WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
HIVI NDIVYO MSANII DIAMOND PLATNUM ALIVYONG'ARA KWENYE TUZO ZA NZUMARI 2012 (NZUMARI AWARDS 2012), NCHIN KENYA, KAMA "MSANII BORA WA KIUME"
HIVI NDIVYO MUHAS ITAKAVYONG'ARA...
- NI KATIKA KAMPASI (CAMPUS) MPYA YENYE KUVUTIA
Michoro ya ujenzi wa Kampasi ya Mloganzila iliyo kijijini
Kwembe katikati ya Wilaya za Kisarawe Mkoa wa Pwani na Kinondoni Mkoa wa Dar es
salaam.
Hii ni sehemu ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
inayojengwa kwenye eneo la ekari 3800 kwa ajili ya kutolea mafunzo kwa
wanafunzi wa udaktari na huduma za Afya wapatao 15,000 kwa mwaka, na pia itakua
sehemu ya kutolea matibabu ya maradhi yote makuu na ya kawaida nchini. Kwa
mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, ujenzi
wa Hospitali hii, ambayo pesa ya ujenzi wake imeshapatikana, unatarajiwa kuanza
mwishoni mwa mwezi Januari, 2013 na unatarajiwa kukamilika miaka miwili baada
ya ujenzi kuanza. Kwa maneno mengine Kampasi ya Muhimbili ya Mloganzila
inategemewa kuanza kazi mwanzoni mwa mwaka 2015.
Tayari wataalamu na
wafanyakazi wanaotarajiwa kufanya kazi katika kampasi ya Mloganzila wameshaanza
mafunzo ndani na nje ya nchi. Mara hospitali hiyo kubwa na ya kisasa
itakapokamilika itakua na uwezo wa vitanda vya kulaza wagonjwa mia sita (600).
Sambamba na kampasi ya MUHAS ya Mloganzila pia ujenzi wa Kampasi ya Afya ya
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) umeshaanza na kufikia hatua ya juu na ambapo pia
hospitali hiyo inatarajiwa kuanza shughuli zake rasmi mwaka 2015.
Kwa mujibu wa
Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw.
Emmanuel Humba mchakato wa kufanikisha uanzishaji wa Chuo Hospitali hiyo
vimeshaanza ambapo baadhi ya wataalamu wakiwemo Madaktari na watumishi wengine
wako nchini na nje ya nchi kwa ajili ya masomo na mafunzo mbalimbali.
Chuo
hicho kinatarajia kuwa na vifaa vya kisasa vya tiba vinavyokidhi mahitaji ya
Afya na Elimu ya Udaktari wa kiwango cha Kimataifa, ikiwa ni mikakati kabambe
ya serikali ya awamu ya nne katika kuhakikisha nchi ina wataalamu wengi na
huduma za kisasa za afya ili kuondokana na adha ya kupeleka wagonjwa nje ya
nchi kwa ajili ya matibabu. Kwa sasa MUHAS inachukua takriban wanafunzi 2442 wa
udaktari na huduma za afya kwa mwaka.
Hivyo ujio wa kampasi ya Afya Mloganzila
na Kampasi ya afya ya UDOM utaharakisha mpango wa serikali wa kupunguza wastani
wa wagonjwa kwa daktari mmoja kwa kiwango kikubwa. Hivi sasa wastani ni daktari
mmoja anahudumia wagonjwa 30,000.
IVORY COAST yaingiwa Na Utata
Serikali ya Ivory Coast imeingiwa na kiwewe juu ya
kutekeleza agizo la Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC la kumkabidhi mke wa
Laurent Gbagbo Rais wa zamani wa nchi hiyo, kwa kuhofia kuvurugika mapatano ya
umoja wa kitaifa nchini humo.
Taarifa zinasema kuwa, hatua ya kukabidhiwa
Simone Gbagbo kwa Mahakama ya ICC itaitumbukiza nchi hiyo kwenye hatari zaidi
serikali ya Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast.
Taarifa hizo zinasema kuwa,
Rais Ouattara yuko njia panda kati ya kutekeleza agizo hilo la kimataifa na
kuitumbukiza nchi yake kwenye mfyatuko na mpasuko.
Mahakama ya ICC imeeleza
kuwa, Simone Gbagbo ana kesi ya kujibu kwani anakabiliwa na tuhuma za kutenda
jinai dhidi ya binadamu kuanzia tarehe 16 Oktoba 2010 hadi Aprili 12, 2011
nchini humo. Waranti uliotolewa na ICC wa kutiwa mbaroni na kukabidhiwa mke wa
Rais wa zamani wa Ivory Coast umekabiliwa na upinzani mkali kutoka Ivorian
Popular Front FPI chama kikuu cha upinzani nchini humo.
Subscribe to:
Posts (Atom)