WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
WAISLAAM 20 WAUAWA
LAGOS, Nigeria
Waislamu wasiopungua 20 wameuliwa na watu waliokuwa na
silaha baada ya watu hao kuushambulia msikiti katika kijiji kimoja cha
kaskazini mwa Nigeria.
Mauaji hayo yametokea leo katika kijiji cha Dogo Dawa
cha jimbo la Kaduna. Abdullahi Muhammad, afisa katika eneo hilo amesema kuwa
wanashuku kuwa mauaji hayo huwenda ni ya kulipiza kisasi na huenda yamefanywa
na magenge ya majambazi yenye silaha baada ya kuwapoteza baadhi ya wanachama
wake katika ufyatulianaji risasi uliojiri hivi karibuni kijijini hapo kati ya
majambazi hao na wanavijiji.
Amesema wakazi wa kijiji hicho wamekuwa
wakivamiwa mara kwa mara na watu wenye silaha wanaofanya mashambulizi kutokea
kwenye kambi zao zilizoko msituni.
UCHAGUZI TUNISIA, KUFANYIKA JUNE 2013
TUNIS, Tunisia
Serikali ya mseto ya Tunisia inayooongozwa na harakati ya
Kiislamu ya an Nahdha imetangaza kuwa imekubali kuendesha chaguzi za rais na
bunge tarehe 23 mwezi Juni ambapo rais atachaguliwa moja kwa moja na wapiga
kura.
Makubaliano hayo yamejiri baada ya mrengo wa upinzani kukosoa vikali
kwamba harakati ya an Nahdha inataka kudhibiti serikali na kukwepa uchaguzi.
Harakati ya Kiislamu ya an Nahdha ya huko Tunisia ilishinda uchaguzi wa kwanza
huru nchini humo mwezi Oktoba mwaka jana kufuatia mapinduzi ya wananchi
yaliyomng'oa madarakani Rais Zainul Abidin bin Ali.
Serikali ya mseto ya
Tunisia imesema kuwa wamefikia makubaliano ya kuendesha chaguzi za rais na
bunge tarehe 23 mwezi Juni mwaka huu, na duru ya pili ya uchaguzi wa rais
tarehe saba Julai.
29 Wauawa Nchini Somalia
Watu wasiopungua 29 wameuawa nchini Somalia kufuatia
mashambulio ya kigaidi ya ndege zisizo na rubani za Marekani.
Habari kutoka
Somalia zinasema kwamba, ndege zisizo na rubani za Marekani zimefanya
mashambulio katika maeneo yanayosadikiwa kuwa ya wanamgambo wa Al-Shabab katika
mji wa Merka kusini mwa nchi hiyo.
Mashambulio hayo ya ndege zisizo na rubani
za Marekani yamefanywa siku chache tu baada ya watu wengine kadhaa kuuawa
kufuatia mashambulio kama hayo nchini Somalia.
Ndege zisizo na rubani za Marekani
zimekuwa zikitumiwa kushambulia maeneo mbalimbali katika nchi za Afghanistan,
Somalia, Yemen, Libya na Pakistan.
Umoja wa Mataifa unailaumu Marekani kwa
mauaji yanayofanywa na ndege zisizo na rubani za nchi hiyo katika nchi
mbalimbali ukisema kuwa yanakiuka sheria za kimataifa; lakini hadi sasa
haujaichukulia hatua yoyote ile serikali ya Marekani.
Subscribe to:
Posts (Atom)