Kauli hiyo ameitoa Jiji Mwanza wakati wa uwekaji
wa Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince
phamaceutical cha jijini hapa kilichopo katika Wilaya ya Nyamagana.
Ndikilo amesema haiwezekani hata ajira kama za
kukata majani badala yakuwapa wananchi wanaozunguka maeneo haya mkaenda
kutafuta mtu kutoka mbali, kwani kwa kufanya hivyo mtawafanya wananchi hawa
wasiwe rafiki wa kiwanda na wakati mwingine wanaweza kufanya uhujumu.
Katika hatua nyingine Ndikilo amewaomba mamlaka
ya Chakula na dawa nchini kuona uwezekano wa kukifanyia ukaguzi ili waweze
kukifungua kiwanda hicho mapema na shughuli za uzalishaji
ziweze kuanza mara moja.
" Ndugu zangu haiwezekani kila kitu kimekamilika
halafu wenzetu wa TFDA wanasema watakuja kufanya ukaguzi tarehe ishirini
na nane, alisema Ndikilo na kuongeza, lazima wafahamu kuanza kwa kiwanda ni
ajira, uzalishaji, ukuzaji wa uchumi n.k"
Huku akimtaka Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Chakula na dawa kanda ya Ziwa kuwasiliana na makao makuu kuona
uwezekano wa kufanya ukaguzi wa haraka na kukiruhusu kiwanda hicho kufanya
kazi.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa, alionya juu ya utunzaji
wa mazingira, ulinzi
wa kiwanda kwa wananchi wanaozunguka na kuhakikisha wakti
wote wanatoa ushirikiano kwa Mwekezaji.
Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda
hicho Prince Hetal Vithlani, ameupongeza na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa
Mwanza na wilaya kwa ushirikiano mkubwa waliompa tangu alipokuwa na dhamira ya
kuanzisha kiwanda hicho hapa mkoani,
Katika kuhakikisha anaunga mkono juhudi za
Serikali kuwaletea maendeleo wananchi, Mmiliki wa Kiwanda hicho
bw. ametoa Jumla ya Mifuko ya Sementi 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba
vya Maabara kwa Shule za Sekondari za Lwanyuma na Buhongwa, zilizopo wilayani
Nyamagana sehemu ambayo kiwanda hicho kipo.
Prince Phamaceutical ndicho kiwanda cha kwanza
na cha kipekee katika kanda ya Ziwa, ambacho mara baada yakuanza
kazi, kitakuwa Tegemeo kwa wananchi wa kanda ya ziwa na Mikoa ya Jirani na
kanda hiyo ikiwa ni pamoja na Nchi Jirani.
CREDIT: G-SENGO