WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
MSIBA WA BI KIDUDE: DJ CHOKA AMETOA KAULI HII
Bi Kidude ndio DIVA ninayemtambua simjui DIVA yoyote hapa duniani. Rip bibi
— DJCHOKAblog (@ChokaDJ) April 17, 2013
AJALI; wanafunzi wanusurika kifo
WANAFUNZI zaidi ya ishirini wenye umri wa kati ya miaka 7 -
9 wa shule ya kimataifa ya St Charles
iliyopo Don Bosco katika Manispaa ya Iringa wamenusurika kifo baada ya gari
waliyokuwa wamepanga lenye namba T415AEG kushindwa kupanda mlima na kupinduka.
Ajali hiyo imetokea jana mchana katika eneo la Msikiti wa Hidaya katika kata
ya Mvinjeni katikati ya mji wa Iringa.
Walioshuhudia tukio hilo
wamesema daladala hilo lilikuwa likitokea eneo
la FRELIMO katika Manispaa ya Iringa kuelekea mjini Iringa na baada ya kufika
eneo hilo
lilishindwa kupanda mlima na kuanza kurudi nyuma kwa kasi kabla ya kupinduka.
Alisema shuhuda, Juma Omari kuwa chanzo cha ajali hiyo ni
uzembe wa dereva ambaye alionekana kuendesha gari hilo kwa bila kuchukua tahadhari pamoja na
kutambua kuwa mbele kuna kona na mlima.
Anasema, wananchi walitoa msaada wa kuwatoa katika daladala
na kuwakimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya
mwanamke mmoja ambae jina lake
bado kufahamika
aliyejeruhiwa vibaya mikono yake.
Mmoja kati ya wauguzi wa Hospitali ya mkoa wa Iringa ambae
hakutaka kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa Hospitali hiyo alisema kuwa hali
za watoto hao si mbaya sana
zaidi ya kupata michubuko midogo midogo.
SIMANZI: HABARI ZA UHAKIKA, NI KWAMBA BI KIDUDE AMEFARIKI.
#MADEINTANZANIA - Taarifa Zilizotufikia Hivi Punde Mwanamuziki Mashahuri Wa Taarab Almaarufu Kama Bi Kidude... fb.me/y75CKxsR
— Clouds FM (@cloudsfm) April 17, 2013
Some die with names, Some die nameless. Kazi aloletwa kuifanya KIDUDE kamaliza na hana anachodaiwa. Kupumzika ni haki na wajibu muda ukifika
— Lady JayDee (@JideJaydee) April 17, 2013
RIP Bi. Kidude *tears* loved you that much and I love u so much, can't believe this. Rest in Peace, we will miss u everyday. Sad News *tears
— Diva (@Divamimi) April 17, 2013
#BREAKING: Taarifa za uhakika za sasa hivi ni kwamba BIBI KIDUDE amefariki dunia, taarifa zaidi baadae kidogo. #R.I.P
— millardayo.com (@millardayo) April 17, 2013
RIP Bi kidude.....!we will miss u
— Shetta#TeamShetta (@ShettaTz) April 17, 2013
SUMATRA: Tumekamata Magari 70 kwa Sababu Hizi
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA) imekamata magari 70 ya abiria kutokana na kufanya makosa mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana
kuhusu kero mbalimbali zinazowakabili wananchi, Ofisa Mfawidhi Kanda ya
Mashariki wa SUMATRA , Conrad Shiyo, alisema
magari hayo yamekamatwa kuanzia juzi na miongoni mwa makosa yaliyosababisha
yakamatwe ni kutumia tiketi za bei ya zamani huku wakiwatoza abiria bei mpya,
kitendo ambacho ni sawa na kuwaibia.
“Tumegawa chati za bei kuanzia Jumatatu kwa kila gari, zenye
utambuzi wa bei ya nauli za zamani na mpya hivyo kila mwananchi anayo haki ya
kuoneshwa chati hiyo pindi anapotaka na akinyimwa kuiona hilo ni kosa na mhusika atachukuliwa hatua,”
alisema Shio.
Alisema mamlaka hiyo pia itakamata madereva ambao
wataendesha magari ambayo hayajafuta bei ya zamani ubavuni mwa magari yao na magari yote yatakayokamatwa kwa makosa mbalimbali
yatawekwa katika yadi ya mamlaka hiyo na kusubiri uamuzi wa mkurugenzi kama atayafuta kabisa au la.
