WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
MAUZO MABOVU YAWATENGANISHA MARIAH CAREY NA PRODUCER WAKE WA MUDA MREFU.
SUPER VOICE MAMITO Mariah Carey
ametemana na producer wake wa Muda Mrefu, JERMAIN DUPRI, baada ya Albam yake
kupata mauzo mabaya tofauti na ilivyokuwa imetarajiwa..TTM tunao Mtonyo Kamili.
Aidha inasemekana kuwa, Muimbaji
huyo Mwenye Umri wa Miaka 44 hivisasa, amefikia uamuzi huo mgumu dhidi ya
Jermaine Dupri, ambaye wamedumu katika kazi kwa Muda wa takriban Miaka 20, na kuamua
kuungana na Msimamizi Mwingine, KEVIN LILES.
Kwa mujibu wa Info ambazo TTM bado
tumezipata katika kukamilisha Data Hizi, inasemekana kuwa, wawili hao ambao
walianza kazi rasmi mnamo 1995, awali walienda vizuri na mafanikio makubwa sana
ikiwemo kufanya Hit single ya WE BELONG TOGETHER, lakini baada ya kuachiwa kwa
albam Mpya ya ME I AM MARIA, huwezi amini zimeuzika nakala 100,000 tangia Mwezi
May, mpaka hivi sasa.
Tofauti na Hilo, Pia Jermaine
aliwahi kuingia kunako Noma Nzito baada ya Kumuandalia Perfomance Mariah Carey,
juu ya Wanasiasa wa Angola, jambo ambalo lilipigwa Vita na Wanaharakati wa haki
za binadamu, kwa madai kuwa alifanya kitu kisicho kizuri hasa kwa Siasa
zinazokiuka haki za Binadamu.
HATIMAYE TUMEINYAKA TAREHE YA KUTOKA KWA MIXTAPE YA LIL KIM
LONG time sana tumekuwa tukisubiri
kwa hamu ujio wa Mixtape ya The Queen Bee, Lil Kim, na hata wengine kukata tama
kuhusu kuachiwa kwa Mixtape hiyo, hatimaye TTM tumeinyaka Tarehe ambayo Mzigo
huo unaingia Ofisini.
Kupitia account yake ya Twitter, Kim
ametangaza rasmi kuwa Mixtape Hiyo itaachiwa Rasmi SEPTEMBA 11, na watu wajipange
kuskiliza kile ambacho bibni huyo kakishusha baada ya kukaa kimya Muda Mrefu.
Mixtape hiyo, imepewa Jina la
HARDCORE 2K14, likiwa ni Jina amablo limewahi kutumika katika Moja ya Kazi zake
aliyoifanya Mwaka 1996, na ilikuwa ni Albam ya HARDCORE
Lil Kim Hivi sasa Ni mama wa Mtoto
Mmoja, na Wiki kadhaa zilizopita aliachia Remix ya Beyonce FLAWLESS na ya Bobby
Shmurda HOT FELLA (NIGGA).
Tofauti na Hizo, Lil Kim ameachia
Track ya Kumdiss Nicki Minaji inayokwenda kwa jina la IDENTITY THEFT
Subscribe to:
Posts (Atom)