WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
NIPE FAGIO PROJECT: Washiriki wa Miss Utalii Taifa Waungana na Meya Kufanya Usafi Jijini DSM
TUKO BIZE: Walimbwende hao wakiwa katika zoezi la kuokota taka, huku wakiwa wameambatana na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (Mwenye Suruali ya Khaki)
TUNAPENDEZA : Washiriki hao wakiendelea na zoezi lao
DUH SIO KAZI RAHISI..NGOJA TUWEKE POZI KWANZA : Washiriki hao wakiwa katika Picha ya pamoja na Meya wa Ilala, Jerry Slaa
YEEEEEEES : Washiriki hao wakiwa wamenyoosha mikono kuashiria wanashangilia jambo
CONFIRMED: RADI YAUA WATANO MBEYA
WATU watano
wamefariki dunia mkoani Mbeya kwa kupigwa radi katika matukio matatu
tofauti likiwemo lililoua ndugu watatu wa familia moja.
Ndugu hao
watatu wakazi wa kata ya Nyimbili wilayani Mbozi wamefikwa na mauti
Februari 5 mwaka huu majira ya saa saba mchana wakati mvua kubwa
iliyoambatana na radi za mara kwa mara ikiendelea kunyesha wakiwa
nyumbani.
Afisa
mtendaji wa kata ya Nyimbili Lingtone Nzowa amewataja waliopoteza
maisha kuwa ni Jerumana Halinga(35),David Halinga(5) na Kumi
Halinga(3) ambapo pia radi hiyo imemjeruhi mtoto wa miezi tisa ambaye
jina lake halikufahamika mara moja.
Tukio la pili limetokea katika
kijiji cha Magurula kata ya Utengule Usangu Wilayani Mbarali ambapo
radi iliyotokana na mvua kubwa imempiga Kasim Sagutangu na
kusababisha kifo chake ambapo diwani wa kata hiyo Juntwa Mwalyaje
amesema mvua hiyo imenyesha Februari 3 majira ya saa nane za mchana.
Tukio la tatu limetokea februari 3 katika kijiji cha Mbagala Kata ya
Ilembo wilayani Mbeya ambapo mwanamke Kotanida Petro amefariki dunia
baada ya kupigwa na radi akiwa shambani kwake. Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio hayo
ya vifo vya watu watano vilivyotokana na radi.
Subscribe to:
Posts (Atom)