NA GEORGE BINAGI,Mwanza
Kikao cha kwanza cha
baraza la Madiwani wa halimashauri ya Jiji la Mwanza, leo kimeanza rasmi huku
kikitumia baadhi ya kanuni mpya, baada yam kikao hicho jana kushindwa kufanyika
ili kupisha semna kwa wajumbe wa baraza hilo juu ya kanuni hizo mpya zitakazotumika
kuliongoza baraza hilo.
Miongoni mwa kanuni
mpya ambazo zimeingizwa na TAMISEMI katika vikao vya halimashauri zote hapa
nchini ni pamoja na kila diwani kuandaa na kuwasilisha mbele ya baraza taarifa
ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya Kata yake kabla ya kikao cha baraza
kuanza.
Kanuni nyingine ambazo
ni mpya zinahusu dua maalumu ya kuiombea halimashauri na kuimba wimbo wa Taifa
kabla ya vikao vya baraza la madiwani wa halimashauri kuanza, sanjari na
maswali ya papo kwa hapo kwa mwenyekiti wa baraza la madiwani ambae ni Mstahiki
Meya, ama kwa Mtendaji wa baraza ambae ni Mkurugenzi wa Jiji.
Kutokana na kanuni
hizo mpya, wajumbe wa baraza la madiwani waliafikiana hiyo jana kusitisha
shuguli za kikao cha kwanza cha baraza hilo ili kupata semna kuhusiana na
kanuni hizo ili kuwajengea uwezo na uelewa katika kuzitumia.
Kwa mantiki ,Kabla ya
kikao cha leo kuanza Redio Metro ilizungumza na baadhi ya madiwani ambao ni
wajumbe wa baraza hilo la madiwani wa halimashauri ya jiji la Mwanza ambao
wameeleza kwamba baada ya semna ya jana waliafikiana kwa pamoja katika kutumia
kanuni hizo mpya.
Baada ya kupata
ufafanuzi huyo nje ya Ukumbi wa halimashauri ya Jiji la Mwanza, uliwadia wakati
wa kikao hicho cha baraza la Madiwani kuanza, ambapo tulishuhudia kanuni mpya
zikianza kutumika rasmi, na hapa Mwenyekiti wa baraza hilo ambae ni Mstahiki
Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula aliwaongoza wajumbe katika kuimba wimbo
wa Taifa pamoja na dua maalumu ya kuimbea halimashauri kabla ya kikao kuanza
rasmi kama kanuni zinavyoelekeza.
Baada ya wimbo wa
Taifa na Dua kwa halimashauri, mwenyekiti alitoa mwongozo wa ajenda ya kwanza
ya kikao ambayo ni wajumbe wote kuzingatia suala la mavazi ambayo ni ya heshima
sanjari na majoho huku akibainisha kuwa mavazi na kofia za aina yoyote
havitaruhusiwa katika vikao hivyo.
Ajenda iliyofuata
ilikuwa ni madiwani kuwasilisha taarifa za shughuli za maendeleo katika kata
zao ikiwa ni utaratibu mpya kabisa kwa kuwa hapo awali utaratibu huo haukuwepo,
hali ambayo mwenyekiti amebainisha kwamba imepelekea madiwani kuwasilisha
taarifa zenye mapungufu na hivyo mwenyekiti kutoa pendekezo la kuwepo kwa semna
elekezi juu ya namna ya kuandaa taarifa hizo ambazo zitakuwa zikitolewa kila
baada ya miezi mitatu.