REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

Misa Wapinga kufungiwa Kwa Gazeti la Mwanahalisi

5:15:00 AM Add Comment





Na Frank Joachim
Taarifa Kwa Umma
Kitendo cha kulifungia gazeti la MwanaHalisi kwa muda usiojulikana kinaweza kusababisha hofu kubwa kwa watetezi wa haki za binadamu na wanahabari kwa ujumla. Kitendo hicho kinafuatia kile cha kuwakamata na kuwaweka rumande (Oysterbay Polisi) wanaharakati zaidi ya kumi kwa tuhuma mbalimbali ikiwamo kuandamana kufuatia mgomo wa Madaktari mnamo tarehe 9 mwezi Februari 2012.

MISA –Tanzania inalaani vikali matumizi mabaya ya Dola katika kunyamazisha wanahabari wanapojaribu na kuthubutu kufuatilia matukio mbalimbali na kuarifu umma kuhusu yale waliyoyafanyia kazi kwa kina. Ni rai yetu kwa serikali kuwa ni vyema wabainishe taarifa mahsusi zilizopelekea maamuzi ya kufungia gazeti la MwanaHalisi ili kutuondolea hofu sisi tunaotetea haki na uhuru wa vyombo vya habari. Kuendelea kuficha taarifa husika ni kuendelea kuikanyaga Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (ibara ya 18) kupitia kivuli cha Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ambayo kimsingi imepitwa na wakati na haiwezi kutumika kinyume na Katiba ya nchi.

Ni rai yetu pia kwa serikali ya Tanzania kwamba izingatie Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika yale yenye kuhamasisha utoaji haki kuliko kujikita kwenye kifungu cha 30 cha Katiba hiyo ambacho kimsingi kinaweka mipaka maalumu ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Mipaka hiyo haionekani kuzingatiwa na serikali katika kulifungia gazeti la MwanaHalisi.

Kwa taarifa hii kwa umma, tunaiomba pia serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulifungulia gazeti la MwanaHalisi mapema iwezekanavyo na bila masharti ili kuwawezesha watanzania kuendelea kunufaika na taarifa zinazochapishwa na gazeti hilo ilmradi maadili ya uandishi wa habari yazingatiwe. 

Hii ni haki ya msingi kwa kila mtu na ni vyema aione ikitekelezeka.

Taarifa hii imetolewa na kusaini hapa Dar es salaam leo tarehe 31 Julai 2012.

Mohammed Tibanyendera
Mwenyekiti, MISA-TAN

JK KULIHUTUBIA TAIFA LEO

5:11:00 AM Add Comment



                 Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

Na Frank Joachim
Dar es Salaam, Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alasiri ya leo, Jumatano, Agosti Mosi, 2012, atazungumza na Taifa kupitia Mkutano wa Waandishi wa Habari utakaofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo utakaoanza saa 10 kamili utahudhuriwa na Wakurugenzi Wakuu, Wakurugenzi Watendaji, Wahariri Wakuu na Wahariri Watendaji na utatangazwa moja kwa moja na televisheni nchini.

Ugonjwa Wa Ebola uko Uganda Magharibi Tu.

4:58:00 AM Add Comment



 Na Frank Joachim
Kampala, Uganda
Nchini  Uganda , shirika  la  afya  ulimwenguni  limeripoti  kuwa  watu 36  upande  wa  magharibi  ya  nchi  hiyo  wanashukiwa  kuwa wanaugua  ugonjwa  wa  Ebola, ugonjwa  ambao  huambukiza  na ambao  umesababisha  vifo  vya  watu  14.

Wizara  ya  afya  nchini Uganda  imetangaza  rasmi  kuzuzka  kwa  ugonjwa  huo  katika wilaya  ya  Kibaale siku  ya  jumamosi  na  kusema  kuwa  watu  20 wameambukizwa. Shirika  hilo  la  afya  ulimwenguni , WHO, limethibitisha   kuwa  hakuna  mtu  aliyeambukizwa  nje  ya  wilaya hiyo  ya  Kibaale,  na  kwamba  haihitajiki  kwa  sasa  kuchukuliwa hatua  za  kudhibiti  biashara  na usafiri  kwendea  Uganda.

Hakuna matibabu  ama  chanjo kuutibu ugonjwa huo, na  ni  mara  ya  nne ugonjwa  huo  wa  Ebola  kuzuka  Uganda  tangu  mwaka  2000, ambapo  watu  224  walifariki.
4:51:00 AM Add Comment



Mji Mkuu Wa India, New delhi.
Moja kati ya Mitaa ya India.
 


 Na Frank Joachim & DW
NEW DELHI, India.
Umeme  umeanza  kurejea  asubuhi  ya  leo , jumatano, baada  ya majimbo  20  kati  ya  28  nchini  India , pamoja  na  mji  mkuu wa New Delhi,   kukumbwa  na  kukatika  kwa  umeme. 

 Magridi  matatu makuu kati  ya  matano  ya  kusafirishia  nishati  hiyo  yalishindwa kufanya  kazi. Hali hiyo ni ya  pili  kutokea katika  muda  wa  siku mbili, na imesababisha   zaidi  ya  watu  milioni 600  kubaki  bila umeme. Mfumo  wa  usafiri  ulishindwa  kufanyakazi, hospitali zililazimika  kutumia  umeme  mbadala  wa  genereta  na  mamia  ya wachimba  migodi  walikwama  chini  ya  ardhi  kwa  kuwa  lifti hazikufanyakazi.

 Matukio  hayo  mawili  yaliyofuatana  ya  kukatika  umeme  siku  ya jumatatu  na  jumanne  yamezua  wasiwasi  mkubwa  juu  ya  miundo mbinu   nchini  India  na  uwezo  wa  serikali  wa  kukabiliana  na mahitaji  ya  nishati  wakati  India  inajaribu  kuwa dola  kuu ya kiuchumi duniani.

MNADA BANNER