NDUGU Wa Abiria waliokuwa katika Ndege Hiyo,
walijikuta wakiwa katika hali hii baada ya kubaini kuwa Miili 40 imeonekana
katika Bahari
|
BLACK TOUCHEZ/BBC/DAILY MAIL
MIILI arobaini imeopolewa kutoka
baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji unaendelea,
ikiwa ni Kufuatia kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia, yenye namba
QZ8501At ,
Miili hiyo ilionekana ikielelea karibu na taka
za bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo, moja ya eneo la utafutaji mabaki
ya ndege hiyo.
Aidha taarifa kutoka serikali ya Indonesia
zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika ndege iliyopotea.
Moja Ya Vitu vinavyodhaniwa kuwa katika Ndege
Hiyo, kikielea Baharini
|
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa
imebeba abiria 162, ilikuwa ikitokea
Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore,lakini ilipotea siku ya JUMAPILI.
Utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo umeingia
katika siku ya tatu,na eneo la utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na
tatu hii inashirikisha nchi kavu na baharini.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari
uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka bahari
zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria ikielea majini.
KIFAA Hiki, inasadikika kuwa ni Mlango wa Ndege
hiyo, kikiwa katika maji
|
Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo
walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.Baadaye askari
wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini iliopolewa na
meli ya kivita .
Mkurugenzi mtendaji wa AirAsia Fernandes ali
ingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa ndugu waliopoteza
ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya shirika la ndege la AirAsia
ametuma salamu za rambi rambi .
Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo
unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.