Alisema nia ya mamlaka hiyo ni kuboresha hali ya usafiri
katika kila pembe ya jiji ili kila abiria aweze kusafiri na kufika anakokusudia
bila ya vikwazo vinavyotokana na tamaa za watu wasiotosheka na wanachokipata
kihalali.
Pamoja na mambo mengine alisema hivi karibuni alikutana na
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani katika kupanga mikakati
ya kuyakamata magari yote yaliyosajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma kati ya
mikoa hiyo na kunyang’anywa leseni.
UMEIONA HII
*Washirika wa Ludovick waanza kubainika
*Teknolojia ya mawasiliano yafichua siri zao
MTANDAO wa watu wanaodhaniwa kuwa washirika wa karibu wa
mtuhumiwa wa kupanga njama za kutekeleza ugaidi, Joseph Ludovick, umeanza
kufichuka.
Taarifa za kufichuka kwa mtandao huo, zimekuja zikiwa
zimepita siku tatu baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kutangaza orodha ya majina ya watu mbalimbali, wakiwemo viongozi wa serikali,
kiliodai kuwa ndio wanaopanga mipango ya kishetani kisha kuwasingizia watu
wengine.
Duru za habari kutoka vyanzo mbalimbali vya MTANZANIA
Jumatano zimeeleza kuwa, taarifa za awali za kikachero zilizokusanywa katika
mfumo wa mawasiliano ya simu ya kiganjani ya Ludovick zimeonyesha kuwa amekuwa
na mawasiliano ya karibu na baadhi ya wanahabari waliopata kufanya kazi kwa
karibu na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Mawasiliano hayo yanadaiwa kuwa ni ya mazungumzo ya simu na
ya kumtumia fedha kupitia mitandao ya kifedha ya simu za kiganjani.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mbali na wanahabari hao, pia
uchunguzi umeonyesha kuwa Ludovick amekuwa na mawasiliano ya karibu na baadhi
ya wanasiasa wa Chadema, viongozi wa juu serikalini na katika Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Mmoja wa makachero aliyezungumza na gazeti hili (jina lake
tunalifahadhi) alieleza kuwa taarifa za uchunguzi wa awali uliofanywa kwenye
mfumo wa mawasiliano ya simu ya Ludovick zimeonyesha kuwa mtuhumiwa huyo
amekuwa akiwasiliana kwa karibu na wahariri waandamizi wawili, waandishi wa
habari na wachangiaji wa makala katika magazeti mbalimbali nchini.
Kachero huyo aliwataja wahariri wanaodaiwa kuwa na
mawasiliano ya karibu na mtuhumiwa Ludovick ambao ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti
la Jamhuri, Deodatus Balile na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima,
Ansbert Ngurumo.
Balile na Ngurumo, kwa nyakati tofauti wamepata kufanya kazi
na Kibanda. Ngurumo na Kibanda walifanya kazi pamoja katika Kampuni ya Habari
Corporation Ltd, wakiwa waandishi wa habari wa gazeti la kila wiki la Rai na
baadaye walifanya kazi pamoja katika Kampuni ya Free Media Ltd, inayochapisha
gazeti la Tanzania Daima, ambako Kibanda alikuwa Mhariri Mtendaji na Ngurumo
akiwa Naibu Mhariri Mtendaji.
Kwa upande wake Balile, alipata kufanya kazi na Kibanda
katika Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd na muda mrefu baadaye Kibanda
alichukua nafasi ya Balile ya Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media, baada
ya kuondoka kwenda masomoni nchini Uingereza.
Taarifa za uchunguzi wa kikachero zilizonaswa na MTANZANIA
Jumatano zimeeleza kuwa, Ngurumo, mara kadhaa, amepata kufanya mawasiliano ya
mazungumzo na Ludovick kupitia simu yake ya kiganjani na pia alipata kumtumia
fedha kupitia simu yake hiyo ya kiganjani.
Duru za uchunguzi zinaonyesha kuwa baada ya tukio la Kibanda
siku sita baadaye, Ngurumo aliandika kupitia ukurasa wake wa facebook kuwa
ameibiwa simu yake hiyo aliyokuwa akiitumia kufanya mawasiliano na Ludovick.
Katika ujumbe wake huo, Ngurumo aliandika kuwa; “Kuna mtu
ameibia simu yangu yenye laini mbili - Tigo (0719001001) na Airtel (0782172665)
- tangu juzi na anatumia namba hizo kutapeli pesa kwa watu ambao majina yao yamo kwenye contact
list. Anawatumia watu meseji, hapigi wala hapokei simu anapopigiwa. Anadai
kwamba mimi nina shida naomba msaada na anapendekeza kiwango cha pesa za
kutumiwa.
