizungumza kupitia kipindi cha runinga moja usiku wa Ijumaa iliyopita, Bob Junior alisema chanzo cha yeye kudaiwa ni shoga ni wimbo wake maarufu wa Oyoyo.

Alisema mara baada ya kuitoa video ya wimbo wake huo akiwa anakata sana mauno, watu walikuwa wakimpigia simu, wengine wakimtumia meseji kwamba, anaonekana ni ‘chakra’ maana anayaweza sana mauno.

“Watu wanasema mimi ni shoga, lakini si kweli. Kisa kilianzia kwenye ule wimbo wangu wa Oyoyo. Unajua katika video ya ule wimbo nilikata sana mauno, watu wakaamini mimi shoga.

“Wengine walikuwa wakinitumia hata meseji wakiamini hivyo. Kwa hiyo sababu kubwa ni ile video tu, watu wana mambo ya ajabu sana,” alisema Bob Junior huku watu  alioongozana nao usiku huo wakitingisha vichwa kukubaliana naye.

Ishu ya Bob Junior kuonekana ni chakra pia iliwahi kusababisha amfikishe kortini kwenye Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akidaiwa kumtukana msanii huyo matusi ya nguoni likiwemo hilo la ushoga.

Katika kesi hiyo iliyofikishwa kwenye mahakama hiyo kwa mara ya kwanza Mei 4, 2011 na kusikilizwa na Hakimu Mfawidhi Mariam Masamalo, Wema alihukumiwa kulipa faini ya shilingi 40,000 au kwenda jela miezi 6 ambapo alifanikiwa kulipa.

KESI YA LULU BADO "MAGUMASHI" TUPU...

12:58:00 AM Add Comment
                                                    Elizabeth "Lulu" Michael


 KESI ya msanii wa fani ya filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, imeendelea kupigwa kalenda kutokana na upelelezi wake kutokukamilika.Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidaiwa kutenda kosa hilo nyumbani kwa marehemu Aprili 7, mwaka huu.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Agustina Mmbando, jana ilitajwa mahakamani hapo lakini kwa mara nyingine upande wa mashtaka uliendelea kudai kuwa upelelezi haujakamilika.Wakati kesi hiyo ilipotajwa Novemba 5, mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilisha ili hatua nyingine ziweze kufuata, Wakili wa Serikali, Seth Sekwao alidai upelelezi haujakamilika.

Kutokana na taarifa hiyo ya upande wa mashtaka, mmoja wa mawakili wanaomtetea mshtakiwa, Peter Kibatala alitaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo, ili iweze kusonga mbele.

Wakili Kibatala, ambaye pia ni Makamu Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alidai kila mara upande wa mashtaka umekuwa ukidai upelelezi haujakamilika, jambo ambalo linaifanya kesi hiyo ishindwe kuendelea katika hatua nyingine.

“Ni muda mrefu sasa, kesi hii imekuwa ikitajwa mara kwa mara upande wa mashtaka umekuwa ukidai upelelezi haujakamilika. Hivyo tunawakumbusha upande wa mashtaka ujitahidi kuharakisha upelelezi ili iweze kusonga mbele,” alidai Wakili Kibatala.

Upande wa mashtaka uliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 3, mwaka huu itakapotajwa tena kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.Lulu alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Aprili 11, mwaka huu na kusomewa shtaka moja la mauaji ya msanii mwenzake, Kanumba.

Akimsomea shtaka hilo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Elizabeth Kaganda alidai  Aprili 7, mwaka huu eneo la Sinza Vatcan alimuua msanii, Steven Kanumba.

WAREMBO 12 WAFUZU KUCHUANA VIKALI KATIKA SHINDANO LA UNIQUE MODEL 2012

12:52:00 AM Add Comment












TUME TA MABADILIKO YA KATINA YAANZA KUKUSANYA MAONI WILAYANI KARATU

12:40:00 AM Add Comment
Mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Daudi Ntibenda akizungumza na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (hawapo pichani) jana jumatatu Novemba 19, 2012 wakati wajumbe hao walipofika ofisini hapo kabla ya kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya Wilayani humo. Kushoto ni mjumbe wa Tume, Bi. Mwantumu Malale.




Akina Mama wa kijiji cha Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wakisoma nakala za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha nyepesi wakati wa mkutano wa kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya ulioitishwa na Tume  ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo jana jumatatu Novemba 19, 2012



Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Charles Masero (mwenye shati jeupe) akitoa ufafanuzi kuhusu ujazaji wa fomu za maoni kuhusu Katiba Mpya kwa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Audry Veldan kilichopo kijiji cha Shahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha wakati wa mkutano wa kukusanya maoni ya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya kijijini hapo jana jumatatu Novemba 19, 2012.



 Mkazi wa kijiji cha Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Thimos Mushi (51) akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano wa kukusanya maoni ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijiji hapo jana jumatatu Novemba 19, 2012.


Mkazi wa Kata ya Rhotia Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, John Nando (73)akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya mbele ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo jana jumatatu Novemba 19, 2012 katika Kata hiyo.

PICHA : TUME YA KATIBA










MNADA BANNER