WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
BABY JAY KAZUNGUMZIA SOKO LA ZANZIBAR LILIVYOCHINI, SABABU NA SURUHISHO LINALOHITAJIKA HARAKA IWEZEKANAVYO
Baby Jay : Instagram |
MKALI wa Miondoko ya Bongo Fleva Nchini tanzania, BABY JAY ambaye Maskani yake ni Zanzibar, amesema Kuwa, Soko la Muziki wa Kizazi Kipya katika Visiwa Vya Zanzibar (Tanzania Bara), kiujumla Liko Chini.
Bibie Huyo ambaye Hivi sasa Yuko Chini ya Said Fella, amedai kuwa, Kutokushikamana Baina ya Wasanii Wenyewe, imekuwa ni sababu moja Wapo ya Soko la Bongo Fleva "Kudorora" Visiwani Humo
#StoryOfMyLife : KUTANA NA HAWA, WALIOMSAIDIA CHAKULA NA MAHALI PA KULALA WAKATI ANASOMA SHULE YA MSINGI
Na Baba Juti
JAGUAR Kutoka Nchini Kenya kumbea aliwahi kukosa Nauli kwa ajili ya Kumpeleka Shuleni lakini huwezi amini kumbe kuna watu walikuwa wakimsaidia Kipindi hicho.
Kupitia Account yake ya Instagram, Hitmaker wa "KIGEUGEU" aliandika kuwa ameenda Kumtembelea Rafiki Yake kipindi cha Shule ya Msingi CAROL ambaye yeye pamoja na Ndugu yake EUNICE walikuwa wakimsaidia sana Kipindi hicho wakati anasoma Shule ya Msingi.
Jaguar ameongeza kuwa, walikuwa wakimsaidia Chakula, pamoja na Mahali pa Kulala hasa kipindi ambacho alikuwa akikutana na Uhaba wa Vitu Hivyo.
ULISHAWAHI KUJIULIZA KWANINI WASANII WA MUZIKI WA KIKE WA KIZAZI KIPYA WANAFELI KUANZISHA KAMPUNI ZA KIBIASHARA? CHEMICAL AMESEMA HAYA
INSTAGRAM: CHEMICAL |
FEMCEE Kutoka Nchini tanzania anayefanya Vizuri katika Soko la Muziki wa Hip Hop CHEMICAL MYSELF, amesema kuwa Wasanii Wengi wa Kike wanashindwa kuanzisha Kampuni zao za Kibiashara sababu soko la Muziki halijakaa sawa.
Akizungumza na HIT ZONE ya 93.7 Jembe Fm-Mwanza, Chemical amesema kuwa, wasanii Wengine Kama akina Nikki Minaj na wengineo, wanafanikiwa kuanzisha kampuni zao za Kibiashara, maana Muziki unawalipa
Pia Chemical ameongeza Kuwa, Nikweli Wasanii Wa Kike wanatakiwa Wasitegemee Muziki Tu, lakini Bado utabaki kuwa Mtaji hasa katika Kuanzisha shughuli Nyingine za Kibiashara
Kwa Upande wake, Chemical amedai kuwa, anaamini akishafanikiwa Kimuziki, ndipo atakapofikiria Biashara ya Kufanya, lakini hivi sasa, ni Mapema Mno Kusema
KALA PINA: TUTARAJIE KUSHUHUDIA VURUGU KUBWA BUNGENI HIVI SASA, MAANA WABUNGE WAMEAMKA, NA WANANCHI WAMEAMKA
Kala Pina |
KALA PINA Kutoka Kikosi cha Mizinga, amedai kuwa Amsha amsha ambazo zinaendelea Bungeni hivi sasa, tutarajie kuziona katika Awamu Hii ya Serikali ya Rais Magufuli.
Akizungumza hayo, Kala Pina amesema Kuwa, Hivi sasa Wabunge wameamka, halikadharika Wananchi Pia.
Tofauti na hayo kala Pina amedai Kuwa, laiti kama angekuwa Bungeni , Hakika angepigania Haki
NIKKI WA PILI: TASWIRA YA BUNGE HILI NI BUNGE LA KISIASA, NA SIO WANANCHI. (AUDIO)
NIKKI WA PILI (Picha Kwa Msaada wa Google) |
RAPA Nikki Wa Pili Kutoka WEUSI , amesema kuwa Taswira ya Bunge ambalo Linaendelea Hivi sasa Mkoani Dodoma, Ni Siasa, na Sio Maslahi ya Wananchi
Akizungumza na HIT ZONE ya 93.7 JEMBE FM -Mwanza, Nikki ameongea Masuala Mbali mbali Ikiwemo Demokrasia ambayo Serikali inatakiwa Kusimamia , Na Mfumo ambao Wananchi Tunaweza kuutumia hasa baada ya Kubaini kuwa Wabunge fulani, wanapigania Maslahi yao na hata Chama Chao
MSIKILIZE HAPA
Subscribe to:
Posts (Atom)