“Wapo wachache ambao wameibiwa tayari na wengine walitaka
kuthibitisha kama ni mimi, wakapiga simu
hakupokea. Wanaojua namba zangu za simu wameniuliza kupitia simu yangu ya Voda,
wakagundua ni mtego wa tapeli. Kwa taarifa hii, nawajulisha wote wanaonifahamu
na wasionifahamu watakaoombwa pesa na mimi kutoka kwa yeyote, wasitoe kabisa.
Anayeomba pesa hizo si mimi, ni tapeli!”
Ujumbe wake huo ulizua maswali kwa baadhi ya watu ambao
walihoji ni kwa vipi matapeli hao waliweza kufahamu mpaka namba ya siri ya
M-pesa au Tigo-pesa yake kiasi cha kufikia kupokea fedha kupitia namba zake
hizo za simu?
Wengine walionyesha shaka, wakimuuliza ni kwa nini hakuwahi
kwenye kampuni za hizo simu kwenda kuzifunga na badala yake akaziacha kuendelea
kutumika?
Mmoja wa watu waliochangia katika ukurasa huo wa Facebook,
France Rubian, aliandika akihoji; “Da..! Muda wote huo kaka kwa nini ukae
kimya? Achilia mbali kuibiwa, mbona angeweza hata kukuharibia mambo mengine kama akiwa na nia hiyo? Hapa panazuka mjadala mreeeefu
usiokuwa na majibu sahihi. Simu imeibiwa, wewe kwa muda wa siku2 hujachukua
hatua, aliyeiba anaomba hela kupitia hizo namba zako, ‘password zako pia anazo
ndiyo maana anaweza kuchukua hela.... Mh! Kazi kwelikweli.”
Tambo za kiuchunguzi zilizofanywa na gazeti hili, zimebaini
kuwa moja ya namba hizo za Ngurumo, 0719 001 001 ambayo ndiyo imeandikwa kwenye
safu ya bodi ya wahariri kupitia gazeti analoliongoza la Tanzania Daima, hadi
jana ilikuwa inaonyesha kuwa imesajiliwa kwa jina la Subira Ramadhani.
Alipoulizwa Ngurumo kupitia simu yake ya kiganjani na
MTANZANIA Jumatano kuhusu uhusiano wake na Ludovick na iwapo ana ushirika naye
wowote wa kibiashara, alisema anamfahamu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, lakini hana
ukaribu naye sana
wala hashirikiani naye katika biashara yoyote.
Ngurumo alisema alimfahamu Ludovick akiwa katika harakati
zake za kisiasa mkoani Kagera, baada ya kuunganishwa na Mkurugenzi wa Ulinzi na
Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, aliyeeleza kuwa ni msaidizi wake wa
kisiasa.
“Nilimfahamu kijana huyu nikiwa katika harakati zangu za
kisiasa mkoani Kagera na nilifahamishwa kwake na Lwakatare, ni msaidizi wake.
Alianza kunizoea taratibu na baadaye aliniomba kunisaidia kazi za blog yangu
kwa madai kuwa hana kazi na alidai pia kuwa huwa anamsaidia Mjengwa kazi za
blog yake, lakini kabla sijaanza naye kazi akawa amekamatwa,” alisema Ngurumo.
Alipoulizwa mazingira yaliyosababisha amtumie fedha kupitia
simu yake ya kiganjani, Ngurumo alisema Ludovick alipata kumuomba fedha za
kumsaidia kuhama mahali alipokuwa akiishi, lakini alishindwa kumsaidia kwa
sababu hakuwa nazo na mara ya pili alimuomba Sh 50,000 baada ya kupata wageni
ghafla nyumbani.
“Aliniambia mama mkwe wake amekuja na hana hela, akaniomba
Sh 50,000, nikamwambia hizo nyingi sana ,
basi nikatafuta kiasi kidogo nikamtumia, sikumbuki nilimtumia Sh ngapi, lakini
nadhani ni Sh 20,000 au 30,000.”
Aidha, taarifa zaidi zinaeleza kuwa Balile, ambaye
aliteuliwa na Jukwaa la Wahariri kuwa mmoja wa wajumbe wa timu ya kuchunguza
tukio la kuvamiwa na kuteswa kwa Kibanda, amekuwa akifika ofisini kwa Ngurumo
na kufanya mazungumzo naye kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Balile, naye alipoulizwa kupitia simu yake
ya kiganjani kuhusu uhusiano wake na Ludovick, alisema alimfahamu kijana huyo
kupitia mawasiliano ya mitandao ya kijamii ambapo alianza kujenga naye ukaribu
kabla hawajaanza kuwasiliana kwa simu.
