WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
HUYU NDIYE ALIYEMALIZA KAZI KABISA.....
Mwanamitindo bora wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Unique Model Photogenic Elizabeth Pertty (kushoto) na Unique Model Talent Vestina Charles mara baada ya kutangazwa kwa mshindi.
Mrembo Catherine Masumbiga jana usiku ameibuka mshindi kwenye shindano la Unique Model lililofanyika kwenye Klabu ya New Maisha jijini Dar es Salaam. Nafasi ya pili ilikamatwa na Cesilia Michael huku Amina Ayubu akikamata nafasi ya tatu
Washiriki
waliongia tano bora.
CHAMBO RABA RABA KUSHUSHA "DOUBLE- DROP"
Here we Go !!
Young Disturbing Artist RABA RABA Himself all the way from ROCK CITY, ameamua kupiga
“Double Droping” kunako mwezi wa Kwanza mwakani, yaani 2013, ambapo anatarajia
kudondosha Mkwaju wake mpya, utakaotoka katika Audio na Video kwa Wakati Mmoja.
Kupitia Account yake ya Facebook, Mkali huyo wa “raba raba”
amemwaga hadharani kuwa amekuwa Kimya kwa Muda Mrefu sasa, so anarudi kwa ujio
mpya kupitia Joint hiyo ambayo ataidrop kwa Mpigo na Video Yake. Jamaa mwenyewe
kamwagika hivi :
“Sasa kwa kipindi kirefu nilikuwa Kimya. Narudi kwa ujio
mpya. Napenda kuwaamba mashabiki zangu hasa pande za kanda ya ziwa, mwezi ujao
natambulisha ngoma yangu mpya ambayo naamini mtaelewa nini nafanya. Nashusha
mzigo kwenu Audio pamoja na video kwa pamoja. Napenda kuwaambia ni bonge ya
ngoma zaidi ya ngoma ya kwanza iliyokuwa inatambulika kwa jina la RabaRaba. Kaeni
tayari kwa ujio huu. Nawapenda shabiki zangu.”
TUNAUNGANA NA WANANCHI WA INDIA KATIKA MAOMBOLEZO YA MWANAMKE ALIYEBAKWA
Hivi Sasa Wananchi wa India hasa Wanawake, wapo katika Maombolezo mazito, baada ya Mwanamke aliyebakwa December 16,2012 na kusababishiwa majeraha na Maumivu makali, kufariki Dunia mapema leo hii.
www.joachimjunior.blogspot.com, inaungana na Wananchi wa India duniani kote kuomboleza Msiba huo uliosababishwa na Unyama Mkubwa.
Tuko pamoja kuhakikisha kuwa Unyanyasaji wa Wanawake Duniani kote unakomeshwa.
Mwenyezi Mungu aliaze Roho ya Marehemu Mahali pema Peponi, Amen
BWANA AMETOA, NA BWANA AMETWAA..JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE , AMEN
Imetolewa na
Frank Magnus Joachim
C.E.O
MAANDAMANO YA AMANI YAFANYIKA INDIA
Maelfu ya watu wamejiunga katika
maandamano ya amani katika mji mkuu wa India, Delhi, kupinga kitendo
kilichosababisha kifo cha mwanamke mmoja ambaye alibakwa na kundi la wanaume
mjini humo.
Mwanamke huyo mwenye umri wa
miaka 23, ambaye bado hajatambuliwa, amekufa kutokana na na majeraha Jumamosi
huko Singapore alikopelekwa kupata matibabu maalum.
Wanaume sita wanaoshikiliwa
kuhusiana na tukio la kumbaka mwanamke huyo, sasa wamefunguliwa mashitaka ya
mauaji.
Shambulio hilo la aibu
lilifanyika tarehe 16 Desemba 2012 na kusababisha maandamano kupinga
unyanyasaji wanaofanyiwa wanawake nchini India.
Maafisa wawili wa polisi tayari
wamesimamishwa kazi.
Mwili wa mwanamke huyo
unarejeshwa India katika mazishi yatakayofanyika kwa siri kuepusha ghasia zaidi
za waandamanaji.
"Kwa kweli wanawake wengi
nchini India wanakabiliwa na kitisho katika maisha yao katika mambo mbalimbali
kama vile kunapozuka ghasia, ukosefu wa huduma za afya, kukosekana kwa usawa,
kupuuzwa, lishe duni, kutojaliwa kwa afya ya mtu na utu wake"
Polisi wa kuzuia ghasia wamefunga
eneo la katikati ya Delhi ili kuzuia maandamano zaidi.
Waziri mkuu wa India Manmohan
Singh amesema anaelewa hasira ya wananchi, ametaka hatua zaidi zichukuliwe ili
kufanya India kuwa mahali salama kwa wanawake kuishi.
Maandamano pia yamefanyika katika
miji mingine ya India ikiwemo Calcutta, Bangalore na Mumbai.
Mwandishi wa BBC, India anasema
kwa zaidi ya wiki mbili, mwanamke huyo ambayo hajatambulishwa amekuwa ishara ya
mateso makubwa wanayopata wanawake wengi nchini humo.
Amesema, hata baada ya mazishi,
mawazo yataendelea, kwa wananchi kuisukuma serikali kuchukua hatua kuhakikisha
namna haki za wanawake zinavyoweza kulindwa.
CHANZO: BBC NEWS
Subscribe to:
Posts (Atom)