IKO HIVI...
Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Henry amejikuta mikononi mwa vyombo vya
dola baada ya kumchoma mkewe sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia pasi na kumuua mtoto wake wa
mwaka mmoja kwa madai kuwa
mwanamk huyo amekuwa akitoka kimapenzi na baba yake mzazi........
JAMAA ANAVYOSEMA
Akiongea kwa majuto makali huku akiwa "nyuma ya
nondo", Henry anadai kuwa alifanya hivyo bila kukusudia
"Nakiri kwamba nilifanya maamuzi ambayo sikutegemea
kuyafanya katika maisha yangu.Nilikuwa napandwa na hasira kubwa kila nikimuona yule mtoto akiamka na
kulilia maziwa .
Moyo ulikuwa ukijaa nakunifanya nishindwe hata kupumua
na ndipo siku moja ndani ya moyo
wangu nilisikia sauti ikiniamuru nimuue
yule mtoto maana si damu yangu.
Bila kujizuia, nilimshika shingoni, nikamkaba na
kumpiga kwa nguvu......." Henry
alielezea tukio hilo huku aimwaga machozi
ya uchungu
"Najua kuanzia
sasa maisha yangu yatakuwa ni gerezani tu.Nakubaliana na yote ila nimeona ni bora jamii
iujue ukweli.......
Mtuhumiwa, HENRY
HAYA.....IMEKUWAJE KUWAJE?...HEBU TUPE KISA KAMILI KAKA KATILI
Mke wangu Mercy alikuwa na mahusiano ya
kimapenzi na baba yangu mzazi .Kabla ya tukio hili, nimekuwa nikimuonya mara nyingi sana kwamba aache tabia hiyo na asiende nyumbani kwa baba maana nilikuwa nimeshausoma mchezo huo.Mbaya zaidi mke wangu
hakutaka kunisikiliza.....
Siku moja mke wangu aliaga kuwa anataka kwenda kwa rafiki yake.Nilimkataza
na kumwambia kuwa asitoke wala kwenda kokote lakini
hakunisikia.Baada ya muda kidogo nilizuga na kumwambia kuwa natoka kidogo.Baada ya nusu
saa nilirudi nyumbani na sikumkuta mke
wangu.....
....Nilisubiri kidogo huku akili ikiwa haifanyi kazi.Baadaye
moyo ulinituma kuwa niende kwa baba
nikamuangalie maana si mbali sana kutoka nyumbani........
Nilifika na kugonga mlango.Baba alitoka akiwa amejifunga
taulo tu.Nilipojaribu kuingia ndani
alinizuia.Baada ya kuzozana naye kwa muda
niliamua kuacha na kurudi
nyumbani.......Sijui mke wangu alitorokaje
na kuniwahi kufika nyumbani,
lakini niliporudi nilimkuta ameshafika.
Badala ya kuchukia,
nilijikuta nacheka sana .yaani nilikuwa kama mtu aliyerukwa na
akili.Nilijisogeza pembeni na kuanza
kuvuta sigara ili kupunguza hasira......
Ilipofika usiku, nilichukua nguo yamteja wangu na kuanza
kuipiga pasihuku nikiwa na mawazo mengi.Baadae nilisikia sauti ndani ya moyo wangu ikiniambia nijikaze japo nimulize ili niujue
ukweli.Wakati huo pasi ilikuwa ni ya moto kwelikweli. Ghafla maamuzi yakaniijia
kuwa niitumie ile pasi kumtisha ili aniambie ukweli wa tukio zima......
Nilimsogelea na kumwamsha.Alipoamka nilimuomba anieleze ukweli tena
kwa nia nzuri kabisa.Mercy hakunijibu kitu
na badala yake alikaa kimya.Nilijawa
na hasira na kujikuta namchoma
kwa kutumia ile pasi
Nilipofanya vile,Mercy alikiri kuwa amewahi
tembea na baba yangu mara tatu.....Aliposema vile hasira zilinipanda
zaidi na kujikuta namchoma zaidi......
Wakati nafanya vile,mtoto aliamka na kuanza kulia kama ishara ya
kutaka kunyonya.Nilimwangalia kwa hasira
huku moyo ukiniambia kuwa yule si mwanangu...."
Henry alikaa kimya
kwa muda huku akiwa amejiinamia.Baada ya muda kidogo
alinyanyua kichwa na
kuangalia juu huku
uso wake ukiwa umelowa machozi....
Baada ya kimya cha muda, Henry aliendelea kwa kusema kuwa:"Yalikuwa ni
maamuzi mabaya sana.Wakati yule
mtoto akilia, nilimshika na kumkaba
shingo.Baada ya kumkaba nilimpiga kwa ngumi.
Wakati najiandaa kumpiga mara ya pili, mke wangu aliudaka
mkono wangu.Nilipoona ameshika mkono, nilitumia mkono mwingine kumuunguza
zaidi huku mkono mwingine ukiendelea kumpiga mwanangu.....Mwanangu hakuweza kutoa sauti tena."Alimalizia
Henry huku akilia kwa sauti kubwa