Balile alisema, Ludovick alimueleza kuwa anavutiwa na
uandishi wake wa makala na aliomba amfundishe kazi ya uandishi wa habari, jambo
ambalo hakuweza kulifanya kutokana na majukumu yake mengi.
Hata hivyo, alivyoulizwa iwapo amekuwa akimtumia fedha
Ludovick, alisema hajawahi kumtumia hata mara moja, licha ya kumuomba mara
kadhaa na kutaja mara ya mwisho aliyomuomba akiwa mkoani Iringa, kwa maelezo
kuwa alikuwa amekwama nauli ya kwenda Makambako, hivyo aliomba kutumiwa Sh
20,000 kwa ahadi ya kuzirudisha baada ya kurejea Dar es Salaam.
Alieleza zaidi Balile kuwa, alitafuta kiasi hicho cha fedha
kwa ajili ya kumtumia, lakini kabla hajatuma alipata taarifa kuwa amekamatwa na
polisi.
Alipoulizwa Balile iwapo amewahi kujadili mwenendo wa
mwandishi yeyote wa habari na Ludovick na hata kumpatia mawasiliano yake,
alikiri jambo na kueleza kwa ufupi kuwa ni kweli alipata kutoa mawasiliano ya
namba za simu ya mmoja wa waandishi wa habari kwa Ludovick, lakini baada ya
kupata habari za kukamatwa kwa mkanda wa Lwakatare, alishtuka na kuamua
kujipeleka mwenyewe polisi kueleza namna alivyotoa namba hiyo kwa Ludovick na
mambo mengine anayoyajua kuhusu Ludovick.
Vyanzo vingine vya habari vya MTANZANIA Jumatano vimeeleza
kuwa miezi michache kabla ya Ludovick kutiwa nguvuni akituhumiwa kushiriki
mipango ya kigaidi, alijaribu pasipo mafanikio kujenga uhusiano wa karibu na
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msaki.
Vyanzo hivyo vya habari vinamtaja Balile kufanya kazi ya
kuwaunganisha Ludovick na Msaki, vikidai kuwa ni Balile ndiye aliyempigia simu
Msaki kumtaarifu kuwa Ludovick ni kijana wake na ana shida ambayo Msaki anaweza
kuitatua, hivyo amempa namba yake ya simu ya kiganjani ili awasiliane naye.
Kwamba siku chache baada Msaki kupokea ujumbe wa Balile,
alipigiwa simu na Ludovick ambaye kwanza alimpongeza kwa uandishi mzuri wa
makala, kisha akamuomba awe mwalimu wake wa uandishi wa habari, jambo ambalo lilimshangaza
Msaki, kwa sababu haandiki makala magazetini na hivyo alimueleza kuwa taarifa
alizopatiwa siyo sahihi na kumkatia mawasiliano.
Mbali na Balile na Ngurumo, taarifa za kikachero zinaeleza
zaidi kuwa wapo pia baadhi ya waandishi wa habari wanaotajwa kuwa na
mawasiliano ya simu na Ludovick, jambo linalozua hofu kuwa Mtandao ambao
aliutaja Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema, Mabere Marando ni mkubwa na si tu
kwamba unaigusa serikali na CCM pekee, bali pia wanahabari na baadhi ya
wanasiasa.
Jumapili Aprili 14, Marando, alijitokeza mbele ya waandishi
wa habari na kutangaza orodha ya majina ya watu mbalimbali, wakiwemo viongozi
wa chama na serikali kuwa ndio wahusika wa mipango ya kishetani.
Miongoni mwa viongozi wa juu wa CCM waliotajwa na Marando ni
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Mwigulu Nchemba, aliyedai kuwa uchunguzi wake
ulibaini simu yake kufanya mawasiliano ya mara kwa mara kwa watuhumiwa wa
ugaidi. Hata hivyo, Mwigulu amekwisha kaririwa akieleza kuwa yuko tayari
kueleza kile anachokijua kuhusu mtandao wa ugaidi mbinguni na duniani.
Marando aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutokana na
uzoefu wa kazi yake ya ushushushu, amechunguza na kubaini kuwa watu hao
aliowataja ndio wahusika na vitendo viovu na kuahidi kuwa ataongoza jopo la
mawakili wa Chadema kumteteta Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho,
Wilfred Rwakatare, anayekabiliwa na tuhuma za kushiriki kupanga ugaidi
mahakamani.
Subscribe to:
Posts (Atom)